Msitu wa Udzungwa hatarini kutoweka

Lutala

JF-Expert Member
Jun 17, 2010
848
103
Boniface Meena, Mwananchi Jumapili

UTAFITI uliofanywa katika hifadhi ya msitu wa Udzungwa, umeonyesha kuwa msitu huo, unapaswa kuokolewa kwa kuwa uko hatarini kutoweka kama hatua za haraka, hazitachukuliwa.

Ripoti ya utafiti huo, iliyozinduliwa jana jijini Dar es Salaam, imeeleza kuwa baadhi ya viumbe hai wako mbioni kupotea kama mbega mwekundu anayepatikana katika hifadhi hiyo, pekee duniani.

Ripoti hiyo, imeonyesha kuwa umakini mkubwa unahitajika kukabiliana na athari za uwindaji wanyamapori katika misitu ya hifadhi nchini, hasa Udzungwa mkoani Morogoro kwa kuwa ni muhimu kwa maisha ya maelfu ya watu.

Kiongozi wa maandalizi ya ripoti ya utafiti huo, Francesco Rovero kutoka makumbusho ya Trento ya Sayansi asilia nchini Italia, alisema mwelekeo wa kupungua kwa bioanwai ni mkubwa.

“Mwelekeo wa kufanana wa kupungua kwa bioanwai pia ulibainika kwa swala wadogo wa porini kama funo na idadi ya wanyamapori imekuwa ni ndogo ukilinganisha na idadi ya wanyama katika misitu, iliyohifadhiwa vizuri,”alisema

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA), Amani Kitegile ambaye alikuwa mmoja wa waandaaji wa ripoti hiyo, alisema uwindaji wa nyama pori na uharibifu wa misitu ni tatizo kubwa. “Haya ni baadhi ya mambo yanayosababisha kupungua kwa bioanwai,”alisema.

Alisema msitu huo, ambao unatoa huduma ya maji kwa wakulima wanaoishi bonde la Kilombero na mabwawa ya Kihansi na Kidatu, una umuhimu wa kipekee kwa kuwa una hifadhi zaidi ya jamii 84 ya mimea na wanyama ambao hawapatikani sehemu yoyote duniani kama Ngolaga na Sanje.

“Hatua zinapaswa kuchukuliwa sasa, kama tunataka kubadilisha mwelekeo wa kutoweka kwa bionwai zetu na upotevu wa misitu, kabla hatujachelewa,”alisema.

Mkuu wa Kilombero, Evarist Kilo alisema Udzungwa iko katika hali mbaya na inahitaji msaada mkubwa wa haraka ili kuiokoa.

Alisema uharibifu wa mazingira, uwindaji na ukataji miti kwaajili ya mbao umefanya hifadhi hiyo, iendelee kupotea taratibu.


Alisema tangu mwaka 2007, hakuna ulinzi bora katika hifadhi hiyo na alisema ana wasiwasi kama wasimamizi wa halmashauri na wizara, wanafuatilia suala hilo, kwa karibu.

Mhifadhi wa hifadhi ya Udzungwa, Dk Fortunata Msoffe alisema msaada mkubwa unahitajika kiokoa msitu huo, kwa sasa.

HOJA YANGU UTAFITI PIA UFANYIKE KUHUSU SHIDA WANANCHI WA VUJIJI VINAVYPOKANA NA HIFADHI
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom