Msomi ni yupi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msomi ni yupi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sumbalawinyo, Jun 15, 2010.

 1. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #1
  Jun 15, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Mara nyingi hapa kwetu Tanzania tumekuwa tukisikia kuwa wanafunzi wa chuo kikuu wakiitwa wasomi.
  Je msomi ni yupi haswa? Kweli mtu ambaye hana hata cheti wala hajafaulu mitihani yake ya mwisho anastahili kuitwa msomi?
  Mi naona wasomi waitwe wale tu ambao wamesha graduate kuanzia level ya degree.
  Wanafunzi waishie tu kuitwa wanafunzi wa chuo.
  Pole sana madenti mnaopenda kuitwa wasomi
   
 2. minda

  minda JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  wivu tu unakusumbua umekimbia umande sasa umefulia hadi akili. "msomi" kama neno linavyojieleza ni anayesoma na si aliyehitimu.
   
 3. m_kishuri

  m_kishuri JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2010
  Joined: Jan 27, 2010
  Messages: 1,489
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hakika hiki ni swali gumu sana kulijibu, haswa ukuangalia viongozi wetu hapo nyumbani ambao wapo kwenye hilo daraja la usomi, lakini matendo yao hayaendani na usomi wao. Ninavyofahamu mimi ni kwamba elimu inatakiwa ikukomboe, iwe taa, na ikubadilishe kuelekea kwenye hali bora, hata kama ni elimu ya secondari au college. Lengo hilo lisipofanyikiwa, ina maana elimu haikufanya kazi yake, hata usome mpaka mwisho wa madarasa. Nikichukulia mfano wa viongozi wawili waliokuwa madarakani nchini mwetu katika vipindi tofauti, yaani Rais Mkapa na Dr.Andrew Chenye (Mwanasheria Mkuu), hawa wote ni maalumni wa HAVARD University, vyeti vyao ni FIRST CLASS. Lakini tumeshuhudia yaliyotokea katika utendaji kazi wao. Hivi karibuni nimesikia kwamba gari ambayo bwana Chenge alipata nayo ajali, ambayo ilopoteza maisha ya wasichana wawili, haikuwa na bima! huyu ndio mwanasheria mkuu wa serikali, sasa hapa usomi uko wapi? Ni Afadhali hata yule ambaye aliishia darasa la nane la mkoloni, lakini anauchungu na nchi yake, watu wake, na anafata sheria za nchi, kuliko WASOMI ambao wanafikiria matumbo yao na account zao za nje.
   
 4. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  aha, toka lini madenti hasa wa udsm na udom wakawa wasomi? hao ni "wasomi watarajiwa" sio wasomi kamili....ndo maana hawajui hata kinachoendelea duniani,....kwenye kampeni hizi watasukuma gari ya kikwete akiwatembelea wakati bumu linabana....sasa utamwita mtu msomi wakati hana pulani kumkichwa bado...hao ni watoto kwanza hata kujitegemea hawawezi, ndo maana wanapeperushwa na ccm vyovyote ipendavyo....usiharibu sifa ya wasomi halisi bwana, dah!
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  Hata mimi nilishajiuliza swali hili, nikapata mawazo tofauti.

  1. Hao wanafunzi wa chuo kikuu si wasomi in the sense ya "intellectual".
  2. Wanaweza kuwa wasomi kwa usomi tofauti, wa kiswahili, ambao haujawa translated kutoka "intellectual" kwa maana ya kwamba kazi yao kwa sasa ni kusoma/ kujifunza. Kwa definition hii usomi ni sawa na uanafunzi.

  Lakini nafikiri a more convincing reason ni kwamba.

  3. Tanzania wasomi proper ni wachache, hata kama unaamua kuwaita university graduate wote kwamba ni wasomi (ingawa si wote intellectuals), watakuwa wachache. Kwa hiyo kama wanavyosema, in the land of the blind the one eyed is king, kwatika nchi ambayo watu wanaohitimu A-Level ni wachache, wanaokuwa angalau wamefanikiwa kufika chuo kikuu, regardless ya kwamba hawajafaulu, wanaonekana kama washaingia katika kundi la wasomi.

  Tukiongeza namba za wahitimu wa chuo kikuu, hata hao wahitimu tutawachuja na kusema katika waliohitimu fulani ni msomi na fulani si msomi.

  Tukipunguza wahitimu mpaka wa form four, hata hao wa form four wataonekana wasomi. Hii label ya usomi inavyotumika bongo ni relatively sana. Ama sivyo tungekuwa na "wasomi" wa kuhesabika.
   
Loading...