Msimu huu kwa Mpira huu 'mwingi' wa Yanga SC tutawasingizia Wananunua tu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,370
108,412
Najua huko ( huku ) Mitaani sasa Gumzo ni Yanga SC 'Kanunua' kwa KMC FC na kwamba Kipa Farouq Shikalo na Beki Vicent Dante Chikupe ndiyo 'wamechomesha' kwa Kuchukua 'Mlungula' Yanga SC kwakuwa walitoka huko.

Nadhani JamiiForums nzima hakuna asiyejua kuwa GENTAMYCINE Mimi ni Simba SC 'lia lia' na kama kuna Timu au Klabu siipendi duniani basi ni Yanga ( japo kwa Ulaya ni Manchester United nayo siipendi pia ) ila leo nataka kusema Ukweli bila kuwa Mnafiki na Mgumu wa Kukubali Uzuri wa Kikosi cha Yanga SC na Mikakati yao ya 'Kiufundi' Uwanjani.

Ufuatao ni Mtizamo wangu GENTAMYCINE wa Jicho la 'Kiufundi' la kwanini Yanga SC inafanya vyema katika NBC Tanzania Premier League na kama Timu zote Pinzani ( ikiwemo yangu ya Simba SC ) zisipojipanga 'Kimkakati' zitafungwa sana tu na kuendelea Kuimba Wimbo wetu wa Kipumbavu ( Kipopoma ) wenye 'Wivu' mwingi kuwa Yanga SC inabebwa au inahonga Timu ( Vilabu ) Pinzani......

1. Yanga SC wamesajili Kiushindani

2. Yanga SC ina Wachezaji wenye Tamaa ya Mafanikio

3. Yanga SC ina Kocha mwenye Kipaji cha Kuwasoma Wapinzani hasa Kiudhaifu wao

4. Yanga SC ina Wachezaji mahiri wa Kigeni wenye kujua Kumaliza Mechi

5. Yanga SC imefanikiwa zaidi Kuwajenga 'Kinguvu' Wachezaji wake na nampa mno Sifa Kocha wao mpya wa Viungo kwani Wachezaji wa Yanga SC wa sasa wana Nguvu na inawasaidia

6. Yanga SC wana Mshikamano mkubwa kuanzia ndani kwa Wachezaji wao husika na hata nje wa Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wao

7. Yanga SC ina Wachezaji wenye 'Confidence' ya hali ya Juu kitu ambacho 'Kiufundi' pia huwa kina Faida na kuwa 'Tishio' kwa Timu (Vilabu) Pinzani.

Wana Simba SC Wenzangu leo mnisamehe Mwenzenu GENTAMYCINE kwa huu Ukweli na Uwazi wangu bali na Sisi hatujachelewa ama Kuyaiga baadhi au hata yote haya ya 'Kiufundi' kutoka kwa Wapinzani wetu Yanga SC ili tuendelee kuwa Bora zaidi yao ila tukizembea 'Kimikakati' basi ni dhahiri Msimu huu huenda Yanga SC nao wakajiuliza na hata Kutuvua Ubingwa.

Najua fika kuwa Ligi Kuu ndiyo Kwanza bado Mbichi ila Wahenga zetu hawakukosea walipokuja na hii 'Misemo' isemayo 'Dalili ya Mvua ni Mawingu' na 'Biashara asubuhi Mahesabu jioni' hivyo Simba SC tusibweteke wala tusikariri au tusiishi Kimazoea kwani si kila mwaka Upepo utakuwa upande Wetu tu na tusisahau kuwa hata Bingwa wa Msimu huu hachukui zile Shilingi Milioni 70 au Shilingi Milioni 80 tulizozizoea bali sasa anachukua Shilingi Milioni 500 kutoka Azam.

Hongereni tu Watani zangu mpo vizuri.
 
Kuna Watu huwa mnanilazimisha niwe nawajibu hovyo ( vibaya ) hapa JamiiForums halafu mnanilaumu.
Haina haja ya kumtukana cha msingi kama muda wako wa kulala haujafika mjibu tu kwamba kulala ni miongoni mwa nguzo muhimu za afya muda ukifika nitalala ndugu yangu.
 
Hakuna cha kuiga kutoka utopoloni. Simba inaiga mazuri kutoka kwa akina Mazembe, Mamelod , Raja casablanca n.k. Ni bahati tu imewaangukia hizo mechi tatu ila hamna timu hapo.
Hapana msimu kidogo wana afadhali tofauti na misimu minne hii iliyopita. We Mayele unamchukuliaje kwa mfano?
 
Hivi we jamaa hawa yanga unataka kuwa kopa ama nini, mbona unawapa ujiko hivi?
Mimi siyo Mwana Simba SC tu pekee kama ulivyo bali ni Mwana Simba SC lakini pia ni Mwanamichezo na Mdau mkubwa wa Mpira halafu sina Utamaduni wa Unafiki, Ushamba na Upumbavu kama mlionao wengi Wenu.

ANGALIZO / ONYO

Tafadhali kama unajijua Wewe ni Mwana Simba SC ambaye hupendi Kusikia Yanga SC ikisifiwa Kimpira ( Kimchezo ) na Mimi GENTAMYCINE nakuomba uwe unaacha ama Kufungua au hata Kusoma tu Threads na Posts zangu hapa JamiiForums.

Sijajiunga JamiiForums ili niwe tu nawafurahisha Wana Simba SC au wana CCM Wenzangu bali GENTAMYCINE nipo hapa kama Mtu Huru na mwenye Mtazamo na Mawazo yangu ambayo hayafungamani na upande Wowote ule. Yanga SC na CHADEMA ( Wapinzani ) wakipatia sitoacha Kuwasifia na acheni kutaka Kunipangia cha Kuandika hapa kwani Uhalali huo hamna na Wala hamtoupata.

Nimemaliza.
 
Back
Top Bottom