Msingi wa Biashara ya HUDUMA (sio lazima uuze bidhaa, Unaweza fanya biashara ya huduma)

Kibenje KK

JF-Expert Member
May 28, 2016
267
380
Kwa Tanzania ukiwa na Biashara ya huduma unaonekana kuwa Huna Biashara. Mpaka Uwe na Bidhaa za Kushika mkononi kama nguo,Kalamu,majembe,nk..Hapo Ndo unaonekana kuwa MFANYABIASHARA. Hiki kitu Siyo Sahihi hata Kidogo. Kwa sababu huduma ni sehemu ya biashara pia.

Na Nchi Tajiri zaidi kama USA,UK,China ...Zimewekeza zaidi katika huduma kama usafirishaji,utalii,Elimu,Afya,Sanaa,burudani,ufundi Nk. Huku Nchi nyingi Zimewekeza katika Bidhaa ambazo bei yake mara nyingi MIAKA na MIAKA haipandi ya Kuanzisha Huduma fulani Wakati mwingine hazina Gharama Sana ( mara nyingi stating capital ndo kubwa Baada ya hapo mwendo wa faida kwa wingi)

Usitafute bidhaa tu tafuta hata huduma Ili uweze kujiajiri. % kubwa Elimu ya Darasani huandaa watoa huduma.( Jambo jema sana) Tatizo ni Kwamba Haitoi Elimu ya kujiajiri kupitia hizo huduma. Kumbuka kuuza Bidhaa ni rahisi sana kuliko huduma. Machinga kuuza shati na soksi pale kariakoo ni kugusa tu.

Mtoa Huduma ya utalii,usafirishaji, Sanaa, burudani, Ufundi, habari, MC, desgners, huduma ya Sheria nk..zinabitaji Branding kubwa Sana tofauti na Hapo utakuwa mtu wa Kawaida Sana na huenda usipate wateja wa kutosha.

Au kukosa Kabisa mtu wa Kukulipa Pesa. Ila kama Unauza bidhaa za kushikika kama Soda Au cement Kampuni lishafanya Branding wewe ni kumalizia kuuza tu( sijasema usijibrand) Kama unatoa huduma jenga Brand Imara Sana na kutengeneza Pesa halitatakua Tatizo.

Note,SHULE haifundishi somo la Branding.Jifunze Mwenye kwa kutafuta wataalamu . -( Naweza kukusaidia ukapata kozi ya Branding juu ya biashara yako. WhatsApp 0762815104)


Kelvin Kibenje

Mtaalamu wa mauzo na masoko
 
Mie ni mfanyabiashara natoa huduma ya kuweka aluminium kwenye milango na madirisha nawezaje kubrand biashara yangu
Tumia mitandao ya kijamii.

Kuwa na kazi au picha ya kazi zako na logo inayokutambulisha

Jitangaze
 
Back
Top Bottom