Msimlaumu Magufuli kwa ujumla Watanzania siyo watu wakutafuta maendeleo

WILE

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
4,071
2,000
Hizi ni sababu zilizonifanya niandike hii mada

1) Tunapenda kulalamika kuliko kutatua matatizo.
2) Kila kitu tunategemea serikali itufanyie
3) Kwenye kila jambo tunatanguliza matumbo yetu badala ya Taifa
4)Tunapenda ngono na starehe kuliko kazi
5)Tunakimbia changamoto
6)Uvivu uliopindukia na kupitiliza kiwango cha uvivu wa binadamu wa zama hizi
7) Kupenda vya bure.. hapa naongelea misaada ya wahisani
8) Kufanya kazi bila matokeo kuonekana..
9) Kuendekeza wizi,ufisadi na udokozi kwenye sehemu za kazi.

Binafsi nadhani hatutaweza kubadilika lakini tuna jukumu kubwa la kuhakikisha kizazi kijacho kiwe na tabia na sifa tofauti na hizi.
 
DON

JF-Expert Member
May 6, 2008
861
500

Hayo yote ni kweli tubadilike tutafute maendeleo si kwa kulalamika na tuukubali ukweli. Kazi haitaki siasa
 
Wong Fei

JF-Expert Member
Apr 13, 2016
3,931
2,000
AWAMU HII WATAKA VYEO NI WENGI SANA. Wao kusifia ndiyo wameona dili. Komaa huenda ukaitwa sbb nafas ni nyingi sana awamu. Unaweza kuziba gap la wanaotumbiliwa.
UNGEKUWA UMEKOSA MKOPO WA CHUO USINGEANDIKA UTUMBO HUO. NGOJA TUONE SBB AWAMU HII WENGI WAMEJITOA UFAHAMU.
HONGERA YAKO, NI MAWAZO YAKO.
#CHOMAKADISSM#
 
Drifter

JF-Expert Member
Jan 4, 2010
2,298
2,000
Hizi ni sababu zilizonifanya niandike hii mada

1) Tunapenda kulalamika kuliko kutatua matatizo.
2) Kila kitu tunategemea serikali itufanyie
3) Kwenye kila jambo tunatanguliza matumbo yetu badala ya Taifa
4)Tunapenda ngono na starehe kuliko kazi
5)Tunakimbia changamoto
6)Uvivu uliopindukia na kupitiliza kiwango cha uvivu wa binadamu wa zama hizi
7) Kupenda vya bure.. hapa naongelea misaada ya wahisani
8) Kufanya kazi bila matokeo kuonekana..
9) Kuendekeza wizi,ufisadi na udokozi kwenye sehemu za kazi.

Binafsi nadhani hatutaweza kubadilika lakini tuna jukumu kubwa la kuhakikisha kizazi kijacho kiwe na tabia na sifa tofauti na hizi.
Mleta mada jitahidi kuelewa serikali ni nini; si mtu binafsi kama kaka au dada yako. Hao ndio huwezi kushinda unawalaumu kwa mkwamo wako. Serikali ndiyo huweka mazingira ya kukuwezesha au kukukwamisha kujiletea maendeleo. Serikali ndio huweka au kudhibiti mazingira ya ufisadi. Inatumia kodi na rasilimali zetu kufanyia hayo.

Unawajua Wachina walivyo hatari. Jiulize kwa nini kwao ufisadi umedhibitiwa hasa na wanachapa kazi si mchezo. Utapeli wanafanya zaidi nje ya nchi au kwa wageni. Usiandike habari za serikali na wananchi kama vile unaelezea familia yenu.
 
Ndahani

JF-Expert Member
Jun 3, 2008
16,807
2,000
Wale wanaojituma na kuwa wabunifu, tofauti itaonekana tu. Wale wanaotegemea kula kwenye siasa na biashara za ujanja ujanja kazi ipo
 
Manchris Jbisd

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
693
500
Tafuta maana ya serikali. Tafuta kwa nini kuna serikali. Tafuta kwa nini serikali zilianzishwa. Tafuta serikali ni ya nani. Mwisho tafuta maana ya kodi na kwa nini kodi inakusanywa.

Tafuta kimaana halisi. Sio kisiasa.
 
kukudume2013

JF-Expert Member
Jan 8, 2013
1,484
1,500
Mkuu umesema kweli kweli japo sio woote lkn ni wengi ktk jamii, naongezea kidogo kucheza pull mchana kweupe,kupiga madeal ,soga vijiweni,starehe nyingi ,kufuatilia mambo ya watu na kusemana,na kupenda Subeti bila kujua ndo tunaumizwa kwenye betting,nk
 
kijana wa leo

JF-Expert Member
Nov 28, 2011
2,801
2,000
Hayo yote uliyoyaandika ungeeanza kujiuliza ni kwanini? katika kila ulichokiandika anza na neno kwanini, ukipata jibu nadhani utaufuta huu uzi wako.
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
13,354
2,000
- Siku Hizi Kila Mtu Mwanaharakati Wa Kisiasa, Mchambuzi Wa Mambo Ya Siasa

- Mambo Mengi Na Fursa Za Kiuchumi Tumeachia Wahindi, Hata Viwanda Tunawategemea Wao Ndo Wajenge

- Wabongo Kila Mtu Mpiga Domo Na Porojo Kibao, Anachoweza Ni Unafiki Tu Na Matusi Mitandaoni

