mwanatanu
JF-Expert Member
- Jan 22, 2008
- 851
- 127
Nimependa sana msimamo wa Dr Mpango kwenye hili suala la makontena ya samani. Kusimamia katika kile unachokiamini, kutokubali kumnyenyekea mtu ambaye yupo kwa ajili ya maslahi fulani ya kwake binafsi na ni ya muda mfupi tu.
.
Kweli kabisa Dr Mpango alijilipua yaani alikuwa amekasirika sana hata ukiona video ile anaongea mpaka unaona mshipa juu ya jicho la kulia lacheza.
Nadhani ingawaje dhana ni mbaya lakini jinsi alivyoongea kwenye clip na kusema yuko tayari kujiuzulu kuna kitu nyuma ya pazia ambalo limemkera sana tena sana.
Halafu media house zote zilikosa kuandika kuwa yuko tayari kujiuzulu ambayo kwangu niliona ni habari nzito zaidi.
Nani yuko nyuma ya PAZIA ndio kitu cha kujiuliza