Msiokuwa na kazi na mnajidekezadekeza kitaa huko soma hapa!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msiokuwa na kazi na mnajidekezadekeza kitaa huko soma hapa!!!!

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Marketer, Sep 10, 2012.

 1. M

  Marketer JF-Expert Member

  #1
  Sep 10, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 261
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nawasalimu wakuu!

  Nimeguswa kuyasema haya kutokana na tabia ya watu wachache wenye viherehere humu JF vya kuponda baadhi ya opportunity zinazotolewa na wadau humu wenye mioyo ya huruma kwa wasio na kazi.

  Kitu cha muhimu kumbuka HUNA KAZI hivo usidharau na kukashifu any opportunity, kutoridhika na nafasi iliyopo its okay, sawa hujaridhika basi endelea kusoma thread zingine sio kuponda manake kwa yule mwenye shida utamkwaza kuikubali ile nafasi. Isitoshe kazi ni heshima hata kama hailipi ila unaamka unaoga asubuhi, mkaa bure sio sawa na mtembea bure, mtembea bure huenda akaokota.

  Katika safari yenu ya kutafuta kazi naomba niwashauri machache

  1. MSIJIDEKEZE. Kama unatafuta kazi mda na hujapata basi ujue hutafuti vya kutosha! Wewe uko mkoani unachofanya ni kuingia zoom na kuapply kumbuka mko million na wote mnaingia na kuapply hata wakipata 100 kila siku uwezekano wa kufikiwa ni mdogo. Kuweni wabunifu/creative kwenye kusaka ajira. Mfano nunua lakuchumpa lako amkaa saa kumi na moja kama wenye kazi, anza kudondosha bahasha yenye cv na criteria zako ofisi mpaka ofisi, wiki nzima hata mwezi ikibidi, trust me Mungu si athumani utapata hata moja, japo soli ya viatu itakuwa imeisha.

  2.ACHENI MASHAUZI. We mtu umetoka chuo hata experience huna unapeleka cv ina title Accounting Manager/ Senior Accountant etc, yaani hata mtu hasomi hadi mwisho anaona hujielewielewi. Wewe mahali huna ndugu japo wa kusingiziwa, peleka cv andika any post that fits my qualifications, utapewa hata ucashier au assistant accountant ambayo ni better 100% kuliko kukaa nyumbani. Seriously unaweza kuwa unapeleka sana cv huitwi sababu unachokitaka hakipo, ila ukiomba chochote kilichopo utapata mapema.

  3.HAKUNA KAZI NZURI UJANJA WAKO TU. Unaweza kupata kazi amabyo contract mbovumbovu haina hata mvuto, ukaikataa kumbe usilolijua litakusumbua. Kamwe usikatae kuripo kazini kisa mkataba hujakuridhisha, we karipoti tu maybe ufanye hata mwezi ndo uache. Nasema hivi coz kuna kazi hasa hizi zetu za masoko/marketing unakuat mshahara take home 300,000 Mind you hapo una masters yako, unaweza ukakataa, ila nikiwa nina mdamrefu kwenye fani hii nakwambia kubali, coz unaweza kuta comissions hadi 6,000,000m kama utaclose big deals. This is a Fact! sasa hizi comission kwenye contract hazionekani, hiyo siri ya biashara unaweza kuwa umeacha best job you may ever get. Acha comission kuna kazi za Procurement 10% hazionekani kwenye mkataba. Kuna kazi zina mideal ya hatari ambayo ni nomaaa, mshahara ushahidi tu.

  4.UKIONA UNATAFUTA KAZI FLANI HUPATI JUA RIZIKI YAKO HAIPO HUKO. Mimi kwa profession ni Accountant, tena nina C.P.A bt sikuwahi kupata kazi ya uhasibu nikaridhika nayo, actually nilikuwa napata bt kazi tembo mshahara sisimizi, kuna rafiki yangu akanitafutia kazi za marketing sikufurahi, tena nilipanga nisiende, bt akanipa altmatum nifanye for 2 weeks nikiboreka niache, nikaenda kutest zali, Nikagundua Marketting is the DEAL. Mishahara midogo ndio, ila allowance za hatari mara 3 ya mshahara, sijui vocha, transport, facilitation, entertainment, acha illegal kama 10% za kuzidisha bei.Im officially a marketer. In short usifocus kuwa in your life lazima ufanye kazi flani, think wider, unaweza kuta kuna kazi nzuri kuliko unayotafuta hujajua tu na ndo riziki Mungu aliokupangia.

