Msimamo wa Chama cha Siasa vs Mawazo Binafsi ya Mwanachama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msimamo wa Chama cha Siasa vs Mawazo Binafsi ya Mwanachama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MsandoAlberto, Feb 12, 2011.

 1. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  WanaJF,

  Kumekuwa na mkanganyiko au kutokuelewa kwa faida na hasara, mipaka na nafasi ya mawazo binafsi ya wanachama wa siasa.

  Imekuwa ni kawaida kwa Mbunge wa CDM, CUF, TLP au NCCR kusema jambo na kuonekana amenunuliwa na CCM simply kwa sababu neno lake linapingana na msimamo jumla wa chama.

  Ni kipindi gani Mbunge anaruhusiwa kutoa mawazo yake? Ni kwa kiasi gani Mbunge anaweza kupingana na msimamo wa chama chake?

  Je ni athari kiasi gani inawezakutokea kwa hali hiyo kuwepo?

  Uhuru wa kutoa mawazo unaishia baada ya chama kutoa msimamo wake? Kwa mfano, mwanaCDM kusema waziwazi kwamba si sahihi kutoka kwenye vikao (mimi sisemi sio sahihi) atakuwa amepotoka au amenunuliwa?

  Inawezekana kama chama kimepiga kura kuhusu jambo fulani na kura ya wengi ikapita ni makosa kutoa msimamo tofauti? Najaribu kuangalia kura ya wingi sio guarantee kwamba msimamo ni sahihi! Ukizingatia kura zetu Tanzania zinategemea ushawishi (pursuasion) kuliko mtu anachoamini (conviction).

  Tuelimishane kwa mujibu wa uelewa wetu.
   
Loading...