Msimamo wa uamsho juu ya kuendelea kupinga muungano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msimamo wa uamsho juu ya kuendelea kupinga muungano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mangaline, Jun 2, 2012.

 1. Mangaline

  Mangaline JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 1,052
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kauli ya mkuu wa kikundi cha wana uamusho Zanzibari juu ya kile wanachodai kuendelea kupinga muungano kwa maombi mpaka kieleweke, si jambo la kupuuza. Msimamo alioutoa mkuu huyo, siku moja tu baada ya raisi wa zanzibar kutoa kauli na msimamo wa serikali ya zanzibari, na kulaani vikali vitendo hivyo, na bado mkuu huyo wa uamusho kujitokeza hadharani na kwa ujasiri na kutoa maelekezo na huku akisikilizwa na umati mkubwa wa wananchi wa zanzibari, vinaashiria uwepo wa nguvu na msukumo wa kipekee katika suala hili, ukiwa nyuma yake. siamini na wala haiingii akilini kuwa mtu huyu hana umma nyuma yake, ukiwemo msukumo wa viongozi na nguvu za dola na wana siasa wa zanzibari. hivi kwa nini mapema tu, serikali ya zanzibari ilikubali kufidia uharibifu uliofanyika, hata kabla ya kesi kufika mahakamani? kuna mengi ya kujiuliza kabla ya mkuu wa kaya kutoa uamuzi. HERI NUSU SHARI KULIKO SHARI KAMILI.

  MAONI YANGU.
  Namwomba mkuu wa kaya, afikiri mara mbili kila atakapo toa uamuzi, ili tatizo la muungano lisije likaleta matatizo ya kufikishana the heigi hapo 2016.
  MUNGU IBARIKI TANGANYIKA, MUNGU IBARIKI ZANZIBARI, RIP TANZANIA
   
 2. M

  Musia Member

  #2
  Jun 2, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 94
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  uko sawa kabisa, hawa wana nguvu kubwa nyuma yao. na wanaungwa mkono na serikali yao ndio maana hata baada ya kutangazwa kwamba hali imedhibitiwa bado kuna kanisa jingine lilichomwa moto.
  jiulize hiyo doria ilikuwa ya aina gani?
   
 3. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,583
  Likes Received: 1,675
  Trophy Points: 280
  Raisi legeleeg hawezi mahamuzi magumu!
   
Loading...