Elections 2010 Msipojipanga mtakosa kura

Mdanganywa

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
620
342
Tangu Jumatatu list ya wapiga kura imeshabandikwa vituoni. Hivyo muda wote wa wiki hii ni muda wa mtu kuhakikisha jina lake lipo kama lilivyoandikwa kwenye kitambulisho cha kupigia kura na kama namba ya kitambulisho chake ilivyo.

Imegundulika kuwa wengi hawajatilia uzito na hadi sasa hawajaenda kituoni na kugundua usumbufu unaoweza kujitokea.

Kuna vituo vina zaidi ya wapiga kura zaidi ya 6,000 na hivyo imebidi kugawanya majina kwenye mafungu manne au zaidi ya watu wasiozidi 500. Kuna mafungu A, B, C, D na hata zaidi ya hapo. Vilevile hata ile A imegawanyika zaidi na kuwa A-1 , A-2, A-3 au zaidi

Kabla ya kufika kituoni huwezi kujua hali hii na hivyo mtu anadhani kwamba akifika kituoni ni ni rahisi kupata jina lake kwamba kiasi cha kuangalia jina kwa alphabet order.

Wengi wanatumbukia katika mtego huu kwani mtu anafika kituoni na badala yake anajikuta ameangalia jina lake kweli kwa alphabet order lakini kumbe ameishia kwenye fungu A peke yake ambalo nalo limegawanywa A-1 , A-2 na A-3 au zaidi.

Hajui kwama inabidi afanye akikosa jina kwenye A yenye A-1 , A-2 na A-3 inabidi afanye hivyohivyo kwenye B, C na D.

Nimeshuhudia wengi tu wakikata tamaa anapokosa jina kwenye A ambako makaratasi ndipo yalipoanza kubandikwa. Matokeo yake anaamua kuondoka akinung'unika kwamba akidhani jina lake halipo. Binafsi nimeshiriki kusaidia watu wa aina hii kupata majina yao na walikuwa kweli wameshakata tamaa.

Lakini bado licha ya usumbufu huo tu anaondoka akidhani imetosha bil kufikiri kwamba anatakiwa aandike kuwa ameona jina lake kwenye A-1 au B-3 au C-2. Hivy ni wazi Jumapili ataanza tena kutafuta ili ajipange. Naamini hata humu JF kuna watu wanaweza kuwa ni wahanga wa tatizo hili. Kwamba ukimuuliza yuko mstari au chumba gani hatajibu zaidi ya kusema ameona jina lake na inatosha.

Hakika hii italeta usumbufu mkubwa itasababisha kuwe na vurugu ya kutafuta majina badala ya kufika na kwenda moja kwa moja kwenye foleni.

Sioni hili likihubiriwa kama tatizo. Tusitegemee NEC itutafunie kila kitu kwani ukombozi uko mikononi wetu. Vilevile tusisukume mzigo kwa vyama kututangazia namna ya kupuguza usumbufu bila sisi kutoa ushirikiano wa kuhabarisha vitu ambavyo vimo ndani ya uwezo wetu.

Wewe uliyegundua hili na uliyepata habari hii tuma hata message 10 tu za simu kwa rafiki zako na wao watatuma kwa 10 zaidi na ujumbe utawafikia wengi.

Wanabuni mbinu za kuvuruga uchaguzi wana mwaka hawalali wakibuni mbinu hii na ile. Wewe unashindwa vipi kuiweka hii wiki nzima ya kudhibiti mbinu hizo ikiwemo hii ambayo inatosha kabisa kuleta usumbufu bila hata kuongeza mbinu zingine!

Waambieni wenzetu, kwamba waende kituoni kisha waangalie wako kwenye mpangilio upi. Ukikosa kalamu na karatasi basi andika kila kitu kama vile unatuma message ya simu na kisha badala ya kuituma inai-save hadi Jumapili.

ZAIN na nadhani mitandao mingine imeanzisha code unayoweza kuangalia jina lako kama lipo kwenye kuto fulani. Ni kiasi cha kutuma namba ya kitambulisho chako (Vote ID) kwenye 15455 kisha umtandao unakuletea majibu.

Wenye uwezo wa kuangalia internet tumshajadili humu kwamba ni kiasi cha kufungua website ya NEC na kuingiza Vote ID kisha bonyeza SEND. Website ni {www.nec.go.tz/?modules=reg_status&sub}.

Tuelimishane kwamba unaweza kwenda kwenye internet CAFE au unaweza pia kutumia simu zenye internet. Uchache wa simu hizi hautuzuii kusema uwepo na matumizi yake kwani mimi nimemsadia mmoja aliyekosa jina lake na imesaidia kwani kwenye internet tuliweza walau kujua mtu yule yuko kwenye B na tukaenda moja kwa moja B-2 tulipokuta jina lake wakati alikuwa ameshakata tamaa.

Sijui wenzangu mnasemaje na ni ruksa kuboresha wazo hili
 
Back
Top Bottom