Msome Yahya Msangi

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
3,767
8,684
NINI ASILI YA NDOA aka marriage?

Tafsiri nyepesi ni: muungano wa binadamu wawili kwa minajili ya kuzaa.

Ndoa hazikuletwa na dini kama wengi tulivyofundishwa. Ndoa zilikuwepo kabla ya imani za kidini. Jamii ya enzi ya "wawindaji na wakusanyaji aka "hunters and gatherers " ambazo zilikuwepo kabla ya Hizi Dini zetu zilifanya ndoa. Ndoa za enzi Hizo zilikuwa za vikundi vya hadi watu 30. Madume kama 5 na majike 25. Midume 5 inakuwa na haki ya kuzaa na mijike 25. Mgoni anakuwa mwanaume asiye katika wale 5 kujirusha na mmoja kati ya wale majike 25. Ukidakwa, adhabu ni moja tu! kifo! Ila kama wenzako kwenye kundi lako wanaamua kukutetea basi kunazuka vita. Wanaoishindwa wanaporwa majike yao. Wanajipanga upya.

Ndoa hizi zikifungishwa na wazee maalum. Anaweza kuanza dume na jike na wengine wanajiunga baadae. Ikitimia idadi wanatangaza kuwa "ndoa imekamilika". Akifa mmoja wao anatafutwa wa kuziba pengo.

Enzi hizo kubaki mke na mume peke yenu ilikuwa ni hatari. Mtavamiwa kirahisi. Kwa hiyo kuwa wengi kwenye ndoa ilikuwa mbinu ya ulinzi wa ndoa.

Mwanamke mgumba alifukuzwa fastaa kwenye kundi. Alihesabiwa ni hasara kwenye ndoa.

Baada ya jamii ya wawindaji na wakusanyaji binadamu akaanza shughuli za Kilimo na ufugaji (Agrarians and normadics). Nao waliendeleza utaratibu wa ndoa walioukuta kwa muda. Lakini shibe na utajiri humtia mtu jeuri. Wanaume wakaanza kujihoji! Nina uwezo wa kumlisha mke na Watoto, Nina silaha (mashoka, majembe, Mundu) kwa Nini nichangie mke? Kwa Nini nisiwe na uhakika kuwa hutu Mtoto ni Wangu?

Tartiibu wanaume wakaanza "kumiliki" wamama! Huyu wangu! Lakini kutokana na uhaba wa midume, uwepo wingi wa chakula na mifugo, mahitaji ya nguvu kazi (watoto) ndoa za wake wengi zikaongezeka. Na kwa kuwa sifa kuu ya mwanamke ilikuwa idadi ya watoto anaototoa wamama wakaanza mashindano ya kuzaa. Mimi nimezaliwa family ya watoto 12 ! Baba na mama mmoja (Allah awafanyie wepesi inshaallah).

Hali hiii ikaendelea kwa karne kadhaa hadi zilipoibuka dini. Na bado zinaibuka mpyaaa zenye miungu wanaokula chips!

Baadhi ya Hizi dini zikaweka taratibu zake.

Mifano: kuweka sharti la mwanamke ndiye atoe mahari.Unaweza kudhani wamekosea kutokanaa na imani yako lakini walikuwa na mantiki. Kumlinda mwanamke! Kama hakutaki hakutolei mahari! Unaondoka!

Wengine wakaweka sharti aolewe mmoja tu MPAKA kifo. Lakini nyumba ndogo wapo

Wako walioweka shurti waolewe wanne tu. Lakini mechi za nje wamo! 4 haiwatoshi.

Zipo imani haswa US zinakataza ndoa. Zinaamini ndoa ni dhuluma dhidi ya wanawake. Unaweza usikubaliane nao lakini ndicho wanachoamini kama ambayo wéwé ulivyoamini utaratibu wako ambao nao una mawenge!

Zipo jamii ulaya wanaishi vijiji wanaviita "No marriage villages"! Yaani vijiji ambavyo sifa ya kuishi ni kutokuwa n'a ndoa". Wanaamini ni "safe heaven" kwa wamama na wababa wasiotaka ndoa. Ukilazimishwa watakutetea! Ni Sawa tu na "eco villages" aka vijiji rafiki wa mazingira. Hawatumii hydropower au umeme utakanao n'a mafuta. Hakuna kukata mti au kuchafua mazingira. Ni uamini wao usiwalazimishie unachoamini wéwé!

Ndoa kama unavozifahamu wéwé zilianza Karne ya 8! Karne nyingine Ndiyo za kina hunters & gatherers, Agrarians & Nomadic people.

Nikuache na hii: kabla ya Karne ya 8 wagiriki walikuwa wanataka hivi Siku Binti Yao anaolewa: "I pledge my daughter for the purpose of producing legitimate offspring." Yaani "nakukabidhi Binti yangu kwa minajili ya kuzaa watoto wasio haramu"! Yaani anamuonya kijana asimpeleke binti yake kwenye ndoa ya vikundi.

Kwa asili hiii ukweli ni kwamba watu hawaoani kwa kuwa juna mapenzi Love) kati yao. Watu wanaoana ili wazae watoto wasio haramu!

Nikipata nafuu na wasaa nitaeleza ni Nani na Nini kilileta hii dhana feki ya mapenzi (love) katika ndoa?! Utashangaa kwa kuwa ilitokana na matendo ambayo mungu ameyakataza na kutuonya tusiyatende!

Asalaam!
 
Jamii inahitaji mawazo huru kama haya kwaajili ya kupiga hatua zakimaendeleo
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom