Msimamo wa Nyerere, Mareale UN ulikuwa mmoja

Ndakilawe

JF-Expert Member
Jul 6, 2011
4,815
2,813
​Hivi majuzi , mzee Kisumo alipokuwa anahojiwa na gazeti la mwananchi alisema kuwa Nyerere alipokwenda UN kati ya mwaka 1955, 1956 na 1957 alikutana na Cheaf Marealle akimpinga Tanganyika kupewa uhuru, au akitaka uhuru wa KILIMANJARO pekee(Chagga land)!

Kisumo ni mzandiki na alikuwa na chuki binafsi na ukoo wa Marealle, ndio maana amekuwa akitoa kauli hizo za kuuchafua ukoo wa Maraelle na kuharibu historia nzuri na chief huyo.

Na chakusangaza mpaka leo kwenye mashule, vyuoni watu wamekuwa wakifundishwa hivyo, kumbe ni juhudi binafsi za Marealle kumchafua Chief. Hata mimi nilikuwa nimeathirika na hiyo mitizamo hasi ya watu juu ya Paramount Chief Marealle.

UKWELI HUU HAPA; Kama ilivyosemwa na ndugu wa ukoo pia kwa mujibu wa maandiko mbalimbali katika historia, ambayo Kisumo nahakika hakuwa kuyasoma, hata wale Wahadhiri wangu UDSM cjui walikuwa wapi hawakuyapitia wakati wakinifundisha huu uongo wa Kisumo. Wanahistoria hao ambao ni AJ HUGHES katika kitabu ch East Africa, J CLAGGET TAYLOR ktk kitabu cha Political Development of Tanganyika na BERNARD CHIDREZO ktk kitabu cha Tanganyika and International Trusteeship, wote kwa upande mmoja wakisema kuwa Chifu na Nyerere waliafikiana juu ya lini Tanganyika ipewe uhuru wake, wakati Nyerere akisema muda wa kijiandaa kujitawala uwe "kati ya miaka 20-25 mwaka 1955, na mwaka 1956 iwe na kati ya miaka 10-12, Chifu Marealle alisema mwaka 1957 kuwa muda wa kujiandaa kujitawala iwe ni kati ya 10-15.

Katika hotuba ya mwaka June 18, 1957, Mwalimu Nyerere alisema hotuba ya Chifu UN ilikuwa ya maana kuliko ya kwake, " the statement of Chief Marealle II .....has been greater significance than mine"' na kwamba Chifu alikuwa anawakilisha Chifu wa Taifa na mwakilishi wa machifu wenzake.

Sasa huyo Peter Kisumo inayesemwa kuwa alikuwa karibu na Mwalimu kwann anataka kutudanganya, ni watanzania wangapi leo wanamaoni hasi juu wa huyu chifu, Je, serikali inachukuwa hatua gani kurekebisha hii historia ya Marealle ambaya inazidi kuharibiwa na Kisumo.
 
Mkuu mimi mwenyewe nilipigwa na butwaa baada ya kupewa kanda ya Chief Marealle akihutubia UN... Jamaa alikuwa Jembe kweli kweli, chakushangaza nasikia zile kanda zilipigwa marufuku na zilifichwa zaidi ya Bange! Kwa wale wanaokumbuka tukio la pale ARS ambapo JKN alikwepa kupita kwenye red capet na badala yake alimkimbilia na kumkumbatia Thomas Marealle watakuwa wanajua kilichotokea... Wonder why til to date Malkia anailipa familia ya Chief Marealle?...Mengi yanafunikwa lakini ukweli utasimama kuwa ukweli daima...a notion kuwa rais hatatoka kaskazini hawataki ku-acknowledge mchango wa watu wa kaskazini ulivyokuwa mkubwa ktk ukombozi wa bara hili; USA inatambua kuwa kaskazini mwa Tanzania kuna vichwa vya ukweli si madafu! Massawe wa NASA huwa analindwa akija bongo kuliko hata Obama!... Soon mtajua umuhimu wa mnowabagua kila kukicha ...
 
so watanzania wa kanda nyingine hakuna vichwa ni madafu tu? huo ni ubaguzi na dharau za kijinga sana,unaweza ukawa umeleta jambo zuri ambalo wengi tunaweza kufurahia kujua au kuelimika lakini mwishoni ukatibua na hivyo kuharibu hata maana ya yote uliyoandika.
 
Rejea kusoma post yangu Mkuu...hakuna mahala nimetoa tuhuma za kuwalaumu watu wa kanda nyingine na kuwafananisha na madafu kama unavyotaka kuwaaminisha wewe... instead nimekemea propaganda za kijinga za CCM zinazoendekeza ukabila na ukanda wakati kaskazini kuna watu wazuri tu wanaoweza kuisaidia nchi hii ikapiga maendeleo ya haraka...kwani wewe ni zao la walioshindwa kuuzwa hata kwa dinari moja enzi za biashara zile za kuuza watu? pole ndugu...
 
Ndugu yangu mbona unametawaliwa na Ukabila sana? Huyu Chief Mareale alikwenda UN kuwakilisha Watanzania na Siyo Wachaga. Ninaona umeanza kujisifia kwamba Kasikazini kuna watu wenye akili sana kwa hotuba ya Chief UN. Tukianza kuwa na Umimi Mkoa wa Mara watasemaje, Wakwele nao watasemaje, huko kwa Mkapa watasemaje? N.k. Kila kiongozi anayekwenda nje anawakilisha mawazo ya Watu wote anaowatawala na siyo kabila au dini anayotoka.
 
Acha Umimi. Hebu tuangalie hivyo vichwa vya Watanzania kwa njia ya umimi “ Basili Mramba, Grey Mgonja, Danniel Yona, David Mathayo, Edward Lowasa, Ritha Mlaki, Cleopa Msuya, Jumanne Maghembe, Fredrick Sumaye, Merry Nagu, Mbuge Lema, N.K. Sasa unda time ya Watanzania kwa kuangalia viongozi waadilifu kikanda. Hawa hapa ni viongozi wa Tanzania au walikuwa. Wetu sote na kama ni waovu walikuwa wakiwakilisha mawazo ya wananchi waliowachagua. Tafakari kisha chukua hatua. BADILiKA LEO.
 
Rejea kusoma post yangu Mkuu...hakuna mahala nimetoa tuhuma za kuwalaumu watu wa kanda nyingine na kuwafananisha na madafu kama unavyotaka kuwaaminisha wewe... instead nimekemea propaganda za kijinga za CCM zinazoendekeza ukabila na ukanda wakati kaskazini kuna watu wazuri tu wanaoweza kuisaidia nchi hii ikapiga maendeleo ya haraka...kwani wewe ni zao la walioshindwa kuuzwa hata kwa dinari moja enzi za biashara zile za kuuza watu? pole ndugu...

Ukanda gani ambao hauna watu wazuri wanaoweza kuisadia nchi ikapiga hatua ya maendeleo ya haraka?
 
Mwalimu Nyerere alisema hotuba ya Chifu UN ilikuwa ya maana kuliko ya kwake, " the statement of Chief Marealle II .....has been greater significance than mine"' na kwamba Chifu alikuwa anawakilisha Chifu wa Taifa na mwakilishi wa machifu wenzake.

Nenda katafute quote sahihi. Nyerere hawezi kusema sentensi kama hiyo.
 
Alichosema Kisumo ndicho sahihi!. Mjerumani alikuwa akitumia utawala wa direct rule, Muingereza ndio akaleta indirect rule ya devide and rule!. Wagawanye uwatawale kwa kuanzisha utawala wa uchifu!. Machifu walifanywa wajione wao ndio bora zaidi, na mkuu wa machifu wote Tanzania alikuwa ni Mangi Mkuu, Thomas Marealle!.

Ni ukweli usiopingika watu wa koo hizi za kichifu walipendelewa ikiwemo kupewa nyumba na Malkia kule London!. Hawa walikuwa ni vibaraka wa wazungu!, walinuona mkoloni ni bora zaidi kuliko mtu mweusi!. Mpaka leo, mpaka kesho makabila anajisikia fahari sana kuishi kuzungu, kuvaa kuzungu, kutembea kizungu, kuongea kuzungu na kutokana na kuupenda uzungu, baadhi ya wanawake wa wetu hupenda kujibadili ili wafanane na wazungu, kuvaa mawigi na nywele za bandia za kizungu, kubadili rangi kwa kujichubua wawe kama wazungu, kujikondesha kuwa na shape kama wazungu, masikini dada zetu hawajui, kuwa hata ladha hubadilika na kuwa ya kizungu!.

Mpaka leo mpaka kesho, nazijua baadhi ya familia zenye uwezo, wanawake wao wanakwenda kujifungulia London!.

Nimebahatika kusoma na one of them toka ukoo wa Mangi Mkuu, hawa jamaa ni mayai kweli kweli!. Tulipomaliza tuu form four, mwenzetu huyoo London!. Nilipopata fursa ya kuja Uingereza, nilimtembelea, life ilikuwa safi!, jamaa wana nyumba ya ukoo London ila yeye na mkewe walipanga nyumba nzima jirani!. Maisha ni ya kudeka deka tangu Tanzania hadi London!.

Tangu tulipoachana Bongo hadi tunakutana London ilipita yapata miaka 10!. Tulipafanya tathmini ya pamoja kati ya miaka 10 ya bongo, mimi nina nini, na miaka 10 ya London mwenzangu ana nini!, akatamani kurudi bongo na mimi nikamuunga mkono. Miaka miwili baadae alirudi na familia yake ila its very unfortunatelly maisha ya bongo yalimshinda!, family ilisambaratika for sometimes, ila kutokana na kuona familia bora, family ili take controll, familia ikatengamaa na jamaa akaona bora arudi kuishi London, huko amezoea zaidi na maisha anayaweza kuliko maisha ya huku!.

Back to Mangi Mkuu, aliside na wakoloni kuwa Watanganyika bado hatiko tayari kujitawala mpaka labda baada ya miaka 15-20!. Akapendekeza kwa vile Kilimajaro ilikuwa juu kimaendeleo, watoe uhuru kwa majimbo kwa Kilimanjaro kupewa uhuru wake kwanza, maeneo mengine yakishaendelea nayo ndio yapewa uhuru hadi Tanganyika yote iishe!.

Chief Marealle ali undermine juhudi zozote za Tanganyika kujiwala, Nyerere baada ya kulijua hili, ali team na wale Waswahili masikini wenzake na wale wazee wa Gerezani, tukapata uhuru!. From there alifutilia mbali uchifu, Mangi Mkuu Mareale akamind sana, akahamia London!. Nyerere aliwawasideline baadhi ya makabila kwenye urais!. Never will this country be ruled na rais kutoka baadhi ya makabila!. Laana ya Nyerere itatushukia!.

Poleni!
Merry X-mass
Pasco
 
​Hivi majuzi , mzee Kisumo alipokuwa anahojiwa na gazeti la mwananchi alisema kuwa Nyerere alipokwenda UN kati ya mwaka 1955, 1956 na 1957 alikutana na Cheaf Marealle akimpinga Tanganyika kupewa uhuru, au akitaka uhuru wa KILIMANJARO pekee(Chagga land)!

Kisumo ni mzandiki na alikuwa na chuki binafsi na ukoo wa Marealle, ndio maana amekuwa akitoa kauli hizo za kuuchafua ukoo wa Maraelle na kuharibu historia nzuri na chief huyo.

Na chakusangaza mpaka leo kwenye mashule, vyuoni watu wamekuwa wakifundishwa hivyo, kumbe ni juhudi binafsi za Marealle kumchafua Chief. Hata mimi nilikuwa nimeathirika na hiyo mitizamo hasi ya watu juu ya Paramount Chief Marealle.

UKWELI HUU HAPA; Kama ilivyosemwa na ndugu wa ukoo pia kwa mujibu wa maandiko mbalimbali katika historia, ambayo Kisumo nahakika hakuwa kuyasoma, hata wale Wahadhiri wangu UDSM cjui walikuwa wapi hawakuyapitia wakati wakinifundisha huu uongo wa Kisumo. Wanahistoria hao ambao ni AJ HUGHES katika kitabu ch East Africa, J CLAGGET TAYLOR ktk kitabu cha Political Development of Tanganyika na BERNARD CHIDREZO ktk kitabu cha Tanganyika and International Trusteeship, wote kwa upande mmoja wakisema kuwa Chifu na Nyerere waliafikiana juu ya lini Tanganyika ipewe uhuru wake, wakati Nyerere akisema muda wa kijiandaa kujitawala uwe "kati ya miaka 20-25 mwaka 1955, na mwaka 1956 iwe na kati ya miaka 10-12, Chifu Marealle alisema mwaka 1957 kuwa muda wa kujiandaa kujitawala iwe ni kati ya 10-15.

Katika hotuba ya mwaka June 18, 1957, Mwalimu Nyerere alisema hotuba ya Chifu UN ilikuwa ya maana kuliko ya kwake, " the statement of Chief Marealle II .....has been greater significance than mine"' na kwamba Chifu alikuwa anawakilisha Chifu wa Taifa na mwakilishi wa machifu wenzake.

Sasa huyo Peter Kisumo inayesemwa kuwa alikuwa karibu na Mwalimu kwann anataka kutudanganya, ni watanzania wangapi leo wanamaoni hasi juu wa huyu chifu, Je, serikali inachukuwa hatua gani kurekebisha hii historia ya Marealle ambaya inazidi kuharibiwa na Kisumo.

UCHAGGA umeanza je ni gongo tu au mbege? vp mmesha tambikia tayari? tumewamis baa hazina wateja......endeleen kujadili hayo...ila mkumbuke watanzania wa sasa wanawaangalia kwa jicho angavu.
 
Alichosema Kisumo ndicho sahihi!. Mjerumani alikuwa akitumia utawala wa direct rule, Muingereza ndio akaleta indirect rule ya devide and rule!. Wagawanye uwatawale kwa kuanzisha utawala wa uchifu!. Machifu walifanywa wajione wao ndio bora zaidi, na mkuu wa machifu wote Tanzania ndio Mangi Mkuu, Thomas Marealle!.

Ni ukweli usiopingika watu wa koo hizi za kichifu walipendelewa ikiwemo kupewa nyumba na Malkia kule London!. Hawa walikuwa ni vibaraka wa wazungu!, walinuona mkoloni ni bora zaidi kuliko mtu mweusi!. Mpaka leo, mpaka kesho Mchagga anajisikia fahari sana kuishi kuzungu, kuvaa kuzungu, kutembea kizungu, kuongea kuzungu na kutokana na kuupenda uzungu, baadhi ya wanawake wa kichagga Mungu amewapa shape za kuzungu (pasi)!.

Mpaka leo mpaka kesho, zile familia zenye uwezo za kichagga, wanakwenda kujifungulia London!.

Nimebahatika kusoma na one of the Marealles toka ukoo wa Mangi Mkuu, hawa jamaa ni mayai kweli kweli!. Tulipomaliza tuu form four, mwenzetu huyoo London!. Nilipopata fursa ya kuja Uingereza, nilimtembelea, life ilikuwa safi!, jamaa wana nyumba ya ukoo London ila yeye na mkewe walipanga nyumba nzima jirani!. Maisha ni ya kudeka deka tangu Tanzania hadi London!.

