Msimamo: Sitashiriki Misa ya Christmas kwenye kanisa ninalolishiriki miaka yote kwa vile halipigi vita utekaji

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,562
217,891
Baada ya kutafakari kwa muda mfupi nimefikia hitimisho kwamba kuanzia leo sitashiriki ibada zote kwenye kanisa ninaloshiriki siku zote na nililozoeleka kuabudu baada ya kanisa hilo kufumbia macho utekaji unaofanywa nchini mwetu.

Kanisa hili ni miongoni mwa makanisa ambayo watuhumiwa wa utekaji husali pia, nimeamua kujiondoa kwa hofu ya kumchukiza Mungu kwa kushirikiana madhabau na wanaonyooshewa vidole na wananchi huku kanisa langu na viongozi wake wakinyamazia, natambua kwamba dhambi ya kushirikiana na wenye tuhuma hizi itanikabili mimi binafsi mbele za Mungu bila Mchungaji au baba Paroko kunisaidia, najua wapo wanaosema nisali kwa ajili ya Mungu na si kwa ajili ya binadamu, lakini wamesahau kujiuliza kwanini maeneo matakatifu kama makanisa yalianzishwa.

Sitashiriki misa kwenye kanisa linalonyamazia dhambi kwa sababu MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI.
 
Hongera mkuu. Niliacha kushiriki ibada ya sanamu na kushirikiana na hao wanaobariki ukatili tangu 2015.

Nimekua na amani sana kutokushiriki mkate na divai na hao waaminio kutesa na kudhulumu watu ni sifa
 
Hongera mkuu. Niliacha kushiriki ibada ya sanamu na kushirikiana na hao wanaobariki ukatili tangu 2015. Nimekua na amani sana kutokushiriki mkate na divai na hao waaminio kutesa na kudhulumu watu ni sifa
Asante sana
 
Siku hizi hadi viongozi wadini wameingia woga dhidi ya sweikali. Yani awamu yatano inaogopwa kuliko shetani ambaye wanamuhubiri
 
Hongera mkuu. Niliacha kushiriki ibada ya sanamu na kushirikiana na hao wanaobariki ukatili tangu 2015.

Nimekua na amani sana kutokushiriki mkate na divai na hao waaminio kutesa na kudhulumu watu ni sifa
Kwani wewe unatofauti gani na shetani mkuu?
 
Ntakuwa zangu chini ya mti shambani kwa babu namshukuru muumba kwa kunipa uhai hadi kuelekea mwisho wa mwaka. Karibu sana tuungane
 
Back
Top Bottom