Msiwe wabishi, Polycarp Cardinal Pengo alishajiuzulu na hayumo tena madarakani

Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
2,933
2,000
Anaamua papa kulingana na shughuli zake haingiliwi,mfano tanzania ina cardinal mmoja na marekani watano
Marekani kuna logic, wakatoliki kule wanaweza kua wengi kuliko huku Tanzania, misri ina wakatoliki chini ya laki 2 ila makadinari 3. Nini special kwa misri?
 

The only

JF-Expert Member
May 19, 2011
5,994
2,000
Marekani kuna logic, wakatoliki kule wanaweza kua wengi kuliko huku Tanzania, misri ina wakatoliki chini ya laki 2 ila makadinari 3. Nini special kwa misri?
mkuu na mm nimetafakuri sana ,nimebaki kujua hawa sio wahudumu wa kiroho tu bali kuna mambo mengine mengi,ili nikuchanganye vizuri poland in makardinal 7 na idadi ya watu 38 mil ,Tanzania ina mil 50 ila inaye mmoja tu,na je unajua ili uwe papa si lazima uwe cardinal wala padre ,unatakiwa uwe mwanaume ,umebatizwa ,mkatoriki safi na unaushawishi kwa baraza la makardinal
 

Aikambee

JF-Expert Member
Sep 27, 2017
4,039
2,000
Nijuavyo mimi Kardinali wa Tanzania ni P. Pengo, na huyu ndiye atashiriki kwenye kupiga kura ya Papa mpya huko Roma kama ikihitajika kufanya hivyo.

Labda unachanganya kati ya Askofu Mkuu wa Jimbo la Dar na Kardinali!

Kwani Askofu mstaafu hawezi kuwa kadinali?
 

Manjagata

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
8,185
2,000
arch bishop ni anaesimamia diocese nyingi zilizochini ya ma bishop ,arch bishop wa kila nchi wa kila wa jimbo kuu huwa lazima awe mmoja ,ila macardinal sio mabosi wake ni wawakilishi wa papa kuna nchi wako zaidi ya mmoja mfano misri ni watatu,nimependa upenzi wako wa kuhoji we wafaa kuwa rafiki yangu
Teh teh teh tehe teheeeee!
 

fogoh2

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
3,720
2,000
Kwanza hakuna cheo cha kardinali wa tz. Kardinali ni mfanyakazi wa papa anaweza kuwa yeyote kati ya Padri, Shemasi, au Askofu na siyo kwamba kila nchi lazima kuwe na kardinali. Kazi ya ukardinali inaishia tu Vatican kumsaidia papa katika majukumu yake pale vatikan, na ndo mana kila kardinali amepangiwa kazi yake pale Roma. Mkuu wa kanisa katoliki katika nchi yoyote ni Askofu mkuu katika jimbo lake na hakuna Askofu mkuu zaidi ya wenzake na siyo kardinali ni kwa vile tuu pengo alipewa ukardinali na akawa askofu mkuu wa jimbo kuu haimaanishi kwamba kardinali ndo mkuu wa kanisa. Kardinali anaweza kuteuliwa hata shemasi au padre na cheo chao kinaishia Vatican.
Nimejifunza Jambo
 

fogoh2

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
3,720
2,000
Ni wapi nimesema Kardinali ni Mkuu wa Kanisa?
Mkuu wa Kanisa Katoliki ni Papa anaishi Roma. Nilichosema ni kwamba Kardinali P.Pengo ndiyo pekee anayeweza kipiga kura kuchagua Papa kwa upande wa TZ kama ikihitajika.
Kama haikuhitajika kazi nyingine Ni Nini hapa tanzania? Na mkuu wa kanisa katoliki hapa Tanzania Ni nani?
 

kabila01

JF-Expert Member
Apr 21, 2009
4,041
2,000
Taratibu kijanaa unajua papa ukiulizwa ni nani,huwa ni askofu wa rome (ndo dar yenyewe hiyo)
Tafuta katekism ya kanisa katoliki ile kubwa kuliko biblia utapata maarifa mengi kuhusiana na kanisa katoliki. Kadinali sio lazima awe askofu wa Dar. kuna aina tatu za makadinali. kuna watu walikua makadinali huku wakiwa mashemasi mfano ni St. Laurent from Rome Italy. Kila askofu ni mkuu ktk jimbo lake na anawajibika moja kwa moja kwa aliyemteua ambaye ni Papa. askofu hawezi kwenda kuendesha ibada katika jimbo la askofu mwingine bila kupewa ruhusa na askofu wa jimbo husika. Hata pengo hawezi kwenda kuendesha ibada sumbawanga kwao bila kupewa kibali/ruhusa na askofu wa sumbawanga
 

ipogolo

JF-Expert Member
Aug 15, 2011
6,156
2,000
Kuna watu bado hawaamini kwamba Polycarp Cardinal Pengo hayumo tena madarakani na lakini bado wanaendelea kumtukuza huenda asisahaulike.

Ukitembelea baadhi ya Parokia na nyumba za kanisa bado picha ya Polycarp Pengo inaonekana kana kwamba yeye ndiye askofu wa D'Salaam.

Halafu jimbo la D'Salaam limeanzisha mtindo ambao haupo kabisa. Misa inapofika ile sehemu ya kumtaja askofu huwa tunasema "Yaani mtumishi wako Baba Mtakatifu Francis na askofu wetu Jude Thadaues na askofu msaidizi Eusebius".

Sasa siku hizi baadhi ya parokia za D'Salaam zimebuni zikisema "na askofu wetu mstaafu Polycarp Cardinal Pengo".

Sijui hii wamefundishwa na nani tena nimeisikia ikitamkwa palepale St. Joseph ambako ni makao makuu ya kanisa.

Nasema hivi kwamba hii haitakiwi. Maadam Pengo ameshajiulu hatakiwi kabisa kufanyiwa hayo na hastahili.

Tukianza na picha, picha iliyopo ni picha ya Papa Francis wala hakuna picha ya Papa Benedict XVI aliyejiuzulu. Hata ile sala hatusemi "na Papa Mstaafu Benedict XVI" tunaishia kumsema Francis tu.

Hivyo, tukumbushane ukweli. Picha ya Polycarp Pengo iondolewe kwenye ofisi zote za jimbo la D'Salaam kama ilivyoondolewa ya Lebulu (Arusha), Mtega (Songea), Msarikie (Moshi), Butibubage (Mwanza), Papa Benedict XVI (Roma).

Na ile sala Pengo asitamkwe kwani hastahili kama ambavyo hatumtamki Papa Benedict XVI.

Kukumbishana ni vizuri. Jadili kwa hoja.
Cardinal Pengo Polycarp hajajiuzulu Wala hatajiuzulu. Pengo amestaafu.
Jumapili ijayo wakatoliki watakuwa na miss maalum ya kumwaga itakayoadhimishwa Kanisa la Kristu Mfalme- Segerea.
Wakatoliki wa Tanzania wanamheshimu Sana Muhashamu Pengo.
Waache wakristo katoliku waendeshe Mambo yao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom