Msomi gani wa kujivunia nchi hii na amefanya nini?

Safety last

JF-Expert Member
Mar 24, 2011
4,227
1,389
Ukiwa msomi ,ingawa bado sijui usomi unaanzia wapi na kuishia wapi,hii nchi ina wasomi gani wa kujivunia kwa waliyolifanyia taifa,maana kumezuka dhana siku hizi watu wenye elimu ya kawaida wakifanya mambo yenye tofauti chanya wanabezwa hawana shule,Nani msomi tanzania na usomi ni nini???

Wasomi.....wale wanaoitwa na vyombo vya habari kupata maoni yao kuhusu mwenendo wa kisiasa wa nchi hii na kama bunge la sasa linaendesha mabo kistaarabu.....na wale wanaotumiwa na CCM kutafuta opinion polls kuelekea uchaguzi kama vile REDET na wengineo. Hao ndio wasomi wa nchi yetu.

Msomi ni mtu yule ambae hajakimbia Umande!Sijajua unataka wa Kujivunia katika lipi!
Ila wasomi wamejaa kuanzia vijana mpaka wazee!Wengine wapo-makazini na wengine wapo Mtaani!

anayejua kusoma na kuandika...na anayekutumia kujua huko kwa maslahi ya jamii yake.

Msomi ni yule angalau aliyefikia elimu ya chuo kikuu na mwenye uwezo wa kupambanua mambo kwa kina.

Ukiwa msomi ,ingawa bado sijui usomi unaanzia wapi na kuishia wapi,hii nchi ina wasomi gani wa kujivunia kwa waliyolifanyia taifa,maana kumezuka dhana siku hizi watu wenye elimu ya kawaida wakifanya mambo yenye tofauti chanya wanabezwa hawana shule,Nani msomi tanzania na usomi ni nini???

Mkuu, post yako inamaswali kama 4 ya msingi :-

1. Msomi gani wa kujivunia Tz?

2. Amefanya nini?

3. Nani msomi Tanzania?

4. Usomi ni nini?

Tatizo maswali hayo hayako kimpangilio. Mtu atakapokujibu swali la kwanza vizuri, swali la 3 na 4 yanamezwa.

Lakini pia inashangaza ktk kiwango chako cha "ku-define" usomi/msomi umeshindwa kuona waliyofanya. Basi, nakupa ushauri wa bure kuwa tangu sasa elewa kuwa, toka Tanganyika ilipopata uhuru hadi leo nchi hii ktk sekta zote imeendelezwa na mazuzu. Hata aliyekufundisha kusoma + kuandika + kompyuta ni zuzu.

Back
Top Bottom