Lasway.Jr
JF-Expert Member
- Jul 25, 2015
- 230
- 402
Uzi huu ni special kwa ajili ya kujadili mambo mbali mbali yanayohusu maadhimisho ya siku ya wakulima ali maarufu kama 88 , ambapo msimu huu huambatana na Maonyesho ya teknolojia za kilimo, mifugo, biashara n.k zinazolenga kuboresha zaidi sekta ya kilimo hapa nchini.
Maonyesho hawa kwa kawaida hufanyika kikanda ambapo mikoa teule huwa na uwanja spesho kwa ajili ya makampuni, mashirika, taasisi, watu binafsi kwenda na kuonyesha bidhaa na huduma zao ambapo mkulima na mfugaji ndio mlengwa kwenye maonyesho haya.
Katika tanzania maonyesho haya hufanyika katika mikoa ya Arusha, Morogoro, Mbeya, Mwanza, Tabora, Simiyu, asante Dodoma, Lindi, Unguja.
Kuna mazuri mengi kwenye viwanja hivi lakini ningependa tujikite zaidi kwenye teknolojia ambazo zinapigiwa debe na kuonyeshwa ili kusaidia wakulima pia nilitamani tujadili mapungufu ya maonyesho haya ili tuone namna ya kuyaboresha zaidi.
Mwaka huu tumeona mabadiliko makubwa hasa kwenye uzinduzi wa bima za Kilimo, ongezeko la makampuni ya nje na ndani yanayojihusisha na uuzaji wa zana za kilimo, mashine, mbegu, madawa, mbolea n.k.
Tumeona na tutazidi kuona viongozi mbali mbali wakitoa kauli na mapendekezo ya serikali kisera ili kusaidia wakulima
Tumeona mwamko wa wakulima kujitokeza kwa wingi na kutaka kujifunza zaid na mengine mengi ambayo wadau watachangia hapa
Pia mapungufu yameoneka hasa pale tunapoona makampuni mengi au wafanyabiashara wengi wasiojihusisha na kilimo na mifugo kuvamia maonyesho haya.
Ushiriki finyu wa makampuni kutoka nje ya nchi na hili nalisemea ninapolinganisha 88 ya hapa tanzania na maonyesho ya wakulima Mjini Nairobi ambapo kuna wingi wa kampuni za kigeni kuleta teknolojia mpya na kuziuza kwa wazawa.
Zaidi sana kampuni nyingi au waonyeshaji (exhibitors) wengi wamebobea kwenye uzalishaji zaidi. Hakuna exhibitors wengi kwenye upande wa masoko na uchakataji wa mazao ya wakulima kitu ambacho kinanipa wasiwasi sana na kuona ni muhimu zaidi kuliangalia suala hili na kulifanyia kazi.
Karibuni
Tujuze 88 mwaka huu ni nini kipya kizuri na changamoto ni zipi?