Maji taka na uchafu ulio ndani ya ukuta wa majengo ya kituo cha Polisi cha Msimbazi unatishia afya za wakazi wa eneo hilo kama ulivyonaswa na kamera ya mpiga picha wetu Kariakoo jijini Dar es Salaam jana. Hatua za dharura zinapaswa kuchukuliwa kuepusha magonjwa ya kuhara na kipindupindu.
(Picha kwa hisani ya HabariLeo)
Kumbuka hapa vilevile wanaishi familia za askari, inashangaza pale wasimamizi wa sheria wanaposhindwa kuonyesha mfano kwa manufaa yao wenyewe.
Labda MGAMBO wa jiji watumwe hapa kuwawajibisha maafande?