Msimbazi Polisi

Keykey

JF-Expert Member
Dec 1, 2006
3,250
740
03_10_w2cuzg.jpg

Maji taka na uchafu ulio ndani ya ukuta wa majengo ya kituo cha Polisi cha Msimbazi unatishia afya za wakazi wa eneo hilo kama ulivyonaswa na kamera ya mpiga picha wetu Kariakoo jijini Dar es Salaam jana. Hatua za dharura zinapaswa kuchukuliwa kuepusha magonjwa ya kuhara na kipindupindu.
(Picha kwa hisani ya HabariLeo)

Kumbuka hapa vilevile wanaishi familia za askari, inashangaza pale wasimamizi wa sheria wanaposhindwa kuonyesha mfano kwa manufaa yao wenyewe.

Labda MGAMBO wa jiji watumwe hapa kuwawajibisha maafande?
 
MLiona akina Masanja nao walitoa hiyo issue ya usafi wa hapo Polis Msmbazi, kweli inasikitisha
 
Sasa wanaojenga majengo na kukarabati Majengo ya Serikali ni wakina nani? Sio Wizara ya Ujenzi??? Polisi walinde raia na mali zao kisha wakarabati jengo sasa hii uonevu kwa polisi
 
Kama wameiona hii wanapaswa kujirekebisha haraka vinginevyo wachukuliwe hatua na maafisa wa afya wa mkoa haraka sana.
 
Aibu kwa maafande wetu!Wahusika fanyeni usafi. Maafande siku hizi mimi nawapenda sana jinsi wanavyoichapa kazi...tofauti na enzi za mzee wa kununa....Mahita.
 
The question is..(Tujibu kutoka kwa mioyo yetu bila kumung'unya maneno).

Kipya ni kipi hapa??

Mlitegemea kitu tafauti?? Kwa input ipi mliyoweka?? Au mnadhania maendeleo yanaendeshwa ktk mfumo wa perpetual machine??
 
03_10_w2cuzg.jpg

Maji taka na uchafu ulio ndani ya ukuta wa majengo ya kituo cha Polisi cha Msimbazi unatishia afya za wakazi wa eneo hilo kama ulivyonaswa na kamera ya mpiga picha wetu Kariakoo jijini Dar es Salaam jana. Hatua za dharura zinapaswa kuchukuliwa kuepusha magonjwa ya kuhara na kipindupindu.
(Picha kwa hisani ya HabariLeo)

Kumbuka hapa vilevile wanaishi familia za askari, inashangaza pale wasimamizi wa sheria wanaposhindwa kuonyesha mfano kwa manufaa yao wenyewe.

Labda MGAMBO wa jiji watumwe hapa kuwawajibisha maafande?

Mkuu umenifurahisha, mgambo wako kwa ajili ya kukimbizana na machinga maana kunalipa!!Halafu ujue hapo ni choo cha haja ndogo!!! Nisameheni ila ukweli ndiyo huo!!!! Wanakojoa ndani ya chupa za maji ya uhai, na mhusika anajifanya anamwaga maji kumbe ni mkojo!! Na hii inafanyika sehemu nyingi sana hasa maeneo ya foleni hao wauza maji au vitu vya mkononi wanajibanza na gari anakojolea ndani ya chupa faster na kumwaga, huku haogopi nata abiria au wenye magari!!!! Tanzania kuna makubwa (reforms) yanatakiwa, tena kwa nguvu kubwa sii lelemama.
 
Kipindupindu kukitokomeza Dar kwa staili hii ya uchafu ni ndoto za abunwasi. Hii Picha inatoa taswira ya jiji la Dar lilivyo chafu kupindukia na kwamba si mahali salama pa kuishi.
 
Back
Top Bottom