Ndugu zangu mimi ni miongoni mwa watanzania wengi tulioumizwa katika awamu ya tano.
Biashara zangu ziliminywa mwanza, arusha, na Dar es salaam.
Maofisa wa TRA na TAKUKURU walinyanganya leseni ya biashara yangu na vile vile serikali wakarevoke account yangu kabla ya kuchukua pesa takribani milioni 600.
Nilitishwa sana na TRA na TAKUKURU, nilisingiziwa kuwa silipi kodi mbali na kuwa nilikuwa mlipaji mzuri wa kodi na pia niliwapa documents za miaka yote ya ulipaji kodi tangu mwaka 2001 nilipoanza biashara zangu za Kubadilisha fedha maarufu kama Bureau De change..
Serikali hii naomba iwalipe fidia wote waliodhulumiwa kwa sababu hata rais Huyu tunayemshangilia alikuwa sehemu ya tatizo hilo ambalo leo tunasahaulishwa kwa nyimbo za kusifu na haleluya za twitter.
Kumuombea mtu mabaya sipendagi lakini inafikia hatua tunaombeana mabaya ili tu angalau nafsi zitulizane kwa sababu ya dhulma tulizofanyiwa na wenye mamlaka.