Msitu wa maajabu Njombe, una Kuku weusi wasiofugwa, wanawake hupotea wakiingia na "siku zao"

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
Nikiwa shuhuda wa safari ya kwenda katika msitu huo, nimejionea na kusikia mengi.
Ni simulizi ndefu ya kimila ambayo kwa waumini waliobobea, ni lazima wapingane nayo.

By Tumaini Msowoya, Mwananchi tmsowoya@mwananchi.co.tz

Waswahili husema “tembea uone”. Ndivyo unavyoweza kueleza simulizi ya ajabu kutoka mkoani Njombe.

Huenda ni wachache ambao wamebahatika kufika msitu wa Nyumbanitu na kupata simulizi hii.

Binafsi, nimefika ili kuwa sehemu ya historia na kama maji niliyavulia nguo, hivyo sikuwa na budi kuyaoga!

Baada ya kupata taarifa zisizo za kawaida kuhusu msitu huo, nilifanya mpango kwenda kushuhudia yale niliyokuwa nayasikia.

Nilijiandaa kimwili na kiakili na kuanza safari.

Tulipofika tulielezwa taratibu za kuingia kwenye msitu huo mdogo, ikiwa ni pamoja na kutambaa, kwenda kinyumenyume wakati wa kuingia na sehemu nyingine kusubiri maneno fulani yatamkwe ili kupata ruhusa ya kuingia.

Msitu wa Nyumbanitu umebeba jina linalomaanisha “nyumba nyeusi”. Upo katika Kijiji cha Mlevela, Kata ya Mdandu Wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe.

Huu ndiyo msitu uliobeba asili ya kabila la Wabena na ni muhimu kwa utalii kutokana na mandhari yake inayopambwa na utunzaji wa mimea na hifadhi ya mazingira.

Maajabu ya msitu huo ni kuku weusi wenye midomo myekundu ambao wahifadhi wanasema hawazeeki, hawafugwi na wala hawaliwi.

Kuku hao huonekana kwa wingi wakati wa mavuno na inapofika masika, hawaonekani tena.

Pia, inasemekana huwa kuna ng’ombe na kondoo ambao huingia kwa msimu na rangi ya wanyama wanaongia kwenye msitu huo nyeusi.

Kuna rupia ambazo huwa zinawavutia wengi na hivyo kuingia hamu ya kuziiba, lakini kimaajabu hujikuta wakishindwa kutoka ndani ya msitu hadi pale wenyeji wanapoamua kuwanusuru.

Miti na mimea mingine yote iliyoko ndani ya msitu huo imedumu karne nyingi, huku watafiti wa ndani na nje ya nchi wakihangaika kufanya tafiti mbalimbali, hasa kujifunza aina za mimea.

Kuna mapango makubwa ambayo watu zaidi ya mia wanaweza kuishi, huku simulizi zikieleza kwamba mapango hayo yalitumika wakati wa vita.

Simulizi za msitu wa Nyumbanitu ni za kutisha na ndizo zilizonisukuma kupanga safari kwa ajili ya kuutembelea.

Siku ya kujitosa kwenda kushuhudia maajabu hayo, niliondoka Njombe alfajiri na kufika Kijiji cha Mlevela saa 2.00 asubuhi na kukutana na wenyeji wangu ambao ndiyo waliopewa jukumu la kuulinda msitu huo.

Nilikaribishwa vizuri, lakini kabla sijaanza kujitambulisha, mmoja wa wenyeji hao alipigiwa simu ya kuwapo kwa kundi la watalii wa ndani, waliokuwa wamefika kijijini hapo kwa ajili ya kushuhudia maajabu ya msitu huo.

Hivyo, utambulisho ulisimama kwa muda. Tulisubiri hadi walipofika, kisha utambulisho ukaanza, huku mwishoni kila mmoja akitakiwa kueleza nia ya ujio wake kwenye kijiji hicho cha kimila.

Nilifurahi kwa kuwa sikuwa peke yangu tena. Hata hivyo, licha ya wingi wetu bado woga na hofu ndivyo vilivyokuwa vimetawala.

Kilichotutisha zaidi ni tangazo la waangalizi wa msitu huo la kuwataka wanawake walio katika siku zao, yaani kwenye hedhi, kutothubutu kuingia.

“Ni mwiko na ikiwa utajidanganya kufanya hivyo, basi miaka yako yote utabaki hivyo hivyo, hakuna dawa ya kutibu,” anaeleza mmoja wa waangalizi, huku akiwa amepaza sauti yake.

Japo haikuwa mara ya kwanza kwangu kuingia kwenye msitu huo kwa kazi zangu za habari, bado nilijibanza kwa wenyeji wangu ili ikiwa litatokea jambo lolote, nibaki salama.

