Msomi akosoa hoja za Baraza la Vijana wa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msomi akosoa hoja za Baraza la Vijana wa CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kweleakwelea, Mar 23, 2011.

 1. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 436
  Trophy Points: 180
  Na Jacqueline Massano
  23rd March 2011

  Msomi mmoja amekosoa hoja za Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) na kudai kuwa hoja walizozitoa kwenye kikao chao mwishoni mwa wiki zina lengo la kuvuruga amani nchini.

  Baraza Kuu la UVCCM lilikutana hapa mwishoni mwa wiki na kujadili mambo mbalimbali yaliyomo ndani ya CCM.

  Mhadhiri wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini, Dk. Mark Msaki, alisema hoja zilizotolewa na vijana hao zina makusudi mabaya na zina lengo la kuwaziba midomo watu ambao wanapigania haki.

  Alisema kauli ya UVCCM kutangaza kuwashughulikia baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa ni dalili ambazo zinaonyesha wazi bado hawajapata mlezi wa kuwafunda na kuwaonyesha misingi sahihi ya kuwatumikia wananchi.

  Mhadhiri huyo alisema jukumu la UVCCM kwa sasa ni kutatua matatizo ya kiuchumi na kijamii kuliko kutangaza sera za kuleta chuki na kutaka kuwafunga midomo wananchi wenye uchungu na maendeleo.

  “Ningewaona wa maana iwapo wangepambana na watu wachache ambao wanajilimbikizia fedha, kuliko kutangaza vitisho na ubabe kwa baadhi ya viongozi wapenda maendeleo,” alisema.

  Alisema iwapo wangetoa msimamo wao juu ya kupambana na mafisadi, wangeonekana wapo katika maslahi ya taifa badala ya kuonyesha nia kubwa ya kupambana na watu ambao ni wapigania haki za wanyonge.
  MY TAKE: ITAPENDEZA ZAIDI KAMA WASOMI WAKIJITOKEZA BILA WOGA KUSAIDIA KUONYESHA DIRA YA NCHI NA KUWAKOSOA WANASIASA WANAOMISBEHAVE KWA MASLAHI YA TAIFA. BIG UP DR MSAKI
   
 2. Z

  Zero One Two JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2011
  Joined: Sep 16, 2007
  Messages: 9,390
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Hawa vijana walikutana kujadili watu badala ya kujadili issues. Hii ndio hasara ya kukaririshwa mambo. Hawana analytical skills, kwa hiyo wakikutana ni kujadili watu kama waswahili wafanyavyo tu. Kwao kuanguka kwa CCM ni ksababu kubwa ni viongozi wao kusema wanayodhani yatakisaidia Chama.
   
 3. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Hawa pimbi hamna hata haja ya kuwajadili maana wote ni vibaraka, na wasomi uchwara
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  hivi UVCCM ni kina nani? wanafanya nini? kwa maslahi ya nani? kivipi? wana akili? ni wapuuzi?

  tupo tayari kushughulikiwa. wajitokeze, wasiongelee kwenye magazeti.

  tuko kinyume na chama chao cha wahujumu uchumi. muhimu wafahamu hilo.

  we are not after T-shirts, we are not after caps, we are after FREEDOM of our country.
   
 5. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,158
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Huu ni "UMOJA WA VISHAMBENGA WA CCM".ingekuwa ni vijana wangekuwa walau na chembe ya heshima kwa wakubwa zao.Badala ya kusema hayo waliyoyaita tamko.
  Ndugu sitta,sumaye,warioba,butiku,na wengineo.wametoa maoni yao kama watanzania na ni makada wa muda mrefu ndani ya ccm.wanakielewa chama kuliko hawa makamanda wa chama wanaokibomoa chama kwa sasa.(waliowatuma uvccm)
   
 6. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Msomi?

  JF imejadili hao from the Sentiments.!
   
Loading...