Msiwatumikie mabwana wawili, chagueni siasa au utumishi wa umma

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,682
1,110
Hili la wakurugenzi limekaa sawa,je hawa watendaji wa Kata wanao tangaza na kusimamia uchaguzi wa madiwani na viongozi wa mitaa ilihali ni makada wa CCM kama mtendaji wa Kata ya Kihesa ndugu Davis Swebe,sheria inazungumzia nini!!!

Nachelea kusema hivi kutokana na mtendaji huyu kuwa wazi na wakati mwingine kufanya kampeni za chama na kuwa msemaji ilihali ni mtendaji wa serikali asiyetokana na mwamvuli wa siasa(political virtual umbrella )

Point yangu inasimamia wapi!!
Hatuwezi kuwa na muamuzi mzuri anayeweza kusimamia haki ilihali yeye mwenyewe ni mchezaji katika timu ambayo inapambana na timu pinzani, haki akatoa haki sawa, kwa kuwa mtendaji huyu jukwaa la siasa analipenda kuliko kazi ya utendaji, ni heri achie Ngazi abaki na uccm wake.

Ni wakati sasa wa kutenganisha majukumu ya kiutendaji Kati ya mtumishi wa umma na wanasiasa. Tukiachia utamaduni huu unao pandikizwa ili uzoee mazingira ya siasa ilihali ni watumishi wa umma, tunaweza kulitumbukiza taifa kwenye mgogoro usio na tija kitaifa, utakaoleta athari kubwa na mgongano mkubwa katika kusimamia haki.

Huenda ni makengeza ya akili ya makusudi yanafanywa kwa minajili ya kukengeuka maadili ya utumishi wa umma, katika kufanikisha lengo fulani lakini ni muhimu kudhibiti sintofahamu hii yenye lengo ovu dhidi ya Watanzania.

Niwaombe wanazuoni wenye taaluma ya sheria kulimulika hili jambo kwa umakini katika mapambano ya haki dhidi ya batili, ili kuondoa makando kando ya makusudi yenye nia ovu kwa mustakabali wa siasa za nchi yetu, TANZANIA kwanza mengine yatafuata.
 
Back
Top Bottom