Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameeleza Bungeni kuwa hivi karibuni serikali itaifufua reli ya kwenda Arusha kupitia Segera na Moshi. Pia amesema serikali itaifufua reli ya kwenda Tanga, na kujenga reli toka Mtwara, kupitia Tunduma hadi Mbamba Bay. Mpango ni kujenga reli hizi katika standard gauge.
Wana JF acha mnilaumu, lakini ukweli ni kwamba siamini hiki kilichosemwa na Waziri Mkuu. Naona hapa alikuwa anafurahisha genge tu, na kama wabunge wameamini haya maneno basi wanaweza kuamini lolote watakalodanganywa na serikali (believe this and you will believe anything)
Labda kama Waziri Mkuu anamaanisha kwamba hizi reli zitafufuliwa miaka 50 ijayo, au siku tukipata mafuta yetu. Ikiwa ni hivyo basi si sahihi kwa Waziri Mkuu kuongelea kufufuliwa na kujengwa kwa hizi reli kama vile ni jambo litafanyika miaka miwili ijayo.
Au labda Tanzania inayohangaika kupata fedha za kujenga flyover hapa Dar na kulipa mafao ya wafanyakazi waliostaafu ina fedha kibindoni kuweza kufanya haya anayosema Waziri Mkuu? Iweje serikali imeshindwa kulipa mafao ya wastaafu wanaosubiri zaidi ya miaka mitatu na iongelee kujenga na kufufua reli zote hizi? Au serikali imeamua kwa makusudi kuwadhurumu wastaafu ili kutekeleza miradi yake ya kukiinua chama tawala?
Is the Prime Minster trying to insult the intelligence of, not only honorable MPs, but all Tanzanians?
Siamini hata kidogo alichosema Waziri Mkuu. Naona kaongea propaganda tu kwa ajili ya chama chake.