Msimamizi mkuu wa uchaguzi Igunga adhihirisha kuipigia chepuo CCM!

analysti

JF-Expert Member
Aug 24, 2009
729
612
Hi every body, nilikuwa nikisikiliza kutangazwa kwa mshindi wa uchaguzi mdogo huko igunga, nikapigwa na butwaa pale msimamizi mkuu wa uchaguzi alipomtangaza kafumu kuwa kashinda na kisha akapiga kelele IGUNGA HOYEEEEEEEEEEE!!!!

Mashabiki wa CCM wakaitikia Hoyeeee!!.

Ndugu wana JF Mimi concern yangu hapa ni picha anayotuonyesha huyu bwana, Ni kwamba anajidhihirisha kabisa kuwa amefurahia haya matokeo, ikiwa na maana kuwa kabla ya uchaguzi angelipenda yawe hivi, hivyo basi ni dhahiri kuwa yeye kama msimamizi mkuu wa uchaguzi amehakikisha matokeo haya yamekuwa kama yalivyo, kitu kinacho tuondolea imani na uhalisia wa matokeo haya.

Nahitimisha kwa kusema kuwa, msimamizi mkuu wa uchaguzi wa Igunga ameudhihirishia umma kuwa yeye ni shabiki wa CCM kinyume na Kanuni zinavyomtaka msimamizi mkuu wa uchaguzi awe!!!!
 
Huyo unayemsikia magayane ni mhaya misifa na ni ccm damu, anakashfa kibao zikiwemo za sexual harrasment kwa wafanyakazi wa halmashauri lakini anatetewa na wakubwa tena amekuwa akijigamba kwamba yuko beneti na raisi. Kwa hiyo amini usiamini magayane amefanya kweli aliyotumwa na mzee wa g unit
 
Hakika mwisho wa Cku CCM itakuja kujibu mbele ya Ocampo!!, Tusubiri tu. Siku inakuja watakapokuja kulia na kusaga meno!! Waacheni waone watu wote ni wapumbavu!!
 
Hi every body, nilikuwa nikisikiliza kutangazwa kwa mshindi wa uchaguzi mdogo huko igunga, nikapigwa na butwaa pale msimamizi mkuu wa uchaguzi alipomtangaza kafumu kuwa kashinda na kisha akapiga kelele IGUNGA HOYEEEEEEEEEEE!!!! Mashabiki wa CCM wakaitikia Hoyeeee!!. Ndugu wana JF Mimi concern yangu hapa ni picha anayotuonyesha huyu bwana, Ni kwamba anajidhihirisha kabisa kuwa amefurahia haya matokeo, ikiwa na maana kuwa kabla ya uchaguzi angelipenda yawe hivi, hivyo basi ni dhahiri kuwa yeye kama msimamizi mkuu wa uchaguzi amehakikisha matokeo haya yamekuwa kama yalivyo, kitu kinacho tuondolea imani na uhalisia wa matokeo haya. Nahitimisha kwa kusema kuwa, msimamizi mkuu wa uchaguzi wa Igunga ameudhihirishia umma kuwa yeye ni shabiki wa CCM kinyume na Kanuni zinavyomtaka msimamizi mkuu wa uchaguzi awe!!!!
Mkuu Analysti nilikuwa nasikiliza hayo matokeo kupitia Radio One na kwa kweli hata mimi kitendo chake kushangilia kilinistaajabisha sana. Hizi ndizo aina za watu wenye dhamana juu ya mustakabali wa maendeleo ya taifa hili.
Lakini naamini mfumo uliopo unaruhusu mienendo ya aina hii kuwepo, laiti kama kazi hizo zingekuwa za kuomba na kufanyiwa usaili na kisha kupewa mkataba naamini hawa vibaraka wasingebweteka namna hiyo.
Nchi hii inaangamia kila siku ipitayo.
 
Wayahudi wanasema hakuna buyu la pesa lilikaa katikati ya mlango miaka 100 bila kudondoka kisa kamba ikiwa imezeeka na kuzidiwa kwa uzito .Pia kumbuka kila muosha maiti naye kuna siku ataoshwa .Sasa basi ngojeni mtajionea .
 