  5.MTAMALIZA MABUCHA NYAMA NI ILE ILE! Utakuta mtu ukobusy kutafuta kazi in big organisations, its good ila ujue tu mishahara haipishani. Rate za banks ni 300000 , 400000, 500000, 600000 take home chache zinafika mpaka 800,000take home kwa garduate ila nyingi ni 400000 -500000 sasa unaweza kuwa mahali ukahisi unadhulumiwa ukawa mnyonge na kiburi kingi, ukaona wenzio wanafaidii kumbe mnapata sawa sema yeye anabebwa na jina la Bank tu. Watu hawasemi mishahara ya ukweli ila rate ni zile zile tu, so ni heri uridhike na ulipo na kufocus kupanda cheo kuliko kukazana kuhama.

  Nimechoka kutype bado nina mengi ila kwa haya yatawafumbua macho na kuwarudisha baadhi yenu kwenye straight line 180degree

  ATAFUTAE HACHOKI AKICHOKA KAPATA, ZIDISHENI MAPAMBANO.
   
 2. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #2
  Sep 10, 2012
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,236
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  Nilianza kazi 07/08/2007 kwa gross ya 350000/ baada ya mwezi 2 niltamani kuacha kwani pressure ya mauzo ilikuwa kubwa na mwisho wa mwezi kipato kiduchu but somebody advised me to hang in there for while, duh baada ya kuzoea kazi na macommission, madeal yaani hamna kazi nzuri kama ya sales, now my take home is 1.8m, company car 24/7,house rent not exceeding 400000/per month, with my CBe diploma am in cloud nine.
   
 3. Triple G

  Triple G JF-Expert Member

  #3
  Sep 10, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  ahsante mkuu nimejifunza kitu hapo kwa busara zako.
   
 4. M

  Marketer JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 261
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkuu na wewe usimwage mtama kwenye kuku wengi hawa masharo baro kuzunguka juani wataweza? wanataka AC na kugonga mihuri na signature, kiyoyozi cha kwenye gari kinaleta mafua.

  Seriously sales and marketing pays
   
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Sep 10, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Opportunities zilizokuwepo Tanzania sasa hivi ni kuliko Afrika nzima au hata Ulaya na Amerika, ukweli ubaki kuwa Ukweli, kazi ni nyingi sana, labda uwe mzembe tu.
   
 6. peri

  peri JF-Expert Member

  #6
  Sep 10, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  mmenena vzr sana wakuu, tatizo linaanzia watu wanapokuwa vyuoni wanakuwa na expectation za ajabu mno, kubwa kupita kiac.
  Wanapokuja kukutana na maisha halisi wanapata shida kuyakabili.
  Unakuta mtu ni fresh hana uzoefu hata wa wiki moja but anakuwa na mawazo ya kuajiriwa kampuni kubwa tena ktk nafasi ya juu.
  Hizo ni ndoto za mchana.
  Wapo wengi wamekalia vyeti wanasubiri ajira ziwafwate badala ya kuzifuata wao.
   
 7. s

  suli Member

  #7
  Sep 11, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 57
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  nakusalute wewe mtoa mada, umeongea kweli tupu ! aksante sana
   
 8. s

  sajosasi Member

  #8
  Sep 11, 2012
  Joined: May 27, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  shukran
   
 9. V

  Von Mo JF-Expert Member

  #9
  Sep 11, 2012
  Joined: May 7, 2012
  Messages: 1,830
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Nimemkubali mtoa mada naunga mkono kwani kabla sijapata kazi nilifanya application zaidi ya 200 na kuzunguka ofisi karibia zote, lakini nilibahatika kuitwa interview 20 na nilihudhuria interview 7 na nilipata nafasi mbili nimechagua moja...lakini kimsingi nimetafuta kazi kwa bidii sana, mpaka kuna kipindi nilimlilia Mungu kwa Maombi, namshukuru Mungu sana. Ni kweli ndugu zangu jitahidini kufuata ushari wa mtoa mada
   
 10. Obama wa Bongo

  Obama wa Bongo JF-Expert Member

  #10
  Sep 11, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 4,767
  Likes Received: 2,494
  Trophy Points: 280
  asante kwa ushauri be blessed
   
 11. F

  Fmewa JF-Expert Member

  #11
  Sep 11, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 294
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ushauri wako ni mzuri sana ndugu mtoa mada, nimefurahishwa sana. Ni kweli vijana wengi tunatamani kupata post za juu mara baada ya kumaliza vyuo, kumbe inabidi tufahamu kuwa maisha huanza hatua kwa hatua matokeo yake unafikia lengo.
  Kwenye point no 4 uliyotoa hapo juu nimekumbuka kua mimi nimesoma computer engineering lakini ktk kutafuta kazi za IT sikupata nikajikuta nimepata kazi inayofanana na kazi za Call centre wenyewe tunaita Network Operation Centre ni kazi ambayo sikuifikiria na niliidharau ila baada ya kuifanya nimegundua kua kazi nzuri na im proud kufanya kazi hiyo.
  Siku moja niliitwa kwenye interview ya IT Technician lakini wakati nafanya interview yule HR alipoisoma CV yangu aliniambia nisihangaike kutafuta kazi za IT kwani sina uzoefu nazo akanishauri niendeleze kazi hii ambayo naifanya na nina uelewa mkubwa ktk hiyo.
  Kwa sasa nimeacha kukariri mambo ya kutafuta kazi niliyosomea.
  Thanks
   
 12. Penguin-1

  Penguin-1 JF-Expert Member

  #12
  Sep 11, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 400
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  kimsingi umenifanya niongeze juhudi na kuwa na matumaini
   
 13. mojoki

  mojoki JF-Expert Member

  #13
  Sep 11, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 1,333
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ahsante sana kwa ushauri ndugu mtoa, Lakini bado siwezi kufanya kazi ya kuzungusha vyombo mtaan bora niendelee kuonekana mchagua kazi
   
 14. Lucas

  Lucas JF-Expert Member

  #14
  Sep 11, 2012
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 2,451
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  And may God bless you
   
 15. herrypeter1

  herrypeter1 JF-Expert Member

  #15
  Sep 11, 2012
  Joined: Jan 17, 2009
  Messages: 224
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu Mtoa Mada, Ningependa kuchangia mada hii kama ifuatavyo.........
  WAWEKEZAJI WAKATI WA UKOLONI WALISEMA ATUNA ELIMU, WATANZANIA SASA WANA ELIMU WANASEMA ATUNA EXPERIENCE,
  Moja ningependa ueshimu kazi ya marketing as professional ambayo ndo inaendeleza kampuni yoyote kwa kiasi kikubwa but now days watu wamekuwa wakizarau watu wa marketing na kuwafanya kama walimu wa vodafasta.......tuchukuie mfano mtu kasomea engineering unampeleka marketing, Tatizo lilipo na tanzania yetu atueshimu professional na ndo maana muundi anaposhindwa kumpata mtu kutokana na professional yake anaajiri mtu yoyote tu, mtuu mwenye professional yake akubali salary ambayo akuipanga kupata, WHAT IS PROFESSIONAL, TANZANIA WAKATI WA UKOLONI, WAWEKEZAJI WALISEMA ATUNA ELIMU, WATANZANIA SASA WANA ELIMU WANASEMA ATUNA EXPERIENCE,
   
 16. M

  Mudamali Member

  #16
  Sep 11, 2012
  Joined: Jun 15, 2012
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aisee hauko peke yako. Mwenyewe kanipa moyo kuongeza juhudi za u afutaji. Ubarikiwe mtoa mada, umefikiria mbali sana. Thx.
   
 17. M

  Marketer JF-Expert Member

  #17
  Sep 11, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 261
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Exactly Femwa duniani it doesnt matter what you do bt how you do it! Trust me ungepata IT technician ungeonewa mshahara coz kutokuwa na experience kungekupa inferiority complex, bora uji upgarde hapo uombe senior position za hiyo nafasi. What counts ni mpunga unaovuta.
   
 18. M

  Marketer JF-Expert Member

  #18
  Sep 11, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 261
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Herry unakosea kitu kimoja HAUKO PEKE YAKO UNAETAFUTA KAZI, na ukikaa nyumbani apart from kuwa professionless unakuwa jobless and at the same time you hurt so many people wanaokutegemea nawaliokuaminia and it kills your comfidence. The system is bad sawa sasa usiporipoti kazini do you expect itabdilika? FIGHT THE SYTEM FROM THE INSIDE.
   
 19. M

  Marketer JF-Expert Member

  #19
  Sep 11, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 261
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  sisemi ujishushe that much ila usifocus kwenye tittle ya kazi, saa nyingine zinga la cheo ila mpunga wa mawazo.
   
 20. herrypeter1

  herrypeter1 JF-Expert Member

  #20
  Sep 11, 2012
  Joined: Jan 17, 2009
  Messages: 224
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kukiwa na watu kama nyinyi mia ambao mnafanya bora mambo yaende ili mradi upate ata watoto wenu wataishii ivyo ivyo, have your own way mr
   
Loading...