Msondo Yasaka Mbadala wa Gurumo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msondo Yasaka Mbadala wa Gurumo

Discussion in 'Entertainment' started by kilimasera, Dec 23, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  BENDI kongwe ya muziki wa dansi ya Msondo Ngoma inasaka mwimbaji atakayechukua nafasi ya mwimbaji na kiongozi wa bendi hiyo, Muhidin Maalimu Gurumo ambaye ni mgonjwa.
  Meneja wa Msondo Said Kibiriti alisema kuwa Gurumo aliyelazwa katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, atakapotoka hospitali atalazimika kuwa nje ya jukwaa kwa muda mrefu ili kuweza kurudisha afya yake vyema.

  Gurumo amelazwa hospitali ambapo anasumbuliwa na matatizo ya mapafu kujaa maji.

  "Unajua kazi ya muziki ni ngumu. Gurumo hata atakapotoka hospitali tutahakikisha kuwa tunampa muda zaidi wa kupumzika na kurudisha afya yake. Kwa hiyo katika kipindi hiki tunahitaji kupata mbadala wake,' alisema Kibiriti.

  Kibiriti alisema kuwa mwanamuziki wanayemuhitaji ni yule mwenye uwezo mkubwa wa kuimba na kufanya kazi hiyo kwa muda mrefu bila ya kupumzika.

  Wakati huo huo bendi hiyo imekamilisha nyimbo zake nne zitakazokuwemo kwenye albamu yao mpya inayotarajiwa kukamilika mwezi Januari mwakani.

  Nyimbo hizo ni Baba Kibebe,Lipi Jema zilizotungwa (Eddo Sanga), Dawa ya Deni Kulipa 'Papa Upanga' na Kwa Mjomba Hakuna Urithi' (Huruka Uvuruge).

  "Tunatarajia kukamilisha nyimbo mbili mwezi huu na Januari tutaanza zoezi la kurekodi," alisema Kibiriti.
   
 2. Mzalendo Mkuu

  Mzalendo Mkuu JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 737
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Wajaribu tu. Vipaji vipo vingi ila vimejificha sana. Wajaribu kufanya kama Bongo Star search watafanikiwa. Style hiyo pia iliwahi kutumiwa na Clouds Fm wakati walipotafuta vijana wa kutangaza Africa Bambata siku za nyuma kidogo. Alipatikana kijana ambaye alikuwa mzuri sana ingawa siku hizi simsikii tena. Vipaji vipo watafute tu.
   
Loading...