Msomi ni nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msomi ni nani?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MTENGETI, Jun 4, 2012.

 1. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,330
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  wanabodi salaam sana.
  Kuna swali kila siku najiuliza nafikiri nikiwashirikisha majibu nitayapata leo.
  Jana kwenye Taarifa ya Habari ya saa mbili Usiku wanafunzi wa Vyuo vikuu ambao ni wanasisiem walikuwa wakiongea na Bwana January Makamba wakitoa matamko mbalimbali kuhusu chama chao cha CCM.ku
  na neno waliokuwa wanalitumia sana kuwa " eti wao Wasomi" hawaridhishwi na mwenendo mzima wa Chama Chao.
  Neno wasomi ndo linanipa shida kidogo.
  Hivi watu kama Dr. slaa,Dr. Harison Mwakyembe,Tundu Lisu,Issa Shifji na wengine wengi ambao leo tunajivunia matunda ya elimu zao tutawaitaje!. Kama watu waliopo shuleni ambao bado hawajahitimu na kuonesha product za elimu yao nao wanajiita wasomi?
  MI naona hawa tuwape jina linalowastahili yaani WASOMAJI. Je Wewe utawaitaje? natoa hoja
   
 2. m

  mharakati JF-Expert Member

  #2
  Jun 4, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  usomi ni kiswahili ikiwa na maana ya Elite kwa kiingereza ..hawa wanafunzi wa elimu ya juu kwa nchi maskini kama yetu ambayo wananchi wengi hawapati fursa ya kufika huko wanawekwa kwenye kundi la watu elite kwenye jamii na hapo ni wasomi..

  usishangae ukiongea na Prof Baregu, Mvungi, Mwandosya, au Dr Mwaky wakakueleza kitu cha kijamii kisicho na utaalamu mahsusi na ukawa huelewi wakasema wewe unashindwa kuelewa na usomi na upeo wako wote..
   
 3. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #3
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Wasomi ni wale waliofunuliwa ufahamu. Sio lazima uwe umesoma degree. Watu kama kina Rejao , Tume ya katiba , ritz sio wasomi kwakuwa hawana ufahamu.
   
 4. KML

  KML JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 863
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  wangekua wasomi wasingekua CCM hao,huwezi ukajiita msomi alafu una kadi ya ccm.hao ni wakamilisha ratiba vyuoni.
  ebu tujue perfomance yao kama inawezekana
   
 5. u

  umsolopagaz Member

  #5
  Jun 4, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nadhani msomi, ni yule aliye ktk mchakato mzima wa kusoma...tofautisha na mhitimu...kubwa kabisa..yule aliejaaliwa kuwa msomi wa kiwango cha kutukuka huwa na sifa ya kutokuwa na dharahu...hususan kwa watu ambao hayuko nao ktk taasisi yake anayofanyia mchakato wake wa kusoma, akitambua kuwa kusoma kwa kiasi kikubwa ni kujifunza kwa kuishi...anaetambua, msomi ni yule anaeishi maisha yake yote, akijifunza...hususan mwenyewe, na akiheshimu wasomi wengine wanaojifunza wenyewe na kazi zao..shaaban roberts wa tanzania, ni mfano mmoja...na wengine wengi wapo..msomi hana kibri....! na ana heshima, na ana ushujaa wa kuukubali ukweli...kinyume cha hapo, ni kinyume cha msomi...tuseme ni limbukeni wa kitu kidogo alichomaliza kujifunza na nachobakia anakimiliki kwenye mawazo yake tu.
   
 6. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #6
  Jun 4, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  UMEMSAHAU aLLY KOMBO AMBAYE AMEJAA ELIMU AKHERA KICHWANI hahahahah
   
 7. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #7
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  CHADEMA akili zao kama Mama Mushumbushi tu.
   
 8. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  .....mwenye kuleta mabadiliko chanya katika jamii(huyo ndiye Msomi).
   
 9. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #9
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  .....mwenye uwezo wa kuleta mabadiliko chanya katika jamii(huyo ndiye Msomi).
   
Loading...