Msimamo wa UPDP juu ya utendaji wa Rais Magufuli

dizzle1

Member
Jan 16, 2011
85
9
MSIMAMO WA UPDP JUU YA UTENDAJI WA RAIS MAGUFULI

Awali ya yote ningependa kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dr John Pombe Magufuli kwa ujasiri alio uonyesha wa kupambana na ufisadi uliokuwa umekisiri katika taifa letu.

Watanzania kwa ujumla wetu tuna paswa kumuunga mkono kwa kile anachofanya toka ameingia madarakani,kwa mujibu wa report ya jana alipo kutana na wenyeviti na makatibu wa chama ikulu amebainisha mpaka kufikia leo kuna zaidi ya watumishi hewa 7700 katika taasisi za umma.Hii ni idadi kubwa sana ya watu waliokuwa wanapata pato la kila mwezi bila michango yao katika nchi.

Vile vile ningependa kuchukua fursa hii kumpongeza waziri wa ardhi kwa jinsi anavyo simamia ugawanyaji wa ardhi kwa wananchi walio porwa ardhi hiyo kwa kushirikiana na viongozi wa umma wasio kuwa waaminifu.

Tumeona Waziri wa ardhi Mh William Lukuvi akirejesha ardhi hiyo kwa wananchi waliochukuliwa ardhi hiyo kwa mgongo wa uwekezaji,sisi kama UPDP tuna muunga mkono sana kwani moja ya sera yetu kubwa ni kuhakikisha ardhi yetu inakuwa Chini ya wananchi ambao ndio waza na wenye uhalali wa kutwaa ardhi hiyo.

Mbali na pongezi hizo sisi kama chama kinacho amini katika,utu usawa,uwajibikaji,umoja na mshikamano miongoni mwa watanzania bila kujali itikadi zetu za kisiasa,kidini ,ukabila na uchumi tumesikitishwa sana na kauli za baadhi ya wanasiasa za kubeza na kuponda juhudi na ujasiri wa Rais wetu juu ya mapambano ya ufisadi na uwajibikaji.

Rais wetu amekuwa akichukizwa na jinsi taifa letu lilivyokuwa likinyonywa na mfumo wa ufisadi bila kupepesa macho,juzi tumeshuhudiwa Rais akimsimamisha kazi alie kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Ndugu Kabwe kutokana na kashfa ya ufisadi wa stand ya ubungo na ukiukwaji wa utoaji wa tender unao onyesha dhairi ulikuwa na harufu ya rushwa.

Baadhi ya wanasiasa wamekuja juu na kumponda Mh Rais katika mapambano haya na kutumia sababu mfu kabisa kuwa Nanukuu kauli yw alie wai kuwa Naibu katibu mkuu CUF Ndugu Julius Mtatiro kuwa Rais anadhalilisha viongozi na utu wa binadamu.Chama cha UPDP kimesikitishwa na kauli hizi za baadhi ya wanasiasa kuwa nyuma ya mafisadi na kutaka kufifisha juhudi na mapamabano ya Rais katika vita hii kali aliyodhamilia kupambana nayo.

Natoa raia kwa umma watanzania kuwapuuza wanasiasa wa upinzani walio kuwa wananufaika na baadhi ya viongozi wa serikali wanao tumbulkiwa kwa sasa,wao ndio wamekuwa watetezi wakubwa wa masuala ya ufisadi tofauti na kauli zao wanazo ubiri kwa wananchi.

Imetolewa na
Naibu katibu Mkuu Taifa
Felix Makuwa
 
Safi sana UPDP. Penye ukweli, ukweli usemwe na siyo porojo kama vyama vingine na wanaojifanya haki za binadamu.
 
Bado ccm sijawasikia wakitoa pongezi, labda kwa kuwa ndiyo waathirika wakuu wa utumbuaji wa majipu
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


HONGERA RAIS MAGUFULI KWA MSIMAMO WAKO JUU YA MSAADA WA MCC

Ndugu wana habari,Awali ya yote ningependa kuwashukuru kwa muitikio wenu wa kuja kusikiliza msimamo wa chama chetu kuhusu kile kinacho itwa msaada wa MCC.
Mmekuwa mkifanya hivyo kwa muda wote pale mnapo pata taarifa tunacho taka kuhubarisha umma juu ya kile chama chetu kinacho simamia.Ahsante sana kwa ushirikiano wenu na imani yenu kwetu.

Baada ya maelezo hayo mafupi,Mimi Mwenyekiti wa united peoples democratic party ningependa nijikite zaidi katika kile tulicho waitia ,ndugu wanahabari wote mna kumbukumbu wa kile alicho ongea Baba wa upinzani africa ya mashariki Marehemu Mzee Jaramong Odinga alipata kuandika andiko muda mfupi baada ya nchi yake kupata uhuru na baadhi ya nchi nyingine Afrika kuanza kupata uhuru mwanzoni mwa miaka ya 1960 Nanukuu kauli yake ”NOT YET UHURU ” mzee Jaramong alikuwa akiamini uhuru wa nchi za kiafrika bado.

Wachambuzi na wasomi wengi wa nchj za kiafrika waliwai toa matamko mbalimbali juu ya uhuru wa nchi za kiafrika kuwa uhuru tulio pata baadhi ya nchi za Afrika una toa fursa kwa aina nyingine ya ukoloni,wakimaanisha ukoloni mamboleo. Aina hii ya ukoloni umejengwa zaidi katika mfumo wa kututawala tena kwa njia ya akili na fikra na sio ule wa kimabavu ulio kuwepo awali.

