Msomi ashauri kufuta cheo cha DC kuokoa gharama

FOE

Member
Sep 21, 2009
87
6
Dk. Kessy (udsm)amesema mfumo unaosababisha wingi wa vyeo katika halmashauri za wilaya, unaongeza gharama na kusababisha matatizo kati ya viongozi na watendaji.
Alitoa mfano wa nafasi hizo kuwa ni Mkuu wa wilaya (DC) na Mwenyekiti wa halmashauri, na kwamba utekelezaji wa majukumu yao ungeweza kufanywa na kiongozi mmoja. Dk. Kessy alisema mfumo usiofuata wingi wa viongozi katika serikali za mitaa, hususani ngazi za wilaya, unatumika kwa nchi kama Uganda na kuleta mafanikio ya kidemokrasi na maendeleo. Source: Ippmedia.
 
Mkuu FOE heshima mbele.

Hoja ya Dr Kessy wa UDSM imeshawahi kujadiliwa hapa jamvini kwa kirefu sana.Mfumo wetu ni mbovu sana kwanza hausaidii wananchi na taifa kwaujumla wake.Gharama za kuwa na ofisi ya DC ni kubwa na ni mzigo usiokuwa na sababu ya lazima kuwepo.Mshahara wa DC pekee yake ni tsh 1,921,000/= kwa mwezi,hii ni mbali na marupurupu mengine kibao.Kuna gharama nyingine kama uendeshaji wa ofisi ya mkuu wa wilaya,magari[shangingi], nyumba na watumishi kibao.

Fedha za kuendesha ofisi ya mkuu wa wilaya zingepelekwa kwenye sekta ya elimu au kilimo kwa hakika zingesaidia kuondoa umasikini au ujinga unaolisumbua taifa letu.
 
Dk. Kessy (udsm)amesema mfumo unaosababisha wingi wa vyeo katika halmashauri za wilaya, unaongeza gharama na kusababisha matatizo kati ya viongozi na watendaji.
Alitoa mfano wa nafasi hizo kuwa ni Mkuu wa wilaya (DC) na Mwenyekiti wa halmashauri, na kwamba utekelezaji wa majukumu yao ungeweza kufanywa na kiongozi mmoja. Dk. Kessy alisema mfumo usiofuata wingi wa viongozi katika serikali za mitaa, hususani ngazi za wilaya, unatumika kwa nchi kama Uganda na kuleta mafanikio ya kidemokrasi na maendeleo. Source: Ippmedia.
Sijaona tofauti ya DC wat Tz na RDC wa Uganda, in Uganda they called Resident District commissional na anateuliwa na Rais na juzi juzi tu wabunge wa uganda walikua wanapinga kuongezewa kwa marupurupu hao jamaa kwani wanaona hakuna faida yake!
 
Kila sehemu kuanzia wilayani mpaka taifa kuna viongozi wengi ambao hawatakiwi kuwepo. Ni kuongeza ulaji tu huku utendaji ni mbovu mbovu.

Wilayani kwa mfano kuna DED, DAS, mwenyekiti wa halmashauri, DC, mbunge, wote hawa wanafanya kazi gani? Bado hakuna kinachoendelea, wilaya zinazidi kuwa mbovu, vijana wanazidi kukosa kazi, usimamizi wa miradi unazidi kutokuwepo.

Utitiri wa hawa viongozi unaongeza umalaya tu huku vijijini maana hawana cha kufanya na hivyo kujikita kwenye ngono.
 
Umenena!!!!. Lakini wengi wa hawa viongozi kwa sasa wapewa nafasi hizo kama fadhila tu na si kwamba wafanye kazi za maendeleo kwa wananchi, bali waakikishe CCM inaendelea kuepo madarakani na kuwanyonya wanachi hao.
 
yote haya ni kulipa fadhila japo kwa kuongeza mzigo kwa walipa kodi
 
Kazi kubwa ya DC (ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama (w) na mjumbe wa Kamati ya siasa ya CCM) ni kuhakikisha chama chake na maslahi ya chama yanalindwa hata kwa kutumia nguvu za dola.
Mengine ni blabla tuu.
 
This can only be reviewed if there will be a full revamp on the system and it is only system if we will have revolutionary ideas leading the country.
 
Let's face it DC ni cheo political, intended to do CCM's bidding and police the opposition.
 
Back
Top Bottom