Msimu mbaya wa sikukuu toka tupate uhuru

Phillemon Mikael

Platinum Member
Nov 5, 2006
10,518
8,583
Napita njiani ,
Natembea kwa miguu,kwa Mtogole
Kwa mfuga mbwa, na makoroboi
kote kunafanana
kimya kikuu kimetanda

Natembea hadi kariakoo,
ni msimu wa sherehe ,wafanyabiashara kufurahi
watoto kuruka ruka ,wakisubiri zawadi
wazazi wanajichelewesha ,kurudi nyumbani
wakute wamelala
Akilini mawazo ,kusherekea au kulipa ada za shule januari
wanaume wanatamani kubinafsisha familia zao ..
wamama wasio uvumilivu ,wenye maungo ya haja wanakimbia nyumba zao
Umasikini Mbaya

Pengine kariakoo ,iliyosheheni pilika za kununua na kuuza,
sio mfano wa kweli , naona naota ndoto ..
Napanda gari ,nipate fika upesi
kutembelea masaki wanakoishi wazungu japo weusi wa rangi
Naingia mgahawani ,japo nipate kahawa..
Muuzaji aniambia biashara mbaya ni sana
hata walio wakubwa wamekata miguu kufika

Hawa siwaelewi , naenda zangu Ubungo ,
Pia Nitapita Mbagala zilipo stand za mikoani
Hali mbaya haikomi ,magari yamenuna
Ule msimu wa madalali kuruka nazo bei ,bei za nauli
Mwaka huu umekoma ...

Napiga japo simu ,nipate tuma salamu
kijijini kuwapa habari ,mbaya zisizokifani
kuwa nami nimekosa nauli ya mjomba kufika
Babu naye bibi ..,wanieleza masikitiko
Mabonde yote yetu ,yaletayo mazao .
Mwaka huu mbaya , bibi naye aliza
Kilimo kimekataa ,Tujiandae kwa njaaa


Tuma japo senti chache ,dada yangu asisitiza
Maisha ni magumu ,kesho ni majaliwa
Kweli haijapata tokea ,msimu ule mbaya
wa sikukuu kama huuu , hatujui kosa letu
Maulana Twakuomba , roho zetu ziokoe
Tuokoe na mikosi , mbali upate itupa...,
Kosa letu ,hatujui ,Yote haya kustahiki !!!

Tafakari yangu ,kuu
kimya hiki kutawala ,kila mmoja yu kimya
anayeongea ni nani ,mtabiri na mtafiti
wote wale wapo kimya
Wasijue la kufanya , kimya hiki kimezidi
wamuachia afanye ,lake yeye atakalo
ende akalitimize ,

Akikamatwa mmoja ,sisi wote tuwe kimya
akakamtwa wa pili , kuendelea na wa kenda
Tisa kumi wakamatwa ,wote kimya imekuwa
Anafukiwa wa mwisho , japo sio mtoni ..
wa kumtetea yupi ,jasiri aliyebaki
kimya hiki ,homa yetu
Tiba yake ,imekoma
 
Yule wa Kwa mtogole ,Kwa mfuga mbwa ,uwanja wa fisi
kule Mtowisa , kasulu ,
na katerero Ambaye hata mchango wa rambi rambi za tetemeko katoswa
HATA HAJUI MAANA YA NENO DEAL
Kwa mtogole,mfuga mbwa na uwanja wa fisi wao kila siku ni kama sikukuu
Kazi kwako wewe PM,unataka uweke mezani whisky za 50,000,uchinje mbuzi wanne kama si kiti moto
 
Mliozoea hela za dili lazima mlie
Kumbe Tanzania ni maskini kwasababu inafanya deal sasa itatajirika baada ya kuacha mambo ya deal....Siku hizi ata magari hayasimami kwa Magufuri ili watu wanywe chai ...Hotel inakaribia kufungwa
 
Kwa mtogole,mfuga mbwa na uwanja wa fisi wao kila siku ni kama sikukuu
Kazi kwako wewe PM,unataka uweke mezani whisky za 50,000,uchinje mbuzi wanne kama si kiti moto
Nikiwa rais mtalimia meno ! Wananchi wamekuwa maadui ?
 
Kwa mtogole,mfuga mbwa na uwanja wa fisi wao kila siku ni kama sikukuu
Kazi kwako wewe PM,unataka uweke mezani whisky za 50,000,uchinje mbuzi wanne kama si kiti moto

Heri yako wewe ..unajuwa walae wa KANYIGO Walioporwa PESA ZA RAMBI RAMBI , na wa mtogole kwa kila siku sikuu kuu........
mimi mfugaji shambani nina mbuzi,ngombe ,samaki kidogo nimeanza kwahiyo hata nikikosa pesa SINTAKOSA PESA YA GONGO.....gongo na nyama zinaenda tu hakuna shida ...asubuhi nitakunywa maziwa kukata sumu ya pombe ...
 
ndo mawazo hayo mimi leo nlkuwa kariakoo pilikapilika ni kubwa mno,,,,,,,lakini ndo hivyo hata nigeria walishangilia kufanya mabadiriko lakini sahivi wana hali ngumu kuliko kipindi cha JONATHAN..ndo maana me sitegemeagi selikali iniletee maisha mazuri ni mimi mwenyewe
 
Wenyewe watakwambia sasa ndio tunaishi maisha yetu halisi.
Of course maisha yetu halisi kwa kuangalia hali ya Baba yangu na Babu yangu ni ya dhiki na ufukara. Mimi nilijaribu kupambana kuondokana na ufukara lakini naona katika mwaka huu Mmoja nimepiga hatua saba nyuma. Mimi sikuwahi kuwa mpiga dili na sijui dili zinapigwaje wala msiniseme vibaya
 

Similar Discussions

12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom