Msiwasafirishe walimu kwa malori-CWT

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
AJIRA YA UALIMU SIJUI INA MKOSI GANI YAANI UKIPATA KAZI YA UALIMU UNAKUA MTU WA KUNYANYASIKA TU
ETI KARNE HII WAALIMU WANASAFIRISHWA KAMA MIZIGO NDANI YA MALOLI KWENDA KUSIMAMIA MITIHANI

CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT) wilayani Chamwino kimeitaka Idara ya Elimu katika
halmashauri hiyo isitumie malori kuwasafirisha walimu wakati wakiwapeleka kwenye vituo vya kusimamia mtihani wa darasa la saba unaoanza leo.

Mwenyekiti wa CWT wilayani humo, Amani Msanga alitaka yatumike mabasi au magari
madogo kufanikisha hilo.

Aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matayarisho ya mitihani hiyo katika wilaya yake.

Msanga alisema kuwa hali ya maandalizi ya mtihani huo wilayani humo, kwa kiasi kikubwa,
yamekamilika na kwamba kinachosubiriwa ni kuwasambaza wasimamizi hao katika vituo
walivyopangiwa.

Alisema asingependa kuona walimu hao wakibebwa kwenye malori badala yake, yatumike
mabasi au magari madogo.

Alisema kuwa kila mwaka wasimamizi wa mtihani wamekuwa wakibebwa katika malori kupelekwa kwenye vituo vyao vya kusimamia bila kujali usalama wa maisha yao.

"Kama wahusika wa maandalizi ya mtihani huu wameshatoa pesa kwa ajili ya kukodi malori,
tafadhali warudishieni pesa zao kwa kuwa walimu hawatapanda hayo malori," aliagiza
Msanga.

Msanga alisema kuwa malori ni kwa ajili ya kubeba mizigo na si kusafirishia watu kwani kwa
kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na kanuni za usalama barabarani.

"Kama walimu watalazimishwa kutumia malori hayo, wachukue namba za magari hayo na kupiga simu Polisi na naomba ushirikiano kutoka kwa Jeshi letu la Polisi," alisema.

Aidha Mwenyekiti huyo aliwataka watahiniwa kuwa makini katika kujibu mtihani wao ili
waweze kufaulu na kujiunga na kidato cha kwanza mwakani.
 
Yaani hii kada inadharaulika sana.
Dah,sijui kwa nini mkuu.Mishahara wanawalipa midogo na incentives hakuna.Yaani karne hii civil sevant asafirishwa kwa lori?Au nao ni waoga sana kudai haki kwa sababu ya kuogopa kufa njaa?Pathetic
 
Back
Top Bottom