Wasimamizi wa msitu huo wanasema ikiwa mtu ataingia bila kufuata masharti anaweza kuzunguka kutwa bila kutoka, licha ya kuwa ukubwa ni wa ekari mbili pekee.

Kwa sasa msitu huo unatunzwa na wanandugu , Julius na Alex Msigwa, ambao kabla ya kutembeza wageni msituni huwa lazima waulize nia ya ujio wao.

“Mmekuja wageni wengi japo kila mmoja wenu ana safari yake. Semeni nia ya kutembelea msitu huu ili tuwasaidie na kuwaeleza wazee wetu wawapokee kulingana na shida zenu,” anasema Julius.

Kwa kuwa kila mmoja wetu alifanya ziara hiyo kwa lengo la utalii, isipokuwa mimi niliyekuwa na nia ya kupata simulizi ili niweze kuiandika, nililazimika kujieleza.

“Kumbe ni kama mna nia moja. Jiandaeni punde tutaanza safari ya kuingia msituni,” anaeleza.

Safari ya msituni inaanza

Ijapokuwa kwa nje msitu wa Nyumbanitu unaonekana mdogo, ndani ni mkubwa na umesheheni miti mirefu ya asili tofauti na mwonekano wake kwa nje.

“Hodi! Hodi! Hodi Mutwa! Avagenzi ava vanuhile! Vihwandza whifunza! Hodi vamkongwa, Hodi vamwafute! Hodi Vakiswaga!....twisuka mwanuhile avagenzi ava,” anasema Julius, ambaye ni kiongozi wa msafara akimaanisha kuwa anaomba ridhaa ya kuingia msituni na wageni.

Baada ya kutamkwa maneno hayo na kusubiri kwa dakika moja, tuliambiwa tumeruhusiwa kuingia msituni.

Tuliingia kwa kupitia mlango mdogo ulio pembezoni mwa barabara ya Njombe mjini-Mdandu.

Kwa mgeni si rahisi kuugundua mlango huo mpaka uwe na wenyeji.

Tuliwasili eneo la kwanza linaloitwa Sebuleni.

Tukiwa hapo, kiongozi wa msafara alizungumza kwa sauti kubwa akitaka wale waliovaa viatu, vilemba au kofia wavue.

Pamoja na hali ya hewa kuwa ya baridi kali, hakuna aliyeacha kutii masharti hayo.

“Nyosheni mstari mmoja, hakuna mtu kupita pembeni na hamruhusiwi kuingia mkiwa mmevaa viatu, kofia wala kilemba,” anasema Alex ambaye pia ni mwongozaji.

Kila mmoja aliinama ili kuvua viatu, tayari kuendelea na safari ya kuingia msituni.

Binafsi nilivaa kilemba kwa ajili ya kujikinga na baridi kali ya mwezi Juni, nilitii sharti la kukivua na wakati huo wote, hakuna aliyekuwa akizungumza neno zaidi ya waongoza njia, Alex na Julius.

Hata hivyo, nje ya msitu tuliwaacha kina dada wawili walioshindwa kuingia baada ya kuambiwa, hawangeruhusiwa kwa kuwa walikuwa kwenye siku zao.

Alex alirudia tangazo la kujipanga mstari mmoja mithili ya siafu. Hakutaka kuona watu wanatembea kwa kujiachia, isipokuwa kwa nidhamu ya hali ya juu.

Hakika Nyumbanitu inatisha. Si kwa vitu na simulizi zake za ajabu, bali hata masharti ya kuingia na kutoka yanayoweza kukufanya, ughairi safari yako na kurudi ulikotoka.

INAENDELEA KESHO
 
Mim huwa sielewi kwa maandish tu pekee, hata ungeelezeaje na kwa mifano gani.......
Ila ukiniwekea picha tu......naelewa haraka sana hadith zenu. Kwa hyo hapa nimetoka kapa sababu ya kukosekana kwa picha.
 
duh Niko Mafinga na njombe sio mbali/.....nitaenda kuona hayo maajabu
 
Binafsi kuna kipind nilikwenda Njombe kikazi, izo habar nilizisikia sana, nilivo ambiwa ni msitu wa matambiko ya kibena, nikasema sitagusa kwenye huwo msitu
 
Hakuna cha ajabu hapo ndo mana umeenda kujipanga ili utudanganye, kwanza umeandika kama fasihi, unaanza stori then unarejea mwanzo tena. Muongo utamjua tu anatumia nguvu nyingi sana.
 
Mkuu kesho ukiiweka usisahau kunitag
 
Mim huwa sielewi kwa maandish tu pekee, hata ungeelezeaje na kwa mifano gani.......
Ila ukiniwekea picha tu......naelewa haraka sana hadith zenu. Kwa hyo hapa nimetoka kapa sababu ya kukosekana kwa picha.
Nadhani kwa masharti hayo hawakuruhusiwa kupiga tupicha tuwili tutatu
 
Back
Top Bottom