Ado Shaibu
Member
- Jul 3, 2010
- 99
- 108
MSOMI WA UDSM ATABIRI KIFO CHA CUF 2020
Mwanazuoni kutoka Idara ya Fine and Performing Arts ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dk. Charles Kayoka amesema Chama cha CUF kitadhoofika ifikapo mwaka 2020 kutokana na kupukutikiwa na viongozi na wanachama wake waliojiunga ACT Wazalendo kumfuata Maalim Seif.
Dk. Kayoka amesema hali aliyojionea Zanzibar ambako alitembelea hivi karibuni CUF imeshafutika. Kayoka alitoa mfano wa Stone Town kulikoshamiri bendera za CUF lakini hivi sasa hazizidi mbili.
Kwa upande wa Zanzibar, amesema hakuna Mbunge wala Mwakilishi ambaye anaweza kushinda ubunge kwa CUF kwa sababu "ACT Wazalendo hivi sasa ndio habari ya mjini".
Amesema baada ya uchaguzi mkuu wa 2020 CUF kitapoteza ruzuku na kushindwa kujiendesha.
Kayoka amesema ACT Wazalendo kina uwezekano mkubwa wa kukua na kupata wabunge wengi Zanzibar na kwenye baadhi ya maeneo ya bara.
Sikiliza mahojiano yote aliyoyafanya na Icon TV