Msimlaumu Sana Magufuli - Ubepari Ni Unyama Msisahau

Hahaa mkuu ubepari kama wa bukuku pale sangu na malekela au marehemu yuda
 
WATANZANIA TUNA AKILI DHAIFU SANA.

Ubepari unasababisha waafrika na waarabu ku-risk kufia kwenye boti ili kufika kwa wanaoishi kibepari.

Ubepari unaweza kutoa mazingira bora ya ajira. Mpaka tunaona watu wanafurika wakitaka kuhamia kwenye angalau ajira za kubeba maboksi kuliko huko choka mbaya wanaojitapa na ujamaa.

Ubepari unakupa mazingira bora ya kupata elimu nzuri ambayo mnaitamani.

Ujamaa ni mfumo unaokupa uhakika wa kufa maskini.

Mnajitapa mmataka ujamaa huku mnapora michango ya pensheni za wastaafu. Mabepari mnaowabeza wanakupa huduma za afya na malipo hata kama hukuchangia.

Bahati mbaya wanaoushabikia ujamaa wapo bize wanafurahia matunda ya ubepari.

Ujamaa ni mfumo wa watu wanaoamini katika kuzuia maendeleo ya wachache wakidhani wengi watayapata.

Ujamaa = "MTU MMOJA ANA KISIMA CHA MAJI. SERIKALI INAAMUA KUFUKIA KILE KISIMA HUKU IKIAHIDI KUJENGA VISIMA BILA KUVIJENGA."

Ubepari = ""MTU MMOJA ANA KISIMA CHA MAJI. SERIKALI INAMPA HAKI YA KUSAMBAZA MAJI NA MBINU ZA KUPATA MAJI KWA WATU WENGINE KWA FAIDA".

Bado watanzania hatujamaliza kutubu dhambi za ujamaa na wengine bado wanaendelea kuota njozi za ujamaa.

Utamkuta rais anawalaghai anaowaongoza kuwa ubepari ni unyama. Cha ajabu yeye anapata huduma FIRST CLASS za afya, usafiri, chakula nk. kutoka kwa anaowaita mabeberu huku wananchi wake wanakosa vitabu vya kusomea, walimu wenye weledi, panadol hospitali nk...

TUACHE UNAFIKI NA PROPAGANDA. TUAMBIZANE UKWELI NA TUUISHI UKWELI
 
Wewe mwenyewe upo kwa mabepari alafu unakuja kubwabwaja porojo zako.

Si ndio maana yangu; ninaishi kwa mabepari naujua ubepari uchungu na utamu wake... Watanzania nao watoke kwenye ualinacha.. ubepari ndio mfumo wetu kwa sasa (hata kama hatuupendi vipi) na unakuja na matokeo yake. Hivi ushasikia ripoti zinazotolewa Marekani juu ya hali ya ajira? utashangaa.. umeona soko lao la hisa linavyopanda na kushuka na wakati mwingine unaweza ukafikiria ndio mwisho wa dunia.. kwa taarifa yako:

Mwaka huu peke yake hadi leo hii makampuni makubwa 18 yametangaza kufilisika! Miongoni mwao ni Toys R Us na Brookstone! na kubwa zaidi kati yao Sears!
Hadi hivi sasa mabenki yapatayo 89 yamefungwa Marekani au kuchukuliwa usimamizi wao na Benki Kuu
Kuna maelfu ya watu Marekani wanafukuzwa kazi kila siku na wengine hawajapata kazi kwa miezi sasa (bado wanasaka)..

Hii ndio asili ya ubepari...
 
Mzee mwenzangu,mie nilijiweka kando,niliona kama huyu mtu haeleweki wala hatendei haki wanaomtendea.Kosa kubwa ni Mbowe kumleta Lowassa na kumuengua Daktari.

Naamini kabisa,kabisa kabisa,huu upande unajiegemeza sababu tu ya makosa ya kimkakati ya upinzani 2015,lakini kiukweli huu si upande wako.

Hoja za bandiko lako naziheshimu kutokana na upande ulipo sasa.
 
TUACHE UNAFIKI NA PROPAGANDA. TUAMBIZANE UKWELI NA TUUISHI UKWELI

Umesema mambo muhimu sana na ya kufikirisha... lakini huko huko kwenye ubepari usisahu wapo wengi wanaotaka kuurekebisha kwa kuingiza mambo ya kijamaa.. as a matter of fact utaona ujamaa unatumika katika nchi za kibepari kuukoa ubepari kwa sababu nguvu za ubepari kwa asili yake ni destructive!
 
Mzee mwenzangu,mie nilijiweka kando,niliona kama huyu mtu haeleweki wala hatendei haki wanaomtendea.Kosa kubwa ni Mbowe kumleta Lowassa na kumuengua Daktari.

Naamini kabisa,kabisa kabisa,huu upande unajiegemeza sababu tu ya makosa ya kimkakati ya upinzani 2015,lakini kiukweli huu si upande wako.

Hoja za bandiko lako naziheshimu kutokana na upande ulipo sasa.

Uko karibu sana na ukweli; na ukiangalia ni kana kwamba hakuna cha kujifunza tayari wameanza kuzungumza vile vile tena kuelekea 2020..
 
Siasa ina vinyonga kupita vinyonga wenyewe, watu wanabadilika kwa ustadi kiasi ambacho hata kinyonga original akasome.

Mtu anaandika pumba, ambayo hata kuielezea yeye mwenyewe hawezi ila anatulazimisha tuielewe.
 
Naamini hili ni kosa kubwa; Magufuli anachofanya ni kuulazimisha uchumi umtumikie Mtanzania.. ni kama mtu anaamua kusukuma gari lililokwama kwenye matope.. wakati mwingine anatumia nguvu kubwa sana ya misuli hadi pale litakapokwamuka ndio ashughulikie injini.. na matatizo ya gari lile..
Maandiko yako siku hizi hayasomeki.

Yaani yanakeraaa.

Too low.
 
Back
Top Bottom