Elections 2010 Msimchagulie Zitto Jimbo; hamna hadhi hiyo!

Hili ndilo tatizo letu watanzania, tunataka watu wote wawe na mawazo sawa. Simply kwa kuwa mtu anapingana na vitu fulani na Zitto aimanishi ya kuwa ni chiki binafsi, bali kuna sababu za msingi anapingana naye.

Sasa unaona posti zinazomlaumu na kumlaani Zitto bila kutoa supportive arguments, ndio maana nasema hizi ni chuki tu. Tufike mahali tuache tukubali vipaji vya watu badala ya kumchukia mtu just for the sake ya kumchukia tu!
 
Sasa unaona posti zinazomlaumu na kumlaani Zitto bila kutoa supportive arguments, ndio maana nasema hizi ni chuki tu. Tufike mahali tuache tukubali vipaji vya watu badala ya kumchukia mtu just for the sake ya kumchukia tu!
Mbona hujaomgelea zinazomsifia? Huyu si ndio juzi juzi akichangia kuhusu Commom Market Protocol kasema Wabongo tuna wasiwasi uzio na msingi? Si huyu alisema tununue Dowans kisha akabadilika akasema tutaifishe? Kwa nini unataka tuendelee kumwamini?
 
Uadilifu shurti uwe mpaka kwenye personal life. Tusimsifu tu Zitto bila kuangalia ana mapungufu gani katika maisha ya kawaida nje ya siasa. Bado siamini kwamba Zitto anaweza kuwa mwanasiasa mahiri aliye na msimamo wa kukdumu.
 
Ni kweli Mwanakijiji lakini kule kwetu Tanganyika tunamuhitaji pia. Hao CCM watafurahi sana ikiwa Zitto atagombea Jimbo lingine nje ya Kigoma Kaskazini, ninafurahi kuwa NEC haijaliunganisha Jombo la Kigoma Kaskazini na Kigoma Mjini maana mpango ulikuwa ndo huo sijui wameshituka kitu gani hadi wameamua kuliacha Jimbo la Zitto huru.


Wanahisi kuwa majimbo yanayoongozwa na wapinzani hawawezi kudanganyika tena hivyo Zitto kugombea jimbo jengine kutakuwa na maana ya kuengeza majimbo yasiyodanganyika!
 
Ni kweli Zito ana haki ya kugombea popote nchini lakini lazima naye pia awe na msimamo na ajue kwamba yeye kama kiongozi ni mfano kwa watu wengi, Tatizo langu na Zito ni kutokuwa na msimamo thabiti;
1. kuna wakati alwahi kusema hatagombea tena ubunge tena mwaka huu na angependa kufanya shughuli zakimataifa zaidi na kuendeleza profesional yake, lakini sasa anakuja na kusema atagombea lakini anafanya utafiti agombee jimbo gani.
2. kitendo cha kutangaza anafanya utafiti wa kuua agombee wapi ni usaliti kwa wananchi wajimbo analowakilisha...lazima ajue wao ndio walimuamini na kumpa nafasi ya kuingia bungeni na kupata fursa ya kujulikana, hawa ndio watu wa kuthaminikwake, na kuwasaidia wa gharama yoyotte, lazima Zito ajue kwamba chochote anachopata akiw kama mbunge ni kwa ajii ya wananchi wa Jimbo lake, leo hii anaonyesha dharau za waziwazi kabisa kwa kusema anaweza kugombea sehmu nyingine, hii ni kukosa fadhira kwa watu wake.....

ni bora usigombee kuliko ukagombee sehemu nyingine....tumia busara na kuwa na fadhira kwa waliokufadhiri....wasikilize wazee....maneno ya wazee dawa....
 
zitto inabidi kuchukua hatua za tahadhari kabla kufanya uamuzi wa jimbo gani agombee ubunge. sidhani kuwa kuna maendeleo ambayo zitto kama mbunge anaweza kuyaleta katika jimbo! sijui, labda kuna mtu ana statistics za jimbo ambalo analiwakilisha zitto ambazo zinatoa picha - kabla na baada! naona kuna dhana tete na yenye mashaka kuhusu kugombea katika hayo majimbo mengine. Sidhani na kama kweli zitto anaungwa mkono na majimbo mengine na hata kuweza kupita kwa ushindi. kama kweli anakubalika kwanini basi asimuuze mgombea wa chadema katika majimbo hayo kama alivyoahidi kufanya kwa yule mheshimiwa aliyetoka chadema kwenda nccr? kama kweli ana nia ya kuwakilisha jimbo kwa dhati tu basi arudi home! Ukisoma alama za nyakati, utaona hii si strategy nzuri kwa zitto na chama...
 
"Ameanza Spika na sasa kaja Mwanasheria Mkuu" -wangempa ushauri agombee kwenye majimbo yao! if they like him
 
Kwa kweli inashangaza kuona CCM wanamchagulia jimbo inawahusu nini? au wanaogopa? Zitto namshauri agombee anapoona ataleta mabadiliko....hasa Geita panamfaa kwa sababu dhahabu inaibiwa sana.
 
mimi kunakitu nafikiria kwa mapana yake kuwa, Wanaogopa Zito kugombea kule kwenye migodi maana waheshimiwa wana percent zao , sasa wanaona ikiwa nguvu ya CHADEMA itakua kubwa ipo hofu yakutokea yale ya TARIME ya Chacha Wangwe , ambapo badala ya pesa kwenda kwa waheshimiwa angalau imeanza kutumika palepale halmashauri kusomeshea watoto na kuboresha mazingira ya afya.
 
zito mjanja.anawapoteza tu maboya maadau zake na kuwachanganya.ila mwenyewe anajua atagombea wapi.


Kama ni hivyo tutamuelewa kijana ....
Jinsi navyotamani CCM iondoke madarakani eeeh mungu baba saidia
 
No one really cares agombee atakapo jiskia this is non-issue zitto atakapo gombea it makes little difference to be honest.
 
Zitto akiamua kugombea Jimbo la Geita hawa CCM watakesha kwa kuimba maana watakuwa na uhakika wa kulipata jimbo hilo kwa asilimia zote,tuelewe kuwa mazingira ya kushinda kwa Nyerere na akina Mrema majimbo mbali miaka na kwao ni tofauti kabisa na mazingira yake yanayomsukuma kutoka kwenye jimbo lake la Kigoma kwenda Geita!

Pili asidanganywe na mkutano wake aliofanyia uwanja wa Magereza-Geita mjini uliojaa watu wengi kuwa ndiyo kigezo cha yeye kukubalika wilayani Geita,as usual wapiga kura wengi wa tz wapo vijijini na huko ndipo Mabina Ernest atakapotwaa kura nyingi,kwa ufupi mtandao wa CCM kule Geita una outweigh mtandao wa CHADEMA!

Zitto na nina uhakika wa asilimia zote atarudi jimbo lake la Kigoma ambako huko CHADEMA wana mtandao mpana unao mpa nafasi ya yeye kurudi tena Bungeni;aking'ang'ania hilo jimbo la Geita officially wana mageuzi tutakwa tumekwisha mpoteza Zitto kama mbunge wa upinzani!
 
Mimi nilitegemea Zitto kwa nafasi yake na kwa umaarufu ataanza kuangalia mbali zaidi, je yeye kama kijana anaanzisha ama anahamasishaje vuguvugu la vijana kujikomboa na kusimama kutetea maslahi ya taifa hili changa. Nilitegemea angekuwa mtu wa makongamano, semina na mikutano ya kuhimizana na vijana walio vyuoni na wengine walio katika ajira. Hii ni kwa sababu ya umakini aliouonyesha na mara nyingi amekuwa ana vyanzo vya kuaminika vya taarifa mbalimbali.
Kwa namna hii ndipo atakuwa anatoa mchango wa kudumu na wakuaminika kwa jamii ya nchi hii. Ila akijisahau na kuanza kuwaza masuala ya majimbo na wapi pa kugombea kwa vile anakubalika anakuwa na yeye ameanza kuwaza kama walivyo wanasiasa uchwara tuliowazoea.
Ajiulize, kugombea kwake jimbo tofauti na Kigoma kaskazini, kutainufaisha nini jamii ama kuna faida gani kwa harakati za kusafisha uchafu katika taifa hili? Labda kama anajua akiachia jimbo hilo litachukuliwa na mwanaharakati mwingine wa kuaminiwa na yeye kwa umaarufu na kukubalika kwake akachukue na kupokonya jingine toka kwa mbunge uchwara anayedhani ubunge ni kwa ajili ya tumbo lake, familia yake na walevi wenzake, haya yote yakiwa na manufaa ya kupanua wigo wa mapambano na harakati.
Zitto akifa leo hatutaki tubakiwe na historia tu ya alichowahi kukisema tunatakiwa tubakiwe na ushahidi wa alichowahi kukifanya, na mfano mzuri ni vuguvugu la wanaharakati ambalo, kwa mtazamo wangu, anatakiwa atumie uamaarufu wake katika kulikuza na kulistawisha.
 
Dogo ana elements za wao m' (sisi j") anatupiga changa la macho .....kwani masumbuko lamwai yuko wapi sasa...si alikua kama yeye mbwembwe nyingi ..mwisho wasiku akaonyeshwa fuko la hela kimyaaaaa kapotea karudi wao m',...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom