Uchaguzi 2020 Msimamizi Msaidizi Kata ya Ambureni agoma kutoa Fomu ya Rufaa kwa aliowakata, asema wazifuate kwa Mwenyekiti wa NEC Dodoma, amgomea hata DED

mumburya

JF-Expert Member
Mar 19, 2012
321
448
Huyu msimamizi ana nyodo sana, jana kakataa kuwateua wagombea Udiwani wa Vyama vya Upinzani ikiwemo CHADEMA na ACT.

Anadai kuwa hawakulipa shilingi elfu 5 za ada ya kugombea wakati risiti wanazo na waliambatanisha.

Ikiwa imesalia chini ya saa 1 KWA AJILI YA RUFAA, bado hataki kutoa fomu ya rufaa hata baada ya wagombea kwenda wilayani kwa Msimamizi na kuagiza wapewe, yeye anasema fomu za rufaa zifuateni DODOMA.

Je, huyu mtu nani anamlinda? Je, yupo juu ya Sheria? na je Sheria inasemaje kama mkata rufaa kanyimwa fomu ya rufaa na mrufaniwa?
 
Mahakama ya Rufaa iwajibike kwa maamuzi yake ya kipuuzi, kesi ya kupinga wakurugenzi wasiwe wasimamizi wa uchaguzi mahakama Kuu ilikubali kwamba hakuna usawa wala haki, lakini mahakama ya Rufaa chini ya Jaji Mkuu ikasema kwamba hakuna shida kwa kuwa eti wasimamizi wa uchaguzi yaan ma-DED hula viapo vya kuacha uchama....haya sasa ona toka jana jinsi walivyoharibu zoezi zima la uchaguzi majimbo mengi
 
Mahakama ya Rufaa iwajibike kwa maamuzi yake ya kipuuzi, kesi ya kupinga wakurugenzi wasiwe wasimamizi wa uchaguzi mahakama Kuu ilikubali kwamba hakuna usawa wala haki, lakini mahakama ya Rufaa chini ya Jaji Mkuu ikasema kwamba hakuna shida kwa kuwa eti wasimamizi wa uchaguzi yaan ma-DED hula viapo vya kuacha uchama....haya sasa ona toka jana jinsi walivyoharibu zoezi zima la uchaguzi majimbo mengi
Mahakama chini ya Ccm nao ni wapuuzi wengine. Angalia mienendo yao kesi.. Ni ya hovyo na upendeleo ulio dhahiri. Ukiangalia mienendo ya kesi hapo Kenya na Tanzania ni kifo na usingizi. Utajiuliza hivi hawa majaji na mahakimu wa Tanzania wameokotwa wapi.
 
NEC ingekuwa na watumishi sijui wa CIA au FBI ndo ingetenda haki ila hawa wachumia tumbo wa tanganyika vilio havitaisha milele maana wanatii mamlaka za juu
 
Ifike mahali sasa NEC iwe na watumishi wake yenyewe. Hii kuazima hawa mbwa ni tatizo kubwa
NEC hawako serious. Ingekuwa wote wanaofanya upuuzi kama huu inawachukulia hatua ya kupigwa life time ban ya kusimamia uchaguzi wowote pamoja na kuwapeleka Mahakamani wangekoma. Na baaada ya hapo NEC yenyewe ingepokea fomu hizo na kuongeza muda wa kuwasilisha fomu kwa wengine ambao labda walikatishwa tamaa. NEC wangefuta matokeo yeyote ambako pameonekana figisu zikifanyika wazi wazi, ingewaonyesha wanaowachezea kuwa hawana mzaha.

Amandla....
 
Sheria ni mkononi, kama wao wanavyojichukulia sheria mkononi. Haishi angani wala jupiter, anaishi mtaani, hebu acheni kulalamika.

Mtalalamika leo hivi, kesho vile, keshokutwa mtalala na mtaamka maisha yataendelea kama kawaida. Ifike pahali watu waheshimiane, nahimiza tena, fanyeni kitu
 
Back
Top Bottom