Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Ndugu Waandishi wa habari,mnamo Mwaka 2014 Serikali kupitia Waziri wake wa Elimu wakati huo ,ndugu Shukuru Kawambwa ilitangaza kuanzishwa kwa Program Maalumu ya Stashahada ya Elimu ( Special Diploma in Education).
Serikali kupitia uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma ( UDOM) walikubaliana na wahadhiri wa chuo hicho kufundisha Vijana hawa wa stashahada ya Ualimu na kwamba wangelipwa shilingi million moja (1,000,000) kwa kila somo kwa Semester.
Ndugu Waandishi wa habari ni kwa muda wa wiki tatu sasa kumekuwa na mgomo wa wahadhiri wa UDOM na mgomo huu wa Wahadhiri umesababisha Takribani wanafunzi 7108 nao kuanza maandalizi ya kugoma kuingia darasani bila kufundishwa.
Uongozi wa chuo ulipokea agizo haramu lisilo na hata chembe ya huruma kutoka kwa Waziri wa elimu na mafunzo ya Ufundi Professor Joyce Ndalichako la kuwa ondoa chuoni Wanafunzi hawa ndani ya masaa 24 chini ya ulinzi mkali wa jeshi la Polisi.
BAVICHA inapenda kuhoji mambo makubwa ya fuatayo.
* Hivi wanafunzi hawa walijipeleka wenyewe chuoni na sio mpango wa Serikali??
* Hivi wanafunzi hawa walituma maombi ya kusomeshwa UDOM ??
* Hivi wanafunzi hawa wamekosa nini?? Kwani wao ndio waliwaambia Wahadhiri wagome??
* Kati ya Wanafunzi na Serikali nani mwenye kosa linalohitaji uwajibikaji??
* Hivi kuna kosa gani kubwa lilopelekea wanafunzi hawa kupelekewa magari,ya Polisi,Mbwa na risasi za moto??
* Hivi nani wa kuwajibika kati ya Wanafunzi na Wizara ya elimu??.
Baraza la vijana ( BAVICHA) tunalaani vikali maamuzi ya hovyo yaliofanywa na Serikali kandamizi ya Ccm pamoja na Uongozi wa Chuo Kikuu cha UDOM.
Serikali ilipaswa kuona ni namna gani walipaswa kuwa ondoa Wanafunzi hao lakini utaratibu waliotumia ni wakinyama na unapaswa kulaaniwa na kila Mtanzania,
Watanzania wanapaswa kujua asilimia kubwa ya Wanafunzi waliofukuzwa ni watoto wa Masikini wasioijua kesho yao huko waendako na hii ni dalili ya wazi kuwa Serikali imeshindwa kutetea hoja yake ya kuwa saidia Masikini wa nchi hii.
BAVICHA tunaitaka Serikali ya Ccm itambue kuwa madai ya walimu wa chuo Kikuu cha UDOM ni ya msingi na yanapaswa kusikilizwa na kufanyiwa kazi haraka na Waache tabia ya kujitoa ufahamu kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao.
BAVICHA tunaitaka Serikali kuagiza ofisi ya mkaguzi wa hesabu za Serikali afanye uchunguzi wa matumizi, ya fedha za chuo kikuu cha UDOM na kufanya "Leadership screening" kwani kumekuwa na hombwe kubwa la uongozi katika chuo hicho.
MASWALA YA BUNGE
BAVICHA tumesikitishwa na kushangazwa na kauli iliyotolewa na Naibu Spika wa Bunge la jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoona swala la UDOM kuwa ni tatizo na linapaswa kujadiliwa Bunge.
Tunawapongeza Wabunge wa UKAWA pamoja na baadhi ya Wabunge wa ccm waliojitoa kwa hali na mali kuwa saidia Wanafunzi na vijana wenzetu wa UDOM waliofanywa wakimbizi na Serikali ya Ccm ndani ya nchi yao.
BAVICHA inasikitishwa sana na Mwenendo wa Bunge linavyoendelea hivi sasa kwa kutozingatia misingi ya sheria na utawala bora kwa kuzidi kufanya ukandamizaji wa Wabunge wa vyama vya upinzani.
BAVICHA tunaitaka Serikali ya Ccm chini ya Magufuli kufuata misingi ya haki,Demokrasia na utawala bora ili kuleta ustawi wa jamii tunayoitaka na kama hayo hayatawezekana,
BAVICHA litaandaa na kuongoza maandamano yasiyo na kikomo ya vijana wote nchi nzima ili kudai yafuatayo,.
1.Utawala wa sheria
2.Utawala Bora
3.Uhuru wa vyombo vya habari
4.Uhuru wa Bunge kuoneshwa Live kwa wwanachi wote
Tunawataka viongozi wote wa BAVICHA nchini kuanza maandalizi ya kupokea na kutekeleza maagizo tutakayo yatoa kwa hatua za awali kupinga Udikteta unaofanywa na watawala.
Imetolewa na,
Idara ya habari na Mawasiliano
BAVICHA Taifa.