Msimamo wangu: Sirudishi biashara zangu Tanzania

Ndugu zangu mimi ni miongoni mwa watanzania wengi tulioumizwa katika awamu ya tano.

Biashara zangu ziliminywa mwanza, arusha, na Dar es salaam.

Maofisa wa TRA na TAKUKURU walinyanganya leseni ya biashara yangu na vile vile serikali wakarevoke account yangu kabla ya kuchukua pesa takribani milioni 600.

Nilitishwa sana na TRA na TAKUKURU, nilisingiziwa kuwa silipi kodi mbali na kuwa nilikuwa mlipaji mzuri wa kodi na pia niliwapa documents za miaka yote ya ulipaji kodi tangu mwaka 2001 nilipoanza biashara zangu za Kubadilisha fedha maarufu kama Bureau De change..

Serikali hii naomba iwalipe fidia wote waliodhulumiwa kwa sababu hata rais Huyu tunayemshangilia alikuwa sehemu ya tatizo hilo ambalo leo tunasahaulishwa kwa nyimbo za kusifu na haleluya za twitter.

Kumuombea mtu mabaya sipendagi lakini inafikia hatua tunaombeana mabaya ili tu angalau nafsi zitulizane kwa sababu ya dhulma tulizofanyiwa na wenye mamlaka.
Serikali hii naomba iwalipe fidia wote waliodhulumiwa kwa sababu hata rais Huyu tunayemshangilia alikuwa sehemu ya tatizo hilo ambalo leo tunasahaulishwa kwa nyimbo za kusifu na haleluya za twitter.
 
Ku"revoke" account maana yake nini? Ilifungwa na pesa yako ikaishia au vipi. Wewe mfanya biashara wa pesa hata uchaguzi wa maneno ya kibiashara hujui. Wanaweza ku"reoke" leseni siyo account. Account hufungwa. Hata hivyo, Bureau de Change mlikuwa majizi wakubwa tu. Siyo kila anayedai aliminywa kikodi ni kweli aliminywa. Wengi mlikuwa mna under declare mapato. Na wengine mlijiingiza kwenye biashara ya kimataifa ya kutakatisha pesa. Lakini sasa kila mtu anamlaumi jiwe. Ninyi ndiyo mlikuwa mnashirikiana na wauza madawakatika utakatishaji pesa, tena hata exchange rates zenu kwa wauza madawa zilikuwa za kuwapa faida nyinyi. Hii ilijulikana kwa hata watu wa kawaida, hata zile guidelines za kuuza na kununa pesa mlikuwa hamfuati.

Mlikuwa na wizi mwingine wa kubadilisha noti ndogo. Eti noti ya dola mia ilikuwa na thamani kubwa kuliko ya 50, 20, 10, na 5. Kama huo si wizi ilikuwa nini. Sasa unafuta huruma huku umewaibia watanzania maelfu kwa njia hii. Wauza madawa mlikuwa mnawauzia $ kwa kiwango cha juu. Kama thamani halisi ya $ ilikuwa shilling 2000 ninyi mlikuwa mnaweka 2.500 mpaka 3,000. Ninyi ndiyo mlikuwa mnafanyas biashara ya madawa inashamiri TZ maana hela ya hao wauzaji ilikuwa inatunziwa kwenu kwa commission.
you have limited exposure, you better shut up
 
Mama Samia akiingia mtego wa wafanya biashara kukushinikiza ufanye wanavyotaka umekwisha.
Subiri waanze kuumana
Target ni T2,unadhani zitatoka wapi?
Huyu Samia namuona atakua mkali kuliko Magufuli,mpaka December,watu wataanza kufikiria Rais mwingine Kama kawaida yetu wabongo
 
Jamaangu walipofunga account yake na kuchukua hela wala hakufanya kitu chochote zaidi zaidi alipata usingizi katikati ya bara bara karibu saa nzima huku jasho linamtoka Kama maji wasamalia wema walipomstua alitoa gari pembeni ilikua Fortuner baadae anapigiwa simu alipoti kituo chochote cha karibu alichokifanya alipeleka ile Fortuner nyumbani alitoka na kichwa cha Scania mpaka Lusaka, Zambia ndio akapanda ndege mpaka SA huko nyuma walizoa magari yote nyumbani aliposikia mporaji kaenda nimesikia karudi kitachimbika huko balaa...watu waliumizwa sana tena wale walipa Kodi hata kukwepa hawajui kisa walikua na pesa ndefu bank...
 
Wewe hujui chochote kuhusi biashara, uchumi na uwekezaji. Mawazo yako kuhusu uchumi, yameishia kwenye kuta za chumba chako.

Unachotakiwa kufahamu, ni kuwa hakuna nchi maskini hata moja Duniani iliyowahi kuendela ama kwa kuongeza ukubwa wa kodi au uwingi wa kodi.

Nchi ikiwa masikini inatakiwa kushusha sana viwango vya kodi ili kuvutia uwekezaji. Viongozi wetu wajifunze toka Dubai na Ghana. Wajinga wanadhani kuwa kodi ikiwa kubwa sana ndiyo kupata makusanyo makubwa!!
Ghana wana akili sana na ni wasomi kweli Mkuu
 
Ku"revoke" account maana yake nini? Ilifungwa na pesa yako ikaishia au vipi. Wewe mfanya biashara wa pesa hata uchaguzi wa maneno ya kibiashara hujui. Wanaweza ku"reoke" leseni siyo account. Account hufungwa. Hata hivyo, Bureau de Change mlikuwa majizi wakubwa tu. Siyo kila anayedai aliminywa kikodi ni kweli aliminywa. Wengi mlikuwa mna under declare mapato. Na wengine mlijiingiza kwenye biashara ya kimataifa ya kutakatisha pesa. Lakini sasa kila mtu anamlaumi jiwe. Ninyi ndiyo mlikuwa mnashirikiana na wauza madawakatika utakatishaji pesa, tena hata exchange rates zenu kwa wauza madawa zilikuwa za kuwapa faida nyinyi. Hii ilijulikana kwa hata watu wa kawaida, hata zile guidelines za kuuza na kununa pesa mlikuwa hamfuati.

Mlikuwa na wizi mwingine wa kubadilisha noti ndogo. Eti noti ya dola mia ilikuwa na thamani kubwa kuliko ya 50, 20, 10, na 5. Kama huo si wizi ilikuwa nini. Sasa unafuta huruma huku umewaibia watanzania maelfu kwa njia hii. Wauza madawa mlikuwa mnawauzia $ kwa kiwango cha juu. Kama thamani halisi ya $ ilikuwa shilling 2000 ninyi mlikuwa mnaweka 2.500 mpaka 3,000. Ninyi ndiyo mlikuwa mnafanyas biashara ya madawa inashamiri TZ maana hela ya hao wauzaji ilikuwa inatunziwa kwenu kwa commission.
Daah kazi kweli kweli kwa hiyo unataka upate Elimu kwa nini dola ishirini rate exchange ipo tofauti na dola mia katika Nchi nyingi Mkuu ni bora ukae kimya kama kitu hukijui usilete chuki za hovyo kisa umeona milioni 600 watoto wadogo tuu wanashika hiyo hela tena ya harali kuliko unavyoaminishwa...
 
Kilichosaidia ni kwamba kuna milioni 900 nilikuwa nimeweka katika benk kuu ya Ethipia ndiyo hawakuweza kuichukua.

Sasa hivi nipo najiiimarisha nchini Ethiopia.
Ethiopia unajiimarisha kwa biashara hiyohiyo ya Bureau de change au?
 
Alikuwepo lakini alikuwa hana mamlaka kwa yule bwana mwendazake nifikiri hili liko wazi wala halihitaji elimu ya PHD
Twitter imeteka akili za wengi sana, ni wachache sana wanaopita kule wanabaki na akili zao, hongera.

Kuhusu kurudisha biashara au vipi endelea kusoma upepo kwanza, maana kama ulivyosema hata huyu aliyepo nae alikuwepo wakati ule, japo yeye anaonekana tofauti ameshatoa agizo kwa TRA tusubiri utekelezaji.
 
TRA na TAKUKURU wanaweza kweli kua na shida lakini pia watu wa kubadilisha pesa mlikua na shida nyingi na kubwa.

TRA imara haiwezi kupendwa na wafanya biashara. Huo ndio ukweli.

Kipindi kile cha kikwete watu wanakwepa kodi hawalipi mbona hatukusikia TRA ikilalamikiwa kua haikusanyi kodi, ni dhaifu? Mbona hatukusikia?

Mama Samia akiingia mtego wa wafanya biashara kukushinikiza ufanye wanavyotaka umekwisha.
Sjui ni kwa nini Watawala huchagua kwa biidii zote eneo hilo la kuwalaumu Wanainchi wao kwa makosa yao wenyewe.

Kama Watu hawapendi kulipa kdi mliwahi kujiuliza ni kwa nini?....au mnakusanya tu Polisi na bunduki kwenda kuwapora?.

Wakati mnaomba madaraka si huwa mnatuaminisha kwamba mtayamudu majukumu yenu?, ajabu ni mkishapata mnatugeuka na kutumia mabavu kutatua kero za Wanainchi wenu.

