Msitu wa Shengena unamiti 17 inayotibu saratani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msitu wa Shengena unamiti 17 inayotibu saratani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MIUNDOMBINU, Apr 18, 2010.

 1. MIUNDOMBINU

  MIUNDOMBINU JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2010
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Na
  Daniel Mjema,Same

  HIFADHI ya mazingira asilia ya Chome ambayo inafahamika zaidi kama msitu wa Shengena uliopo Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, ina aina 17 ya miti ambayo kama itatunzwa vizuri ina uwezo wa kutibu ugonjwa wa Saratani.

  Mtaalamu bingwa wa tiba mbadala anayechukua shahada ya udaktari wa falsafa(PhD) nchini Philippines , Dk Rashid Dachi alisema pamoja na kuwepo kwa miti hiyo,wilaya hiyo inaongoza kwa wagonjwa wengi wa Saratani nchini.

  Dk Dachi aliliambia Mwananchi Jumapili juzi katika washa ya elimu ya utetezi wa mazingira iliyoandaliwa na Shirika la Better Living Advocates kuwa ili miti hiyo iweze kutibu ugonjwa huo inapaswa ivunwe kipindi cha masika tu.

  Alifafanua kuwa pamoja na Tanzania kuwa na hazina hiyo ya miti katika hifadhi hiyo, lakini miti hiyo haitunzwi na imekuwa ikikatwa na kuchomwa moto kwa wingi na iko mbioni kutoweka kama hatua za makusudi hazitachukuliwa.

  “Wilaya ya Same ina wagonjwa wengi wa kansa kuliko wilaya yoyote ya Tanzania kwa sababu mlima wetu ni savannah tree kwa hiyo maji yake yana madini magumu ambayo hayasagwi mwilini,”alisema.

  Dk Dachi alifafanua kuwa miili ya binadamu ni dhaifu kusaga madini hayo aina ya calcium, fluoride na zink na inapotokea hivyo, chembechembe za saratani zinajibadili tabia na kujenga ugumu ambao unabadilika na kuwa saratani.

  Kwa mujibu wa Dk Dachi, ziko kata katika wilaya hiyo ambazo watoto wanazaliwa wakiwa na mapungufu (abnormal) kutokana na kunywa maji yenye madini hayo na katika kipindi kifupi wamepokea wanawake na watoto 48 wenye saratani.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Shirika la Better Living Advocates, Wilberstone Tenga alisema kutokana na kasi ya uharibifu wa mazingira katika hifadhi hiyo, Jamii inapaswa kushiriki kikamilifu katika kuwafichua wahujumu.

  Tenga alionyesha wasiwasi wake kutokana na mwelekeo wa sasa wa kuendelea kukauka kwa vyanzo vya maji nchini licha ya jitihada za kuotesha miti na kusema tatizo ni uoteshaji miti ya asili ambayo si rafiki wa hifadhi ya maji.
  Source:www.mwanainchi.co.tz/news
   
 2. Mavella

  Mavella JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2015
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 326
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nasikitika kuiona shengena ulivyo kwa sasa tofauti na ilivyokuwa enzi hizo tukiwa watoto
   
Loading...