Msimu mbaya wa sikukuu toka tupate uhuru

Of course maisha yetu halisi kwa kuangalia hali ya Baba yangu na Babu yangu ni ya dhiki na ufukara. Mimi nilijaribu kupambana kuondokana na ufukara lakini naona katika mwaka huu Mmoja nimepiga hatua saba nyuma. Mimi sikuwahi kuwa mpiga dili na sijui dili zinapigwaje wala msiniseme vibaya
Teh teh teh mimi nilizoea baba Gastón na Jim Reeves nyimbo zao zinatamba kuanzia tarehe moja desemba sasa ni giza tupu la baba jesca kilaza
 
TATIZO JEMBE
mkuu nimeshakusoma,kwa masivina nyuzini,
nchi sa yakojoa wima,kisa? yetu makosani,
jembe tuloweka hima,limekatika mpini,
sasa twachambishwa wima, hamnazo akilini,
eti namba!

Yamebaki labda kesho, shufwa kuwa si witiri,
Warwa kalewa uhondo,mzima huyu daktari?
Viatu vina uvundo,labda havimtoshani,
Eti zimo yuanazo? ama zmeruka hewani,
Eti mashetani?
ahaaaaa kabang....vina na mezani ,hapo pake zimefika...
 
Napita njiani ,
Natembea kwa miguu,kwa Mtogole
Kwa mfuga mbwa, na makoroboi
kote kunafanana
kimya kikuu kimetanda

Natembea hadi kariakoo,
ni msimu wa sherehe ,wafanyabiashara kufurahi
watoto kuruka ruka ,wakisubiri zawadi
wazazi wanajichelewesha ,kurudi nyumbani
wakute wamelala
Akilini mawazo ,kusherekea au kulipa ada za shule januari
wanaume wanatamani kubinafsisha familia zao ..
wamama wasio uvumilivu ,wenye maungo ya haja wanakimbia nyumba zao
Umasikini Mbaya

Pengine kariakoo ,iliyosheheni pilika za kununua na kuuza,
sio mfano wa kweli , naona naota ndoto ..
Napanda gari ,nipate fika upesi
kutembelea masaki wanakoishi wazungu japo weusi wa rangi
Naingia mgahawani ,japo nipate kahawa..
Muuzaji aniambia biashara mbaya ni sana
hata walio wakubwa wamekata miguu kufika

Hawa siwaelewi , naenda zangu Ubungo ,
Pia Nitapita Mbagala zilipo stand za mikoani
Hali mbaya haikomi ,magari yamenuna
Ule msimu wa madalali kuruka nazo bei ,bei za nauli
Mwaka huu umekoma ...

Napiga japo simu ,nipate tuma salamu
kijijini kuwapa habari ,mbaya zisizokifani
kuwa nami nimekosa nauli ya mjomba kufika
Babu naye bibi ..,wanieleza masikitiko
Mabonde yote yetu ,yaletayo mazao .
Mwaka huu mbaya , bibi naye aliza
Kilimo kimekataa ,Tujiandae kwa njaaa


Tuma japo senti chache ,dada yangu asisitiza
Maisha ni magumu ,kesho ni majaliwa
Kweli haijapata tokea ,msimu ule mbaya
wa sikukuu kama huuu , hatujui kosa letu
Maulana Twakuomba , roho zetu ziokoe
Tuokoe na mikosi , mbali upate itupa...,
Kosa letu ,hatujui ,Yote haya kustahiki !!!

Tafakari yangu ,kuu
kimya hiki kutawala ,kila mmoja yu kimya
anayeongea ni nani ,mtabiri na mtafiti
wote wale wapo kimya
Wasijue la kufanya , kimya hiki kimezidi
wamuachia afanye ,lake yeye atakalo
ende akalitimize ,

Akikamatwa mmoja ,sisi wote tuwe kimya
akakamtwa wa pili , kuendelea na wa kenda
Tisa kumi wakamatwa ,wote kimya imekuwa
Anafukiwa wa mwisho , japo sio mtoni ..
wa kumtetea yupi ,jasiri aliyebaki
kimya hiki ,homa yetu
Tiba yake ,imekoma
Bavicha katika ubora wenu...kipindi hiki lazima mtage, Sera Hakuna tena
 
Huo wimbo hata babu aliuimba,
Pesa hakuna uliimbwa tangu enzi za mababu!
Rejea: asiyefanya kazi na asile!

hizo kazi ziko wapi,hima mimi nikafanye ,
bora nyie mwaziona,mawani nipe nivae,
kutumbuliwa wa juu ,wa kwetu chini wakae,
vibarua viko wapi, mageti ya bosi tukae..
ukame umetapakaa,kagera nako mikoa
Njaa inapiga hodi ,mola hiki tuepushe
hizo kazi ziko wapi ,hima tupate kufanya
 
Bavicha katika ubora wenu...kipindi hiki lazima mtage, Sera Hakuna tena
sio kila mtu bavicha hapa , pengine wewe mwanangu au mama yako ananijua ...ukaulizee
ahaaa....sorry nafikiri nyie mnaishi dunia yenye mafuta na asali so hata matatizo ya msingi yasiohitaji akili za vyama inakuwa tabu
 
Haya haya tenaaa
Wapiga dili mtaficha wapi nyuso zenuuu msimu wa skukuu maana mko chweeee
Shenzy sanaaa, mkawa mnakula bata kama ni nchi yenu pekeenu huku sisi twashindia sembe kisamvu
Na badoo, suruali zitawatelemka tuu haiwezekani mimi nivae suruali size 30 halafu kuna nyang'au linavaa size 46 kudadadeki
ndio vijana wetu ..hawa unashinda kijiweni unataka ufanane na wachapa kazi ...kama watu wanafanya kazi wanapata uwe nao sawa kwakuwa umeambiwa hivyo
 
sio kila mtu bavicha hapa , pengine wewe mwanangu au mama yako ananijua ...ukaulizee
ahaaa....sorry nafikiri nyie mnaishi dunia yenye mafuta na asali so hata matatizo ya msingi yasiohitaji akili za vyama inakuwa tabu
Nani hakujui bavicha wewe? Mmeishiwa Sera mpaka mtataga tu
 
Hivi ule usemi wa "kulimia meno" nyie mlijua anawazungumzia waethipia au waganda!!?? Nabado.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom