Msisubiri vikao vya kusuluhishana fanyeni"mapping" ya ndoa zenu kila mara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msisubiri vikao vya kusuluhishana fanyeni"mapping" ya ndoa zenu kila mara

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Sep 1, 2012.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,771
  Trophy Points: 280
  Pengine wakati ukimtafuta wako wa maisha ulikuwa unatafuta vigezo kadhaa najua sio vyote ulivyopata kwakuwa wewe sio mungu kumpa kila kitu mtu anaeitaji ukaona miaka inaenda ngoja nikabane nae huyu huyu...sasa basi kuna wengine waliangalia

  ...elimu
  .....ukabila
  ...uwezo wa familia pengine lazima wawe familia bora kama vijana wa mjini wanavyoita bila kujua wakwe walipataje wakaja kuwa na familia bora
  --wengine wanapenda awe ameokoka anamheshimu mungu na kuamini kupitia uoga wa wa kumjua mungu basi hata kwenye ndoa anakwenda kuheshimu familia
  na mengine mengi tu mwisho wa siku ukaamua sasa saa ya kupleekana kwa wazazi mkaamua kutangaza ucumba na wengine sitaki kwenda mbali wakafungishwa ndoa za mkeka wakiwa wanatambulisha mchumba sababu ya kumpa mimba binti bila ndoa...na mengine mengi tu

  turudi kwenye mada kamili ni vizur baada ya ndoa ukakaa kama miezi ama sita mkafanya tathmini ya ndoa zenu na hili liwe mfululizo na si kusubiri mpaka shetani aingie ndani muanze vikao vya ndoa sikuhizi wazazi wengine kuwatoa nyumban kwenda vikaoni ni dili kama unatoa mahari sasa sipendi iwe kwa mwana jf wapendwa...ni vizuri ukaangalia mpaka miezi hii sita mke wangu tulikorofishana nini na src ilikuwa ni nini ....na wewe mke unakaa na kadaftari chako cha 250 kama huna natoa bure..unaanika mambo ambayo unahisi mumeo aliwakuwa amekasirika na kuhaatarisha hali ya usalama kwenye ndoa zenu nasema hivi nikimaanisha wachungaji sasa wamechoka kusuluhisha ndoa na wengine hata kuwageuka wanandoa ....so sipendi hili li kukute kaaeni chini na si lazima umwambie mwenzio ulichomuuzi wewe mwenyewe ukijua unaweza kubadilika labda nikupe mfano tu

  m mkew angu nilikuwa nikirudi saa tatu na zaidi bila kujua nimepita wapi ndani unakula fresh na unyumba ukitaka unapewa lakini sura itakavyonuna hata asbh unatamani iwe usiku huo ..so ukiwa na akili unhama mapema na kama unajua mida hii inakaribia saa tatu na bahati nzuri nae ni mtandao mmoja basi nanyanyua simu naongea dk 1 nikifika nyumban swafiii nakuwa na amani....mambo aya tusimpe shetan nafasi jamani wakati mwingine shetani ni sisi wenyewe usisubiri kumekucha ndio unahisi kumwambia shengena, mapande, darleo ama saibaba umepata na shida ukahisi mawazo yake yaatakusaidia wanakucheka kwa nyuma nasema kwa kumaanisha....matatizo ya ndoa ni wawili tu hata ukita wazazi mara 10 kama mtashindwa nakwambia hata mwende israel ama vatican kuhiji ayaishi...

  So all in all nionacho hapo ni ukosefu wa ufahamu..nasemaga na sitoacha kusema kuliko mungu akunyime mwana jf ufahamu bora akunyime uajiri akupe ufahamu na ufahamu aununuliwi ni kumjua mungu na kuishi katika matendo yanaompendeza yeye basiiiiiiiiiiii usitarajie unatoka kupiga nyumba ndogo usiku urudi nyumbani ukute amani labda ya syria

  kila la kheri wanandoa wote mliopendana siku ya leo akikisheni amkutamaniana maana najua mshatoka kanisani na sasa ni too lte kurekebisha
   
 2. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2012
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 556
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Huu nao ni ubani tosha wana MMU
   
 3. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #3
  Sep 1, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Hapa kweli umenena!
  Kama ndoa zitajengwa kwa misingi ya kukaa chini na kuongea kamwe hakutakuwa na ugomvi na kuvunjika kwa ndoa!
   
 4. c

  christmas JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2012
  Joined: Jul 21, 2011
  Messages: 2,608
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Gud idea, nimeipenda watakuelewa tu didy
   
 5. Sydney

  Sydney Senior Member

  #5
  Sep 2, 2012
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kiukweli umeongea ndugu, lakini ni kuna magume gume mengine hayakubali kukaa na kutathimini yanakimbilia kwa wazazi tuu, ninao mfano hai mimi na mwenzangu tulitokewa na tatizo yaani gumegume langu hata sms zangu alikuwa anasoma yeye kisha anamwonyesha na baba yake mazazi, hii ilikuwa inanikera sana na hata nilikuwa namdharau sana hata mpaka leo. Yaani hata sometime mimi kama mwanandoa nagundua hapa tumeteleza na naanza kumwambia mwenzangu tukae tuzungumze yaani anavyoanza kupagawa kama mwehu mara oo nimeamua sina la kuongeza, mara ooo tukubaliane kutokukubaliana, mmh.... DUNIANI KUNA MAMBO! Kiekweli sasa nimeshindwa napigana na maisha mwenyewe!
   
 6. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Mawasiliano ni tool mojawapo nzuri kwenye kujenga na kuimarisha mahusiano ya wanandoa huku mkiyarejea mazuri yote mliyotendeana kwa minajili ya kuyaboresha na yale mabaya ni vyema kuyaongea kwa nia ya kusaidiana na kufahamishana ili kuyaacha kabisa yasigeuke kwazo ndani ya ndoa.
  Asante Pdidy kwa mada nzuri.

  Kila la kheri wanandoa wote.
   
 7. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #7
  Sep 2, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Pdidy asante sana kwa somo hili zuri. Kweli kabisa mawasiliano ya mara kwa mara na ya karibu ni ya muhimu sana kwa wanandoa. Hutakiwi kuacha kufanya tathimini ya ndoa yako kila baada ya muda kujua ulikosea wapi na wapi unatakiwa ujirekebishe. Kujua mapungufu yako na kujaribu kuyaondoa. Sio swala la mnakaa ndani ya nyumba mwaka hamjawahi kuongea au kujitathmini kujua je ndoa yenu iko imara au ina mapungufu.
  Asante sana mkuu
  Mafanikio mema kwa wanandoa wote.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...