Msimamo Wa Chama Huenda Ukatawala Mjadala Wa Richmonduli

Shukurani

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
253
11
HOFU YANGU NI MSIMAMO WA CHAMA KUTAWALA WAKATI WA MAJADILIANO

Wabunge CCM wajipaga kuikabili joto la Kashfa ya Richmond
Na Tausi Mbowe, Dodoma
SOURCE: MWANANCHI

WABUNGE wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanakutana leo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kwa ajili ya kupanga msimamo wa pamoja katika mjadala kuhusu ufisadi unaodaiwa kufanywa kwenye mchakato wa zabuni ya kampuni ya Marekani ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond (RDC).

Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda aliliambia Bunge jana kuwa mkutano huo unafanyika leo saa 2:00 usiku katika Ukumbi wa Pius Msekwa uliopo katika viwanja vya Bunge mjini hapa.

Hata hivyo, Makinda hakutaja ajenda zitakazozungumzwa katika mkutano huo. lakini uchunguzi uliofanywa na Mwananchi umegundu kuwa moja ya ajenda kubwa katika mkutano huo, inahusu ripoti ya uchunguzi wa tuhuma za ufisadi zinazoikabili Richmond, uliofanywa na Kamati Teule ya Bunge.

Kwa mujibu wa Makinda, kikao hicho kilitakiwa kufanyika jana, lakini kikaahirishwa hadi leo bila kutaja sababu hasa za kuahirishwa.?

Waheshimiwa wabunge, naomba niwatangazie wabunge wote wa CCM, kile kikao kilichotakiwa kufanyika leo, hakitakuwapo, kimeahirishwa mpaka kesho saa 2:00 usiku. Hivyo wabunge wote wa CCM mnaombwa kufika bila kukosa kwani kikao hiki ni muhimu sana,? alisema Makinda.

Baadhi ya wabunge wa CCM ambao hawakutaka kutaja majina yao, waliliambia Mwananchi kuwa kikao hicho kinalenga kuwaunganisha wabunge wa chama

hicho ili kuondoa mgawanyiko mkubwa uliodhidhirika miongoni mwao na wawe na kauli moja kwa yale yatakayojitokeza kwenye ripoti hiyo.?

Hawa watu wanataka kutufanya sisi ni watoto wadogo. Tunachotaka ni ripoti yetu tuijadili. Suala la nguvu ya chama kutetea masuala ya kitaifa sasa limepitwa na wakati. Mambo ya chama yasichanganywe kabisa na maslahi ya taifa,? alisema mbunge mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.

Habari za awali, ziliarifu kuwa wabunge wote wangegaiwa ripoti hiyo ili waweze kuisoma kabla ya kuijadili kwa undani, lakini Makinda jana hakuzungumzia suala hilo kabisa.

Hata hivyo, mwandishi wa habari hii alipomfuata ofisini kwake kwa ajili ya kupata ufafanuzi juu ya suala hilo, Naibu Spika kupitia Katibu wake, alisema masuala yote yanayohusu Richmond yatazungumzwa leo bungeni yeye mwenyewe akiwapo.

Jana Spika Sitta alikuwa akifanya kikao na kamati ya uongozi kuongelea mustakabali wa Richmond.

Wakati huo huo, Makinda alisema kwamba leo saa tisa, Rais Kikwete anarajiwa kuwasili Dodoma na kuwataka wabunge watakaopenda kwenda kumpokea kufanya hivyo.

Hata hivyo, hakueleza Rais Kikwete anakwenda kufanya nini Dodoma, lakini vyanzo vya habari vinasema kwamba anakwenda kusimamia kikao cha kiutendaji na kikao cha Baraza la Mawaziri.

Katika hatua nyingine, Wabunge jana walipitisha kwa kauli moja azimio la kumpongeza Rais Kikwete kufutia kuchaguliwa kwake kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU).

Azimio hilo lililowasilishwa na Mbunge wa Ilala Mussa Azzan kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje pamoja na mambo mengine lilimpongeza Rais

Kikwete kufutia ushindi huo kufutia imani kubwa ilioonyeshwa na viongozi wa Bara la Afrika.

