Msione vyaelea mjue vimeundwa:Wapinzani wanashindwa kusema ila wanaamini Rais bora atatoka CCM. Hakika CCM ni chama cha wote.

FPT

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
1,201
1,839
Nderemo, vifijo na bashasha huonekana Dodoma kwenye mwaka wa uchaguzi na kuhitimishwa pale mtangaza nia wa CCM anapopendekezwa kuwa mgombea urais. Furaha inayotokea Dodoma inarindima kila kona ya nchi na wengine mpaka kufikia hatua ya kusema' rais ni nani?' ,' amekuwa rais tayari?' hata kama uchaguzi haujafanyika. Hii ni ishara kwamba kila mtanzania ana matumaini na matarajio makubwa ya kuendelea kuongozwa na CCM na wanaamini mgombea urais kupitia CCM ndio rais kwa sababu ana sifa na uwezo wa kuwa rais.

Si CCM tu ila hata wapinzani na watanzania wote kwa ujumla hufuatilia kila nukta ya tukio linaloendelea Dodoma wakati wa mchujo wa watia nia na vyama vingine hutamani hata wale ambao walitangaza nia lakini hawakupendekezwa wawe wagombea wao. Hii ni ishara nzuri kwamba hata upinzani bado unaamini na utaendelea kuamini kuwa Rais bora na aliyebeba matarajio ya wananchi lazima atoke CCM au awe mwana CCM hata kama ni mgombea wa upinzani.

Kwa nini watanzania na hata wapinzani wanaamini Rais Bora atatoka CCM?

i. Urais unahitaji maandalizi na uzoefu : kipimo kimojawapo cha kuwa Rais bora ni kuandaliwa vema kiungozi ili kuweza kushika madaraka hayo makubwa katika nchi. Maandalizi ninayozungumzia hapa si yale ya kufundishwa darasani kama taalumu ila ni yale ambayo mtu anayapata kupitia uongozi mbalimbali wa kitaifa anaopitia. CCM kuna viongozi wa kitaifa wengi kama mawaziri ambao wote wanapata uzoefu na maandalizi ya kuwa ma-Rais. Hii ni moja ya sababu inayowafanya hata upinzani waamini Rais bora aliyepata maandalizi na uzoefu atatoka CCM. Msione vyaelea mjue vimeundwa, Rais Magufuli alipata maandalizi ya miaka 15 kama waziri.

ii. Urais unahitaji umakini na uthubutu: Linapokuja suala la umakini na uthubutu kwa watia nia wa CCM si jambo la kujiuliza mara mbili mbili.mfano ni rais Magufuli alikuwa na uthubutu sana alipokuwa waziri na sifa za watu makini na wenye uthubutu zimejaa tele CCM. Watanzia wasio na vyama na wale wapinzani wanaamini kuwa viongozi wenye uthubutu na makini wapo CCM na kupitia viongozi hao CCM ndio inaweza kutoa Rais bora.
itaendelea

Na Karlo mwilapwa
 
Back
Top Bottom