"Msininyanyase, mimi si mpinzani," kada wa CCM awaasa Jeshi la Polisi

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,064
22,757
"Msininyanyase, mimi si mpinzani," alisikika kada wa CCM wakati polisi wakimbembeleza kama mwana mtukutu apande gari wamsindikize kwenye tawi lao mjini Dodoma baada ya kufanya maandamano wakilalamikia uteuzi wa wagombea wao.

Bila shaka angekuwa mpinzani hicho kipigo ambacho angekipata kutoka mikononi mwa polisi angekuja kuwasimulia wajukuu zake lakini badala yake polisi wanaonekana wakimsihi apande gari na kutoa maelekezo kama vile ni makada wa CCM.

Sasa si ajabu tukashuhudia haya:
  • Msemaji wa Polisi kimyaaa!
  • Msemaji wa Msajili wa vyama kimyaaa!
  • Msemaji wa Tume ya uchaguzi kimyaaa!
  • Msemaji wa vyombo vya dini kimyaaa!
  • Msemaji wa serikali ya Mkoa kimyaaa!
  • Msemaji wa serikali kuu kimyaaa!
"Oh judgement, thou art fled to brutish beasts and men have lost their reason!"

Pia soma > Uchaguzi 2020 - Vurugu zatawala ofisi za CCM baada ya walioshinda kura za maoni Udiwani kukatwa
 
Ninachoamini ni kwamba "Kila ulimi utakiri wenyewe na hakuna jiwe likakalobakia bila kugeuzwa" Udhalimu na uonevu ni mbegu mbaya sana ambayo haiozi hata ikakaa muda mrefu kiasi gani. Itachipua tu na kuleta matunda kwa wote hasa wale waliokuwa wanajiona wako salama zaidi.
 
Kimya kina kishindo, na hivi sasa tunashuhudia kishindo cha ukimya wa miaka minne. Kwa miaka minne mfalme anapita mitaani akishangiliwa na waumini wake.

Ghafla anatokea jasiri moja na kuwashangaaa washangiliaji kwa nini wanashangilia aibu ya mfalme kutanua mitaani bila nguo!

Ghafla ukimya unatanda utafikiri ule umati umemwagiwa maji baridi...umati unazinduka kama vile ulikuwa ndotoni! La haula! Aibu si aibu hiyo!
 
Yani kumbe CCM wanafahamu wazi kwamba wapinzani nchi hii wanaonewa, lakini wapo kimya wanatazama tu, na hao polisi wanajua huwa wanawaonea wapinzani lakini nao kimya tu, hawa watu wasipopata adhabu hapa duniani, basi wataipata tu mbele ya safari hata kama kila siku wanafanya mikutano na viongozi wa dini.
 
..huu uzi moderator ataushughulikia sasa hivi.

..kwa kweli CCM wameliharibu vibaya jeshi la Polisi.

..mpinzania angefanya kama huyu mwana-ccm sasa hivi tungekuwa tunaimba "parapanda."

cc Kilatha
Kwa mazingira ya siasa za leo unaposema sio mpinzani ina maana ni mtu uliestaarabika na mtiifu wa sheria ni kuwapa head start polisi awaitaji kutumia nguvu ili watu watii sheria.

Tumefikia huko kwa sababu wapinzani wanajulikana wao huwa awataki kusikia maelezo ya polisi wala kutii sheria wanapofika kitu cha kwanza ni ujeuri.

Kwa ivyo unaposema wewe sio mpinzani hasa wa CDM mbele ya polisi ni kama unatoa maelezo lengo lako sio kuleta fujo. Si ulimsikia pia akisema yeye mwenyewe ndio aliezuia maandamano.

Unachoitaji ni mfano tu kwa kuangalia anachofanya Lissu mpaka polisi wamechoka wagombea wote wametulia yeye tu ndio fujo barabarani utadhani ni mgombea pekee.
 
.huu uzi moderator ataushughulikia sasa hivi.
..kwa kweli CCM wameliharibu vibaya jeshi la Polisi.
..mpinzania angefanya kama huyu mwana-ccm sasa hivi tungekuwa tunaimba "parapanda."
Halafu kuna watu kila siku wanalalamikia nyuzi zao kufutwa...mimi nawashangaa na naapa sitalalamika uzi wangu ukifutwa. Hao watu wangejua nyuzi zetu ngapi zinafutwa bila maelezo hata wasingelalamika! Ukishakuwa nguruwe, kulalamika ni rukhsa kwa sababu nguruwe hashibi anaweza kula 24/7. Fikiria wapo watu wamekula kwa miaka 60 na bado wanalalamika tu.
 
Kwa mazingira ya siasa za leo unaposema sio mpinzani ina maana ni mtu uliestaarabika na mtiifu wa sheria ni kuwapa head start polisi awaitaji kutumia nguvu ili atii.

Tumefikia huko kwa sababu wapinzani wanajulikana wao huwa awataki kusikia maelezo ya polisi wala kutii sheria.

Kwa ivyo unaposema wewe sio mpinzani hasa wa CDM mbele ya polisi ni kama unatoa maelezo lengo lako sio kuleta fujo. Si ulimsikia pia akisema yeye mwenyewe ndio aliezuia maandamano.

Unachoitaji ni mfano tu kwa kuangalia anachofanya Lissu mpaka polisi wamechoka wagombea wote wametulia yeye tu ndio fujo barabarani utadhani ni mgombea pekee.
Kilatha, sijui una miaka mingapi ndugu yangu ila kwa ufahamisho tu kuna kumbukumbu ya kada wa CCM aliwahi kumkata mtama mkuu wa kituo cha polisi hadi kofia ikadondoka lakini afande kwa unyenyekeu aliokota tu kofia yake na kada hakufanywa kitu.
 
Japo sio msemaji wao polisi awawezi kumuacha huyo kada miaka 800. Leta ushahidi, litakuwa jeshi la ovyo kama hayo usemayo yana ukweli.

Hiyo video unayo refer tu leo yule bwana alikuwa mstaarabu ndio maana naona akapewa treatment ile.

Na ndio lengo la polisi sio kutumia nguvu kwanza. Isipokuwa wana respond kutokana na resistance wanayokutana nayo sio itikadi za mtu aliembele yao.

Tatizo CDM huwa wakaidi na awatoi ushirikiano mara nyingi.
 
Kwa mazingira ya siasa za leo unaposema sio mpinzani ina maana ni mtu uliestaarabika na mtiifu wa sheria ni kuwapa head start polisi awaitaji kutumia nguvu ili watu watii sheria.

Tumefikia huko kwa sababu wapinzani wanajulikana wao huwa awataki kusikia maelezo ya polisi wala kutii sheria wanapofika kitu cha kwanza ni ujeuri.

Kwa ivyo unaposema wewe sio mpinzani hasa wa CDM mbele ya polisi ni kama unatoa maelezo lengo lako sio kuleta fujo. Si ulimsikia pia akisema yeye mwenyewe ndio aliezuia maandamano.

Unachoitaji ni mfano tu kwa kuangalia anachofanya Lissu mpaka polisi wamechoka wagombea wote wametulia yeye tu ndio fujo barabarani utadhani ni mgombea pekee.
Akili zako
 
Uza ubongo huo maana unakaa nao kwa hasara.
 
Back
Top Bottom