Kwa mujibu wa azimio hilo, uchaguzi wa Rais Kikwete ni heshima kwa Watanzania wote na kwamba ni lazima kuuezi kwa vitendo ili aweze kufanya kazi aliyotumwa na wakuu hao ipasavyo.

Wakichagia azimio hilo, Mubunge wa Sumbawanga Mjini, Paul Kimiti alisema tatizo bado kubwa kwa viongozi kwani bado ni wachafu na kwamba wanashika vitabu vitakatifu na kuapa huku mikono yao ikiwa ni michafu.

Kimiti pia alisema kuwa ni lazima viongozi kuhakikisha wanapambana na ufisadi bila woga ili kuhakikisha maisha ya wananchi yanakuwa mazuri.


Alisema Rais Kikwete ni mtu anayesimamia haki na harakati za demokrasia katika bara la Afrika na kwamba kazi hiyo aliinza zamani tangu akiwa mdogo wakati akisoma katika shule mbalimbali.


Naye Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Hamadi Rashid alimpongeza Rais Kikwete, lakini akasema kuwa pongezi hizo ziende kwa vitendo na viashiria vinavyoweza kuleta amani katika nchi yetu na kutoa mfano wa ufisadi na migogoro.


Kiongozi huyo alisema Rais Kikiwete anapaswa kupongezwa kwa kuwa ni kiongozi pekee katika Bara la Afrika aliyetamka hadharani na kukubali kuwa nchini mwake kuna matatizo ya kisiasa na kukubali kushirikiana na vyama vya upinzani.


?Huu ni mfano wa kuigwa kwa Rais wetu ni kiongozi pekee ambaye amekubali katika nchi yake kuna matatizo ya kisiasa viongozi wengine wanapaswa kuja kwetu

kujifunza, katika Bara la Afrika mambo haya huyakuti popote ni Tanzania pekee,? alisema.


Naye Mbunge wa Mtera (CCM), John Malecela aliwataka Watanzania kuacha kulalamika pindi Rais atakapokuwa anasafiri sana na kuongeza kuwa ni lazima wakubali kubeba mzingo wa matumizi kwa kuwa ni lazima ataongeza matumizi yake kwa kiasi kikubwa.


Malecela pia aliwataka wapinzani kuacha kualalamika na kukubali kubebeka na kuufafanisha upinzani ni sawa na mototo asiyebebeka na mzazi wake na badala yake

anatoa miguu nje.


Naye Mbunge wa Peramiho CCM, Jenista Muhagama alisema kuwa heshima iliyolewatwa na Rais Kikwete si ya kwake peke yake bali niya Bunge nzima na wananchi wote, hivyo ili kumuenzi ni lazima wananchi wamuunge mkono kwa vitendo na kuiletea heshima

nchi.


Akihitimisha azimio hilo Azzan alisema kuwa Afrika ni bara tajiri na kwamba migogoro inaletewa kwa makusudi na mataifa ya
 
iri naro arierewekegi. sirichama rao rinamijitu imejazanaga kwenyeribunge. siinajazaga miviti pira kuwaga namisapapu. inakengenuwaga midomo na kupigaga riusingizi. inangojaga kupigaga mikula mure iondokage,
 
Akihitimisha azimio hilo Azzan alisema kuwa Afrika ni bara tajiri na kwamba migogoro inaletewa kwa makusudi na mataifa ya

Kama kawaida yetu tunakataa ku'take responsibility for our action.' Lazima tutafute mchawi!
 
iri naro arierewekegi. sirichama rao rinamijitu imejazanaga kwenyeribunge. siinajazaga miviti pira kuwaga namisapapu. inakengenuwaga midomo na kupigaga riusingizi. inangojaga kupigaga mikula mure iondokage,

Acha utoto !!!!!
 
Msimamo wa sisiemu ya leo ni kuamua kusafisha chama kwa kuwatoa kafara Lowassa na wezi wenzake ili kurudisha imani iliyopotea ya Watanzania kwa chama chao na serikali yao. Hawawezi kufa na tai shingoni na kuwapa mtaji akina Slaa na wapinzani wenzake.
Kama kuna kosa ambalo sisiemu hawawezi kulifanya katika siasa basi ni la kuidharau ripoti hii na kuifanyia usanii wa kuzima bila kufanya chochote.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom