Mskilizeni Salva Rweyemamu kuhusu tuhuma za ufisadi wa BOT etc! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mskilizeni Salva Rweyemamu kuhusu tuhuma za ufisadi wa BOT etc!

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Mkira, Oct 9, 2007.

 1. M

  Mkira JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2007
  Joined: May 10, 2006
  Messages: 425
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ndugu zangu fungueni BBC swahili ya leo asubuhi msike mahojiano ya Salva Rweyemamu mimi nimeskikia leo asubuhi!

  Kwa kweli kwa majibu yake juu ya nini serilaki ifanye kuhusu tuhuma yamenisikitisha sana! Kwanza sijui yeye ameongea kama Rais au la!

  Maana ANASEMA SERKALI HAINA MUUDA WA KIJIBU TUHUMA ZA KIPUUZI ZISIZO NA UKWELI NA KWAMBA ZILISHAJIBIWA BUNGENI ETC!!

  Watu kama hawa ambao wameweka maslahi yao binafsi mbele ni hatari sana wao kuwa washauri wa rais, wanaweza kulifikisha taifa hili pabaya kama ya huko Rwanda etc!

  Mtaalamu anaweza kuifungua huku BBC leo kabla haijatolewa ili aiweke hapa mumsikie ndugu yetu!.

  Mimi sisemi ni za kweli au uongo lakini yeye anasema ni za kipuuzi Je ameisha fanya utafiti?

  JK watu kama akina Rweyemamu ni wa kuwa nao makini sana! japo ni rafiki yako.
   
 2. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2007
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 3,998
  Likes Received: 1,036
  Trophy Points: 280
  sijaisikiliza ila nafuatilia nisikie, wanacheza, wataacha kucheza siku wananchi watakapoingia ikulu kwa miguu. hivi wanashindwa kuchunga kauli zao. Zama hizi sio za kuropoka ovyo.
   
 3. Shemzigwa

  Shemzigwa JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2007
  Joined: Jan 8, 2007
  Messages: 337
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  http://streaming-ws.bbc.co.uk.edgesuite.net/asx.esi?swahili/tx/nb/swa0300.wma
   
 4. K

  Kalimanzira Senior Member

  #4
  Oct 9, 2007
  Joined: Aug 15, 2007
  Messages: 100
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi mlitegemea atasemaje, wakati ndio kwanza ameanza kuonjeshwa utamu wa asali. Lakini Ulimwengu alimwambia Kikwete katika ile barua ndefu kwa rais. Alimwambia katika utawala wake ajihadhari na wapambe amabao kazi yao itakuwa ni kumpamba na kumficha ukweli na hasira ya wananchi pale serikali itakaposhindwa kuwatimizia matakwa yao. Sasa ukimsiliza Salva, utagundua kuwa ndio wapambe wenyewe amabo hata pale mgomo utakaposambaa nchi nzima watamwambia 'mzee usiwe na wasiwasi, wananchi wnakupenda sana na ndio maana walikuchagua kwa asilimia 80"! .....Mtu anayefikiria tumbo lake tu, hakika katika dunia hii ni mtu mbaya sana, maana usimtegemee kwa chochote.
   
 5. Icadon

  Icadon JF-Expert Member

  #5
  Oct 9, 2007
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 3,589
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
 6. Shemzigwa

  Shemzigwa JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2007
  Joined: Jan 8, 2007
  Messages: 337
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
 7. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #7
  Oct 9, 2007
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,068
  Likes Received: 20,132
  Trophy Points: 280
  Mwenzenu yuko katika usingizi mzito kama aliyekula nyama ya Fungo.Mapochopocho ya Ikulu yamempofusha hata hajui kitu gani kinaendelea.Hii ni hatari kuwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu ya nchi mwenye uono finyu kama huyu ambaye kauli zake hazina tofauti na watu kama Makamba,Tambwe na wengine wa daraja hilo.
   
 8. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #8
  Oct 9, 2007
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 369
  Trophy Points: 180
  Lord have mercy.
  Salva must go. wadau anzipetition tuipigie kura
   
 9. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #9
  Oct 9, 2007
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 145
  Uzushi gani?

  Nauliza tena: Uzushi gani?

  Binafsi ninamfahamu Salva kwa kuwa nilifanya naye kazi, kitaaluma.

  Kinachonishangaza ni kwamba, baada ya Mkataba wa Buzwagi (angekuwepo Mwalimu angeuita Mkataba wa Kihuni) kusambazwa kama pipi hadharani, ukweli wa tuhuma zilizotolewa na kambi ya upinzani umeonekana.

  Salva ameingia kwenye ile kambi ya Wapambe wa Mfalme, ambao kila uchao hawaishi kumsifia Mfalme, hata kama anakosea, kwamba anapendeza. Wanasema: Leo Mfalme umependeza kweli! Wakati huo huo, wananchi wanamwona Mfalme akiwa uchi, hajavaa nguo. Wapambe wanampamba Mfalme, kumbe anaumbuka kwa wananchi wake.

  Iko siku upambe huu utakwisha, na Mfalme atangundua kwamba hajavaa nguo yoyote, na hapo ndipo atakapoweka mambo yake sawa. Namtakia kila la kheri Mfalme... afanikiwe katika hilo, lakini kamwe sitajiunga na kambi ya wapambe...

  Sasa, je, tujiulize, Mfalme alikosea kumtea Salva? Au hakujua kwamba anaongeza idadi ya wapambe?
   