Tangu tulipoachana Bongo hadi tunakutana London ilipita yapata miaka 10!. Tulipafanya tathmini ya pamoja kati ya miaka 10 ya bongo, mimi nina nini, na miaka 10 ya London mwenzangu ana nini!, akatamani kurudi bongo na mimi nikamuunga mkono. Miaka miwili baadae alirudi na familia yake ila its very unfortunatelly maisha ya bongo yalimshinda!, family ilisambaratika for sometimes, ila kutokana na kuona familia bora, family ili take controll, familia ikatengamaa na jamaa akaona bora arudi kuishi London, huko amezoea zaidi na maisha anayaweza kuliko maisha ya huku!.

Back to Mangi Mkuu, aliside na wakoloni kuwa Watanganyika bado hatiko tayari kujitawala mpaka labda baada ya miaka 15-20!. Akapendekeza kwa vile Kilimajaro ilikuwa juu kimaendeleo, watoe uhuru kwa majimbo kwa Kilimanjaro kupewa uhuru wake kwanza, maeneo mengine yakishaendelea nayo ndio yapewa uhuru hadi Tanganyika yote iishe!.

Chief Marealle ali undermine juhudi zozote za Tanganyika kujiwala, Nyerere baada ya kulijua hili, ali team na wale Waswahili masikini wenzake na wale wazee wa Gerezani, tukapata uhuru!. From there alifutilia mbali uchifu, Mareale akamind sana!. Akawasideline Wachagga kwenye urais!. Never will this country be ruled na rais Mchagga!. Laana ya Nyerere itatushukia!.

Poleni!
Merry X-mass
Pasco

duh!mkuu,mbona kama una chuki na wachaga?
 
Hivi mzee Kisumo ni nani tena
Mzee Peter Kisumo, ni mmoja wa Wazee wa Baraza la Udhamini la Chama cha Mapinduzi!. Hawa ndio waliokisajili chama cha Mapinduzi na kikishitakiwa mahakamani, hawa ndio husimama kwa niaba ya chama!.

Katika ile kadhia ya Kesi ya Mauaji Mwanza ya mwaka 1976, Kisumo ndio alikuwa mkuu wa mkoa wa mwanza, akamwaga unga kwenye kadhia hiyo iliyomhusisha pia Waziri wa Mambo ya ndani, Mwinyi, waziri wa Usalama, mkuu wa polisi, mkuu wa usalama walitimuliwa kazi, RPC, OCD, RSO na DSO wa Mwanza, walishitakiwa, na kuhukumiwa ambapo ni RSO wa Mwanza pekee aliyeachiliwa na kukutwa hana hatia!.

Anachosema ni kweli kabisa!, Mangi Mkuu alimhujumu Nyerere ili tusiupate uhuru mapema na ndio maana kuna baadhi ya makabila, wataishia kuusikia!, japo mimi siungi mkono ubaguzi wa aina hii!.

Kuna baadhi ya makabila, hujikomba komba kwa wazungu!. Baadhi ya makabila mpaka kesho wanatamani wangezaliwa ulaya. Mimi mwenyewe nimeoa kabila fulani, tulipokuja UK wife akang'ang'ania UK eti hataki tena turudi bongo, na ikibidi kubeba box, tubebe!. Nililazimisha tukarudi kwa lazima kwa vile watoto walikuwa bado wadogo. Baadae tukaenda US, mke akagomea huko jumla!.
Pasco.
 
Huyu sio yule Pasco ninayemfahamu. Huyu ni Mkabila! Anayetetea habari za makabila! Anasema nchi haitakaa kamwe itawaliwe na mchaga hata kama anazo sifa sahihi! Nimemsamehe bure kwa sababu mwishoni amewsema kuwa ana grievances za kindoa na mkewe mchaga! Pole ndugu yangu. Angalia zisikupeleke mbali hadi kujisahau kiasi kikubwa hivyo! Mimi sio mchaga lakini nataka raisi wa Tanzania mzalendo, mwenye maadili mema, mwaminifu, mchukia ufisadi na dhuluma, mtetezi wa maskini, mwenye itikadi safi n.k. bila kujali kabila wala dini yake wala kanda anayotoka!
 
Similar Discussions

7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom