Phillemon Mikael
Platinum Member
- Nov 5, 2006
- 10,534
- 8,619
Napita njiani ,
Natembea kwa miguu,kwa Mtogole
Kwa mfuga mbwa, na makoroboi
kote kunafanana
kimya kikuu kimetanda
Natembea hadi kariakoo,
ni msimu wa sherehe ,wafanyabiashara kufurahi
watoto kuruka ruka ,wakisubiri zawadi
wazazi wanajichelewesha ,kurudi nyumbani
wakute wamelala
Akilini mawazo ,kusherekea au kulipa ada za shule januari
wanaume wanatamani kubinafsisha familia zao ..
wamama wasio uvumilivu ,wenye maungo ya haja wanakimbia nyumba zao
Umasikini Mbaya
Pengine kariakoo ,iliyosheheni pilika za kununua na kuuza,
sio mfano wa kweli , naona naota ndoto ..
Napanda gari ,nipate fika upesi
kutembelea masaki wanakoishi wazungu japo weusi wa rangi
Naingia mgahawani ,japo nipate kahawa..
Muuzaji aniambia biashara mbaya ni sana
hata walio wakubwa wamekata miguu kufika
Hawa siwaelewi , naenda zangu Ubungo ,
Pia Nitapita Mbagala zilipo stand za mikoani
Hali mbaya haikomi ,magari yamenuna
Ule msimu wa madalali kuruka nazo bei ,bei za nauli
Mwaka huu umekoma ...
Napiga japo simu ,nipate tuma salamu
kijijini kuwapa habari ,mbaya zisizokifani
kuwa nami nimekosa nauli ya mjomba kufika
Babu naye bibi ..,wanieleza masikitiko
Mabonde yote yetu ,yaletayo mazao .
Mwaka huu mbaya , bibi naye aliza
Kilimo kimekataa ,Tujiandae kwa njaaa
Tuma japo senti chache ,dada yangu asisitiza
Maisha ni magumu ,kesho ni majaliwa
Kweli haijapata tokea ,msimu ule mbaya
wa sikukuu kama huuu , hatujui kosa letu
Maulana Twakuomba , roho zetu ziokoe
Tuokoe na mikosi , mbali upate itupa...,
Kosa letu ,hatujui ,Yote haya kustahiki !!!
Tafakari yangu ,kuu
kimya hiki kutawala ,kila mmoja yu kimya
anayeongea ni nani ,mtabiri na mtafiti
wote wale wapo kimya
Wasijue la kufanya , kimya hiki kimezidi
wamuachia afanye ,lake yeye atakalo
ende akalitimize ,
Akikamatwa mmoja ,sisi wote tuwe kimya
akakamtwa wa pili , kuendelea na wa kenda
Tisa kumi wakamatwa ,wote kimya imekuwa
Anafukiwa wa mwisho , japo sio mtoni ..
wa kumtetea yupi ,jasiri aliyebaki
kimya hiki ,homa yetu
Tiba yake ,imekoma