UWEZO_WAKO
Member
- Nov 17, 2010
- 39
- 4
Mwalimu aliwasema vizuri CDM, kwa nini nyie CDM hamjasema vizuri? Nauliza kulikoni? Nyerere maisha yake yalipofikia mwisho aliicha familia ambayo kwa hakika inapendwa na watanzania hasa kwa uadilfu wa mwalimu ikiwa ni pamoja na kazi nzuri aliyoifanya Mama yetu Maria kushiriki kikamilifu na yeye kwa nafasi yake. Huo ni kwa upande wa familia lakini kitaifa ni alama ya Taifa au Baba wa wote "Baba wa Taifa". Jina la Mwalimu linatumiwa kote nchini na sasa si la familia peke yao au la ccm peke yao. Kuna wazazi wengi ambao hawana hata ukoo na Mwalimu lakini wakaamua kuwaita watoto wao majina wengine Kambarage, wengine Julius, wengine Mwalimu na wengine Nyerere. Hivyo jina hilo kutumiwa na yoyote hakuna shida na asikudanganye mtu katika hilo. CDM nyie mmefanya nini au mmemuita nani jina la mwalimu. Ninauliza mnipe jibu.
Mwalimu Nyerere aliwahi kuwasifia CDM kuwa ni chama kinachoonyesha kuwa na mwelekeo mzuri, nafikiri aliyasema hayo kwa sababu mara nyingi alikerwa na mwenendo wa chama alichokiasisi yeye. Wakati mwingine aliona kuirekebisha ccm ni ngumu sana ila palipaswa pawepo na chama ambacho kitakuwa na maadili mazuri kitakachokuwa tayari kuchukua nafasi ya ccm. Mwalimu hata kuna wakati alitishia kurudisha kadi ya ccm. Hii ni kwa sababu ni mtu aliyekuwa amechagua jina zuri (Alithamini uadilifu na uthamani wa mtanzania) kuliko yeye kujilimbikizia utajiri na Dhahabu/Almasi. Leo kuna watu wanasema hamna haja ya kuwa na katiba mpya tutaendelea kuwekea viraka iliyopo.
Mwalimu alipoona CDM mna mwelekeo mzuri kwa nini hakunyamaza kwa ajili ya manufaa ya chama chake. Au hamjui ya kuwa alikuwa anawatia moyo kwa ajili ya nyie kuja kuisaidia nchi. Ninaandika haya kwa sababu tuna taka kasi zaidi ili lengo na dhana ya kuwa na upinzani iwepo kwa kiwango cha kutosha. Natumaini mmeona wananchi kuwapa kura nyingi wanataka mabadiliko, ccm ni shamba lililochoka (hakuna tena rutuba) linapaswa lipumzishwe.
Swali langu mnafikiria nini kwa ajili ya Jina la Mwalimu, pale mlipokuwa mnajaribu kulitumia jina la Mwalimu wakati mkijinadi kwa kuenzi Misingi bora aliyoiweka mwalimu hamkuona jamaa walivyokuwa wakali utafikiri wana hati miliki ya Jina. Kwanza hata mwenye jina alitaka kukihama chama chake lakini pia akawasifia nyie. Mimi nawauliza CDM mbona hamjamsema vizuri mwalimu inavyopaswa kuwa? Tumieni jina lake msione aibu, msingi alioujenga mwalimu bado ni mzuri shida ni ukuta, Msifikirie mtajenga juu ya msingi mwingine, msingi ni huo huo tunachotaka kufanya ni kubadilisha ma-engineer wa kujenga.
Nauliza tena CDM mmemuita nani jina la Mwalimu. Nasema msione aibu hata ndani ya CDM kama inawezekana kuwepo na taasisi ya jina la mwalimu fanyeni hivyo. Na hiyo ionyeshe namna amabavyo cdm inafanyia kazi za mwalimu. Mwalimu ana vitabu (ambavyo hata vingine vimefichwa haviko wazi), mwalimu ana hotuba za maadili, nk. Ni vizuri mkawa wabunifu ili pia kuondoa hali iliyopo watu kuita Mwalimu, mwalimu huku wanayoyafanya ni tofauti kabisa na matendo ya mwalimu. Kuweni wabunifu hata ikiwezekani chombo kitakachokuwa kinaratibu kazi za mwalimu watoe hata motisha kuvuta hisia za wananchi ili mradi wang'oe zana ya kwamba Mwalimu ni ccm. Uchaguzi uliopita kuna bibi mmoja aligoma kupiga kura akiomba aonywesha sehemu ya kumpigia Mwalimu maana kura yake alitaka kumpigia mwalimu, mtu mmoja akauliza unamaana unataka kuipigia ccm?. Swali hilo si sahihi, nikataa kabisa hii haikuwa lengo la huyo bibi, badala yake ingekuwa vyema kusema bibi alikuwa anatafuta kumpigia mtu ambaye ana uadilifu kama wa mwalimu...hiyo ingekuwa afadhali. Binafsi hata kama kuna siku CDM mtaiitisha kuwa maalumu ya kuenzi kazi za mwalimu ndani ya CDM hakika nitajumuika. Kweli CDM kiasi fulani mmejitahidi kuonyesha kufuata kwa vitendo yale mwalimu aliyoyaanzisha mazuri lakini swali langu linabaki pale pale MWALIMU ALIWASEMA VIZURI MBONA NYIE HAMJAMSEMA VIZURI MWALIMU? KWENU CDM MMEMUITA NANI JINA MWALIMU AU MNA MPANGO GANI?