Katika mfumo huu wakoloni wamefanikiwa kutujenga katika imani ya kuamini sisi watu weusi hatuwezi kujisimamia sisi wenyewe kwa 100% zaidi ya kutegemea misaada na mikopo toka nchi za ulaya na Marekani.

Kitendo cha Board ya Bunge la Marekani inayojulikana kama MCC kuitisha Tanzania kusitisha misaada waliyo wai kutoa awali katika shughuli za ujenzi wa miundombinu yetu kama barabara na umeme kwa sababu nyepesi tu na isiyo na mashiko kuhusiana na uchaguzi wa Zanzibar,ni dhairi walikuwa wana jaribu kupima kama sisi watu weusi bado tupo kwenye zile fikra zao za kuamini bila wao taifa letu haliwezi kujisimamia.

Ningependa kumpongeza Rais wetu Dr John Pombe Magufuli na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dr Shein kwa kupuuza misaada hiyo iliyokuwa ikiligharimu taifa letu kwa kiasi kikubwa sana na kufifisha juu na mapambano ya watanzania katika kutaka kuiona nchi yetu ina weza kujiongoza yenyewe katika nyanja za kiuchumi.

Wazee wetu walipambana sana katika kudai uhuru wa taifa letu wakiamini nchi yetu ina utajiri mkubwa sana na ikiwa nje ya ukoloni itapiga hatu kubwa sana katika nyanja za kiuchumi,kijamii na kisiasa.Baadhi ya wapigania uhuru wa bara la Afrika laiti kama wangefufuka leo na kukuta bado taifa letu ni tegemezi toka nchi za ughaibuni wangeweza kupatwa na mshtuko mkubwa sana.

Ifahamike kuwa moja ya shabaha kubwa ya nchi za ughaibuni kuleta kile kinachoitwa msaada ni kutaka kutengeneza fursa za uwekezaji kwenye mataifa ya Afrika ili waendelee kuitumia Afrika kama soko la bidhaa zao na sehemu za kudhalisha ajira kwa wananchi wao,walio katika lindi kubwa la ukosefu wa ajira.

Ndugu wanahabari nyie ni mashaidi kuhusu soko la ajira Duniani,ukienda katika nchi za ulaya tatizo la ajira limekubwa kubwa sana ukilinganisha na hapa kwetu ambapo fursa za ajira bado zipo nyingi sana kama serikali itakuwa serious katika kuziibua fursa hizo tofauti na nchi za ulaya ambazo sector karibu zote za uchumi zimeshikwa na mabepari.

Ndugu wanahabari tuna penda mfahamu kuwa tuna unga mkono juhudi kubwa zinazo fanywa na Rais wetu Dr John Pombe Magufuli na Rais wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Dr Ali Mohammed Shein za kutaka kulifanya taifa letu litokee katika mfumo huu wa ukoloni mamboleo na kuwa taifa la uchumi wakati.

Msamamo wa chama chetu UPDP( United People's Democratic Party) ni kutaka nchi iondokane na misaada inayotolewa na mataifa yenye lengo la kufifisha shughuli zetu za kiuchumi na kudumaza mapambano ya fikra chanya ya kuwa taifa lenye uchumi unao jitegemea.

Imetolewa na
Mwenyekiti wa UPDP taifa
Mheshimiwa Farmi Dovutwa
 
Unampongeza kwa hilo huku hao hao Wamarekani wameruhusiwa kufadhiri kwa kutoa fedha nyingi sana kwenye mradi wa SAUTI ambao eti unaeleimisha juu ya masuala ya UKIMWI huku wakisambaza VIRAINISHI vya kusaidia MASHOGA wasichubuke na kuambukizwa UKIMWI je kwa nini na hili asilikatae?
 
Wabongo kwa kupindisha maneno. Hiv tanzania ndiyo imekataa misaada au imenyimwa? Na kama imekataa si irudishe ile instalment iliyokuwa imeisha pokea. Kibya zaidi wanajifanya iti wamekataa misaada hamji hta na solution . Yani hata aliyepost hii hakumbuki kuwa linchi lenyewe linadeni kubwa kiasikuwa hata lenyewe linadaiwa zaidi ya lakitisa kutoka kwenye deni la taifa. Sasa likiambiwa lijilipie sijui linaweza? Swala la nchi kujitegemea ni lamuhimu sana lakiti sio swala la kufumba na kufumbua et nchi inajitegemea. Leo ukisema Tz ijitigemee ni sawa na kuachisha maziwa mtoto wa mwezi 1. Kama mmenyiwa kaeni kimya acheni kumbela njoeni na solution.
ICHI IMEJAA MAKAMPUNI YA KIMATAIFA CHUNGU NZIME YENYE MIKATABA MIKUBWA MIKUBWA ALAFU MNASEMA KUJITEGEMEA!
 
Chama ambacho hakina hata Mwenyekiti mmoja wa mtaa nchi nzima kuendelea kuita chama kwa vile kiliandikishwa kwa msajili ni matusi.
Afadhali hata kuheshimu tamko la kikundi cha vikoba cha mtaani kuliko vyama kama hivi maana waweza kuta kikundi cha vikoba kina wanachama hai wengi kuliko UPDP
 
Back
Top Bottom