- Unakuta Kijana Katumikaaa Kwenye Maandamano Ya Siasa Mpaka Anafikia Miaka 35 Hana Taaluma Wala Ujuzi Wowote Hivyo Hata Wahindi Wakijenga Viwanda Kazi Tutakazopata Ni Ulinzi, Kazi Nzuri Zitachukuliwa Na Wakenya Na Wahindi - Tutaanza Tena Kupiga Domo Na Kulaumu Serikali, Ndio Zetu

- Mtu Mweusi Akili Ndogooo
 
Smart911

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
41,918
2,000
1) Tunapenda kulalamika kuliko kutatua matatizo.
Jibu: Kwa sababu ya mifumo mibaya na utendaji mbovu, msema kweli huonekana mlalamishi siku zote...

2) Kila kitu tunategemea serikali itufanyie
Jibu: Siyo kweli, vingi ukitaka kufanya au kuanzisha mwenyewe unakumbana na vikwazo vingi sana...

3) Kwenye kila jambo tunatanguliza matumbo yetu badala ya Taifa
Jibu: Waliyokuwepo kwenye system, mambo ya kitu kidogo...

4)Tunapenda ngono na starehe kuliko kazi
Jibu: Siyo kweli, mengi ni matamshi tu wachache sana wenyewe huo muda... ndiyo maana unaambiwa za kuambiwa changanya na za kwako...

5)Tunakimbia changamoto
Jibu: Fursa ni za midomoni tu lakini nyingi ni hewa...

6)Uvivu uliopindukia na kupitiliza kiwango cha uvivu wa binadamu wa zama hizi
Jibu: Endapo jitihada zako zinakwamishwa na wachache kwa mlolongo wa kitu kinachoitwa process, ukisubiria unaitwa mvivu huchangamki... Wanaoonekana shapu ni wale watoa rushwa ili mambo yao yaende haraka haraka...

7) Kupenda vya bure.. hapa naongelea misaada ya wahisani
Jibu: Hakuna cha bure, misaada inatolewa kwa sababu... ni vile tu hawaweki wazi kila kitu...

8) Kufanya kazi bila matokeo kuonekana..
Jibu: Ukweli hausemwi...

9) Kuendekeza wizi,ufisadi na udokozi kwenye sehemu za kazi.
Jibu: Hii ni tabia ya kutokuwa na uzalendo.. bali kuwa na umimi... Ili ufisadi upungue au kuisha kabisa inabidi mashuleni toka awali watu wafundishwe uzaelendo na kuthamini rasilimali tulizonazo kwa manufaa ya vizazi na vizazi... Kama kila mtu anawaza kuwa tajiri haya mambo hayawezi kuisha...
Mtu anaimbiwa soma uje upate kazi nzuri uje kuwa na maisha mazuri kama wakina fulani... kweli mtu anajitahidi anapata kazi lakini hayo maisha mazuri hayaoni.. mwisho wa siku anakuwa mdokozi au fisadi au mwizi, ili awe na hayo maisha mazuri...
 
ISIS

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
91,509
2,000
Hizi ni sababu zilizonifanya niandike hii mada

1) Tunapenda kulalamika kuliko kutatua matatizo.
2) Kila kitu tunategemea serikali itufanyie
3) Kwenye kila jambo tunatanguliza matumbo yetu badala ya Taifa
4)Tunapenda ngono na starehe kuliko kazi
5)Tunakimbia changamoto
6)Uvivu uliopindukia na kupitiliza kiwango cha uvivu wa binadamu wa zama hizi
7) Kupenda vya bure.. hapa naongelea misaada ya wahisani
8) Kufanya kazi bila matokeo kuonekana..
9) Kuendekeza wizi,ufisadi na udokozi kwenye sehemu za kazi.

Binafsi nadhani hatutaweza kubadilika lakini tuna jukumu kubwa la kuhakikisha kizazi kijacho kiwe na tabia na sifa tofauti na hizi.
Msema ukweli ni mpenzi wa Mungu. ..kwa kweli message received. ..na tunaanza leo kubadilika. ..stay well
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
13,354
2,000
Mkuu umesema kweli kweli japo sio woote lkn ni wengi ktk jamii, naongezea kidogo kucheza pull mchana kweupe,kupiga madeal ,soga vijiweni,starehe nyingi ,kufuatilia mambo ya watu na kusemana,na kupenda Subeti bila kujua ndo tunaumizwa kwenye betting,nk
Kila Kitu Tunategemea Wahindi Mpaka Kampuni Za Kubet
 
kabila01

JF-Expert Member
Apr 21, 2009
3,914
2,000
Wiki iliyopita nilikua na shughuli ya kupanda shamba langu nikaenda kwenye kijiwe cha vijana wasio na kazi ambacho kipo jirani na kilabu cha pombe za kienyeji ili kuwatafuta vijana wakanisaidie kazi ya kuchimba mashimo. Kila kijana niliyekua naongea nae alipiga chenga aliona ni bora aendelee kukaa pale kijiweni asubiri pombe za kugongea. Shamba lenyewe ni ekari 1 na nilitaka vijana wanne ambapo ningewalipa sh elf 5 kwa kila mmoja na ile kazi haizidi masaa mawili. Yaani nilihangaika sana mpaka nikaenda kuwatafuta vijana wengine kijijini
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom