Msishangae wapinzani kutangazwa kushinda baadhi ya maeneo pamoja na kugomea uchaguzi

Kamgomoli

JF-Expert Member
May 3, 2018
1,865
3,802
Kila kitu kinalazimishwa utake usitake. Hii ndo slogan ya awamu ya 5. Wapinzani wamejitoa uchaguzi lakii serikali imetoa kauli kupitia Waziri husika kuwa uchaguzi utaendelea na wapinzani walioteuliwa watashiriki watake wasitake. Kwa utabiri wangu kitakachotokea ni mchezo ule ule wa kitoto.

Kwa baadhi ya kata mtashangaa wapinzani wameshinda, ku-fix mambo ili ile taswira ya demokrasia ionekane. Yaani wao ndio wataamua mpinzani gani wampe uenyekiti wa mtaa husika. Pia, naona harufu ya mapandikizi kama wale waliounga juhudi. Ambao watashiriki uchaguzi na hao ndio watakaotangazwa kushinda. Nyie subirini episode ijayo mtaamini maneno yangu.
 
Kamgomoli,

Kwa awamu hii ya 5 inawezekana kabisa kama kiranja mkuu ndio alivyokuwa anafanya kipindi cha nyuma kupita bila kupingwa.
 
nadhani mkisikia hivyo mnatakiwa mfurahi sasa maana nao pia watakuwa wamewarahisishia kazi.
 
Haisaidii kitu hapo, hauwezi kufanya kila kitu mwenyewe hata akiweka wapinzaji, hapo mboga ilisha zidi chumvi imwagwe tu.
 
Back
Top Bottom