Hata kama mnaona Mtu anakwepa kodi kwa hiyo ufumbuzi wenu ni kumuondoa asiendelee na biashara...hivi hicho ndio haswa matokeo ya Elimu mlizozisotea mpaka kuitwa Daktari?.

Mimi nilidhani Elimu ingetumika kutengeneza Walipa kodi wengi badala na kubaki kuwazungukia tu Watu wachache mpaka mnawaangamiza kabisa?.
 
Ndugu zangu mimi ni miongoni mwa watanzania wengi tulioumizwa katika awamu ya tano.

Biashara zangu ziliminywa mwanza, arusha, na Dar es salaam.

Maofisa wa TRA na TAKUKURU walinyanganya leseni ya biashara yangu na vile vile serikali wakarevoke account yangu kabla ya kuchukua pesa takribani milioni 600.

Nilitishwa sana na TRA na TAKUKURU, nilisingiziwa kuwa silipi kodi mbali na kuwa nilikuwa mlipaji mzuri wa kodi na pia niliwapa documents za miaka yote ya ulipaji kodi tangu mwaka 2001 nilipoanza biashara zangu za Kubadilisha fedha maarufu kama Bureau De change..

Serikali hii naomba iwalipe fidia wote waliodhulumiwa kwa sababu hata rais Huyu tunayemshangilia alikuwa sehemu ya tatizo hilo ambalo leo tunasahaulishwa kwa nyimbo za kusifu na haleluya za twitter.

Kumuombea mtu mabaya sipendagi lakini inafikia hatua tunaombeana mabaya ili tu angalau nafsi zitulizane kwa sababu ya dhulma tulizofanyiwa na wenye mamlaka.
Sometimes hua nahisi watanzania ni kizazi cha Yuda.
Hua wanafanya kumpenda mtu ikiwa hawampendi, huo ni unafiki.
Amekufa Magu nyomi ya watu ikasema ilimpenda, tumejisahau kama tupo kwenye maombolezo mumeanza kumkashifu.
Watanzania mbarikiwa
 
Namuangalia mama SAMIA kwa huruma na huu mtego wa wafanya biashara, akiucheza vibaya tu kaliwa kwenye kodi.... Kiuhalisia hapakua na mtu alieonewa na milango ya kisheria ilikua wazi sema hapakua na modality nzuri ya ukusanyaji ( ambapo pia bila.kuwabana wasingelipa)

Kwa utafiti wangu mdogo kama wafanyabiashara wanalipa kodi TZ ni 3% tu. Nenda karikakooo kaa mule miezi sita kwa lengo la kujifunza pale maduka yale ni machache kuliko maduka halisi yaliyo vyumbani mwa watu mule.
 
Unamtisha Nani? Baki na biashara zako huko nje huko huko! Tangu uhamishe biashara zako ulisikia tunalala njaa?
 
Namuangalia mama SAMIA kwa huruma na huu mtego wa wafanya biashara, akiucheza vibaya tu kaliwa kwenye kodi.... Kiuhalisia hapakua na mtu alieonewa na milango ya kisheria ilikua wazi sema hapakua na modality nzuri ya ukusanyaji ( ambapo pia bila.kuwabana wasingelipa)

Kwa utafiti wangu mdogo kama wafanyabiashara wanalipa kodi TZ ni 3% tu. Nenda karikakooo kaa mule miezi sita kwa lengo la kujifunza pale maduka yale ni machache kuliko maduka halisi yaliyo vyumbani mwa watu mule.
Ni kweli, wafanyabiashara walizoea kutokulipa Kodi! Wengi Ni kama mafisi!! Mama akiwapa mpenyo kidogo tu tutaumia!!
 
sijui maza house atafreeze vitu vyangu na mm!? maana ananidai "kodi" pia hua namkwepa!
 
A
Jameni,
Kweli hali ilikuwa mbaya kiasi hiki?

Bahati mbaya sana hatupati taarifa za upande wa pili, nako tukajisomea na kuangalia hali halisi..

Inaeleweka, duniani kote, wafanya biashara, au hata mtu wa kawaida tu, ulipaji kodi hakuna hata mmoja anayeushabikia. Lakini inapofikia kiasi hiki, na ukatili/uoneaji juu yake, inashawishi sana kuamini kwamba pamekuwa na ukandamizaji wa wafanya biashara kusikokuwa kwa kawaida.

Kuhusu kutorudisha biashara Tanzania, hizo ni porojo tu. Kama wewe ni mfanyabiashara kweli, na biashara zako unazifanya kwa taratibu na sheria zilizopo, utarudi tu, hali ikiwa nzuri.
Soko lote hili la Tanzania wewe usilikubali, wewe kweli ni mfanya biashara?
Ameumizwa ww hujaumizwa huna machungu!
 
Back
Top Bottom