 10. C

  Chief JF-Expert Member

  #10
  Oct 9, 2007
  Joined: Jun 5, 2006
  Messages: 1,470
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Unanikumbusha yule msemaji wa Saddam wakati wa vita vya Iraq. Alikuwa nani vile?
   
 11. M

  Mwakilishi JF-Expert Member

  #11
  Oct 9, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 484
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Yep mpambe anatetea tumbo lake...Yule msemaji wa Saddam ni "Comical" Ali kama sikosei, anasema "there are no American soldiers in Baghdad wakati wamesimama nyuma yake" si utani!!
   
 12. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #12
  Oct 9, 2007
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Unategemea nini kutoka kwa mtu mwenye guts za kuanzisha Media PR fim ya kutetea mafisadi kama Manji?

  Kama huna habari basi ni kuwa mara baada ya uchaguzi 2005 Slava na kuwadi mwenzie Dr Shoo walianzisha firm ya PR ambayo moja ya kazi iliyowapa pesa nyingi ni ile ya kumsaidia Manji kupambana na kashfa ya mabilioni ya NSSF kwa kutumia vyomb vya habari. Wao ndio waliokuwa wakianda Press Statements na hata media coverage kuhusiana na suala hilo. Waliandika makala nyingi tu za ajabu ajabu kumfitinisha Mengi na vyombo vyake ya habari.

  Mwenzie Dr Shoo kwa kushirikiana na Muhingo Rweyemamu ndio wamekuwa washauri wa karibu wa Karamagi hata kuandaa ile statement yake na za wengine.

  Inasikitisha sana jinsi wenzetu hawa wanavyotumia vipaji walivypewa na mungu na uwezo wao kisomi walioupata kutokana na kodi za walala hoi na walalahai wa Tanzania...

  Tanzanianjema
   
 13. K

  Koba JF-Expert Member

  #13
  Oct 9, 2007
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,149
  Likes Received: 486
  Trophy Points: 180
  lakini jamani ni kweli tunajua wanachoongea ni propaganda tuu na nia ni kumtetea muungwana ni kazi yao..kwani mlitegemea atasema nini? dawa ni kuendelea kurusha marockets tuu mpaka watasalimu amri
   
 14. Gembe

  Gembe JF-Expert Member

  #14
  Oct 9, 2007
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 2,506
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  inasikikitisha kwa mtu huyu ambaye si raia analisemea taifa la watu makini na msikini,
  hawa ndio watu wanaoshiriki katika kuhujumu khali ya Uchumi wa nchi yetu..
   
 15. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #15
  Oct 9, 2007
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 9,883
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Mr Chief,
  yule waziri wa Saddam (RIP) wa habari na utangazaji alifahamika kama Mohamed Saeed al-Sahaf. Hii ndio kazi anayoifanya Salva leo akiwa Ikulu, yaani yeye ni kufagilia utawala tu bila kuoanisha na mantiki ya hali halisi.
  Wasifu zaidi wa waziri wa Iraq unapatikana katika kiungo hiki,
  www.welovetheiraqiinformationminister.com
   
 16. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #16
  Oct 10, 2007
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Muhammad Al Sahaf. Nasikia Marekani wanataka kumpa kazi ya kufundisha kwenye kitengo chao kimojawapo cha propaganda. Miye nilikuwa JKT wakati wa ile Gulf War ya kwanza (1990), na namkumbuka C.O wetu mmoja aliwahi kumsifia Saddam kwenye mkutano na askari (sisi), kwamba Saddam anaweza kuwa na ubaya wake, lakini katika tabia na sifa anazopaswa kuwa nazo askari, basi Saddam alikuwa askari kwelikweli mwili na roho, kwani licha ya nguvu za Marekani na washirika wake, hakujisalimisha wala kuomba suluhu. Na rafiki yangu mmoja anayefundisha pale Kivukoni academy aliniambia kwamba yule Al Sahaf alifuzu haswa somo la Propaganda, ndivyo inavyopaswa kufanyika hadi ndivyo iwe sivyo, chekundu kionekane cheupe kabisa, hata yule anayekiona chekundu ajihisi mwenyewe ana ugonjwa wa akili!
   
 17. M

  Mtu JF-Expert Member

  #17
  Oct 10, 2007
  Joined: Feb 10, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
 18. Shemzigwa

  Shemzigwa JF-Expert Member

  #18
  Oct 10, 2007
  Joined: Jan 8, 2007
  Messages: 337
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  siku zote wee mtu Unalala ama kweli wewe mtu kiatu
   
 19. F

  FDR Jr JF-Expert Member

  #19
  Oct 10, 2007
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 249
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kumfananisha Salva na Alsahaaf is too much wana JF;Hahaaaaaaaaaaaaa,ninyi viumbe mbona mnatisha namna hii;Aah walau leo nimecheka sana,si kwa hoja ila hilo jina Alsaaf;Mungu amjalie muungwana yule popote mafichoni alipo,ktk muongo huu wa Joji Woka Bushi ni mwana PR bora kabisa aliyeweza kuwakonga nyoyo walimwengu,Salva kaka yetu ujumbe huo ukufikie,Amina
   
 20. m

  mzee wa london Member

  #20
  Oct 10, 2007
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Salva hawezi kuwa kama Al sahaf,salva ni opportunist,Al sahaf alikuwa mtu wa Saddam,Salva ni mnafiki mtu wa maslahi.Kabla hajapata post tulikuwa tunaponda sote serikali,leo ana office IKULU!!!!!!
   
Loading...