Msimu wa wanasheria kutengeneza fedha ndio huu umewadia

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Kuna wanasheria wenye hadhi kubwa ambao ofisi zao zipo city centre maeneo ya samora, ohio, mirambo na mitaa ghali kama hiyo. Halafu kuna wale wanasheria wadogo ambao wamepanga kwenye nyumba za mitaa isiyo na majina.

Nadhani kipindi hiki ambacho TAKUKURU wametoka kwenye ile likizo ndefu, hawa wanasheria maarufu wanategemea neema kubwa. Kesi za ufisadi wa mabilioni ambazo mtu yupo tayari kutafuta mwanasheria wa bei kubwa, huja na neema kwa wanasheria.

Ni kama vile ninaziona simu zao zikiwa busy kwa muda mwingi wa zile saa za kazi majira ya mchana. Wateja wa wanasheria ni wale wenye nazo (mpunga) hivyo hata malipo ya kazi sio madogo.

Na kasi ya mapambano dhidi ya ufisadi ikiwa itaendelea hivi hivi, maana yake ni kwamba wanasheria wametangaziwa neema. Ndivyo maisha yalivyo, kile kinachotafutwa kwa nguvu za kusoma sana vyuoni, kinamfaa mtu kwa muda mrefu wa uhai wake. Hiyo ndio raha ya professions, kitapita kipindi fulani kigumu kiuchumi lakini ghafla inaibuka neema pasipo kutarajiwa.
 
Ni kweli mkuu, tulikuwa tunadharau masomo ya arts kwamba ni ya kinadada sasa tunajuta, jamaa wanapiga hela ndefu si mchezo
 
wale ambao waliteuliwa kuwa majaji kipindi cha mwisho cha vasco da gama wanajuta watamani bora warudi mtaani maana shavu la sasa ni zaidi ya shida
 
Back
Top Bottom