Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,571
- 217,925
Baada ya kutafakari kwa muda mfupi nimefikia hitimisho kwamba kuanzia leo sitashiriki ibada zote kwenye kanisa ninaloshiriki siku zote na nililozoeleka kuabudu baada ya kanisa hilo kufumbia macho utekaji unaofanywa nchini mwetu.
Kanisa hili ni miongoni mwa makanisa ambayo watuhumiwa wa utekaji husali pia, nimeamua kujiondoa kwa hofu ya kumchukiza Mungu kwa kushirikiana madhabau na wanaonyooshewa vidole na wananchi huku kanisa langu na viongozi wake wakinyamazia, natambua kwamba dhambi ya kushirikiana na wenye tuhuma hizi itanikabili mimi binafsi mbele za Mungu bila Mchungaji au baba Paroko kunisaidia, najua wapo wanaosema nisali kwa ajili ya Mungu na si kwa ajili ya binadamu, lakini wamesahau kujiuliza kwanini maeneo matakatifu kama makanisa yalianzishwa.
Sitashiriki misa kwenye kanisa linalonyamazia dhambi kwa sababu MSHAHARA WA DHAMBI NI MAUTI.