I was as well puzzled by such partiality from Magayane. Despite much emotions he might have had, he could have reserved his joy till he was behind camera. For political fanatics this is an indication of our weak political and administrative institutions.
 
Huyu Magayane ninaweza kumfananisha na Alfred Masako: jana walipokuwa wanalipoti matokeo ya awali vituo vya mjini mgombea wa CDM alikua anaongoza kwa kishindo Alfred Masako wa ITV akaanza kubwabwata eti hooo kwa matokeo haya watu wa Igunga msije kuanza kulalamika mara eti hatukuzamilia kumchagua mara hoo hatukujua n.k sasa nilitegemea hayo maneno ataendelea kuyasema leo lkn wala ameishia kuwapongeza wapiga kura wa Igunga. Magayane na Masako wote wanafanyakazi za Chama na si kwa manufaa ya wa-Tanzania
 
Mkuu mimi nilikua mbele ya luninga ni kweli kabisa haya unayosema! Lakini kwajinsi nijuavyo mimi huyu jamaa ni muajiriwa wa serikali ya Magamba sasa tutegemee nini kwenye kupanga matokeo na kuyatamka kwa mbwembwe vile? Kamwe asingeweza kuweka kitumbua chake mchanga yoote haya Mungu anajua! Shame on you Magayane and CCM!
 
Tanzania tunahitaji mabadiliko makubwa ya kimfumo. Mambo yanaendeshwa kana kwamba bado tupo chini ya utawala wa chama kimoja.
Juzi nimeshangaa kumwona Kikwete akikutana na tume ya uchaguzi NEC ndani ya Ikulu. Hapa Marekani jambo hilo lisingewezekana kabisa kumwona Obama anakutana na tume inayosimamia uchaguzi wa nchi ndani ya White House. Lakini sijaona mtu aliyeshtushwa na hilo. Tume ya uchaguzi inapaswa kuwa tume huru kabisa kisiasa. Lakini Bongo bado.
 
Huyo unayemsikia magayane ni mhaya misifa na ni ccm damu, anakashfa kibao zikiwemo za sexual harrasment kwa wafanyakazi wa halmashauri lakini anatetewa na wakubwa tena amekuwa akijigamba kwamba yuko beneti na raisi. Kwa hiyo amini usiamini magayane amefanya kweli aliyotumwa na mzee wa g unit

Jambo alilofanya Magayane si la kufurahisha na haliungwi mkono hata kidogo LAKINI jambo hilo kuhusishwa na kabila la WAHAYA pamoja na SEXUAL SCANDALS ni upuuzi mtupu, mwenye hii hoja haelewei analolifanya ktk JF otherwise ni punguani
 
Huyo unayemsikia magayane ni mhaya misifa na ni ccm damu, anakashfa kibao zikiwemo za sexual harrasment kwa wafanyakazi wa halmashauri lakini anatetewa na wakubwa tena amekuwa akijigamba kwamba yuko beneti na raisi. Kwa hiyo amini usiamini magayane amefanya kweli aliyotumwa na mzee wa g unit

ha ha ha ha! mzee wa g unit ...lol yule bishoo tu
 
hi every body, nilikuwa nikisikiliza kutangazwa kwa mshindi wa uchaguzi mdogo huko igunga, nikapigwa na butwaa pale msimamizi mkuu wa uchaguzi alipomtangaza kafumu kuwa kashinda na kisha akapiga kelele igunga hoyeeeeeeeeeee!!!! Mashabiki wa ccm wakaitikia hoyeeee!!. Ndugu wana jf mimi concern yangu hapa ni picha anayotuonyesha huyu bwana, ni kwamba anajidhihirisha kabisa kuwa amefurahia haya matokeo, ikiwa na maana kuwa kabla ya uchaguzi angelipenda yawe hivi, hivyo basi ni dhahiri kuwa yeye kama msimamizi mkuu wa uchaguzi amehakikisha matokeo haya yamekuwa kama yalivyo, kitu kinacho tuondolea imani na uhalisia wa matokeo haya. Nahitimisha kwa kusema kuwa, msimamizi mkuu wa uchaguzi wa igunga ameudhihirishia umma kuwa yeye ni shabiki wa ccm kinyume na kanuni zinavyomtaka msimamizi mkuu wa uchaguzi awe!!!!

kama kuna ushahidi au shaka ya kuchakachua tumuhukumu, lakini kwa kusema igunga hoyeeeeeeeeeeeee siyo kosa labda kama angesema ccm hoyeeeeeeeeeee hapo tungeshika bango kumshambulia. Kumbuka hata viongozi wa vyama shiriki wameridhia matokeo, hivyo yeye kama msimamizi lazima awapongeze wana igunga kujichagulia kiongozi wamtakaye hata kama hatakuwa mzuri basi hiyo hoyeeeeeee yao itageuka na kuwa hoiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii. Usimchukie kwa hilo
 
Hi every body, nilikuwa nikisikiliza kutangazwa kwa mshindi wa uchaguzi mdogo huko igunga, nikapigwa na butwaa pale msimamizi mkuu wa uchaguzi alipomtangaza kafumu kuwa kashinda na kisha akapiga kelele IGUNGA HOYEEEEEEEEEEE!!!! Mashabiki wa CCM wakaitikia Hoyeeee!!. Ndugu wana JF Mimi concern yangu hapa ni picha anayotuonyesha huyu bwana, Ni kwamba anajidhihirisha kabisa kuwa amefurahia haya matokeo, ikiwa na maana kuwa kabla ya uchaguzi angelipenda yawe hivi, hivyo basi ni dhahiri kuwa yeye kama msimamizi mkuu wa uchaguzi amehakikisha matokeo haya yamekuwa kama yalivyo, kitu kinacho tuondolea imani na uhalisia wa matokeo haya. Nahitimisha kwa kusema kuwa, msimamizi mkuu wa uchaguzi wa Igunga ameudhihirishia umma kuwa yeye ni shabiki wa CCM kinyume na Kanuni zinavyomtaka msimamizi mkuu wa uchaguzi awe!!!!

CDM acheni ku mind vitu vidogo, nyie kushindwa kwenu kujipanga na kuwafanya wananchi wakubali sera zenu msimtafute mchawi, jipangeni najua inawauma na aibu mliyoipata , na naamini wengi wenu leo mmejifungia ndani mkilia km watoto wadogo. Yeye kusema Igunga oyeeeeeeeeee kuna shida gani ? angesema ccm oyeeeeeeeeeeeeee hapo ndipo ingekuwa shida
 
nimemshangaa sana jinsi alivolipuka kwa furaha.uko wapi uchaguzi huru na haki?

ULITAKA AFANYEJE? Wa Igunga wamesha amua sasa yeye anune ili iweje? Si lengo lake kumtafuta mshindi? kama mshindi amepatikana si lazima kuwapongeza?

kumbuka maneno ya Zitto wkt akiwa IGUNGA, kuna maneno aliyowaambia wana IGUNGA, hivyo kama hawakumskia, shauri yao, minority waliomwelewa ndio watakaoumia lakini tutegemee wataanza kusambaza elimu ya uraia kwa wenzao wengi ambao bado wako kwenye danger zone ili nao wabadilike wawe wana harakat.

tusimhukumu DED kwa hilo. kama amefanikiwa kumaliza mchakato mzima, anyosababu ya kufurahi kwa kusema IGUNGA oyee hata kama kuna wengine hatujaridhika na CDM kuibuka mshindi. huo ndo ukweli no way out.

Tunastahili kujivunia kwa support kubwa tuliyopata toka kwa wana wa IGUNGA, kama ingeongezeka wiki moja ya kampeni, CCM tungewatupa mbali sana.
 
Mkuu mimi nilikua mbele ya luninga ni kweli kabisa haya unayosema! Lakini kwajinsi nijuavyo mimi huyu jamaa ni muajiriwa wa serikali ya Magamba sasa tutegemee nini kwenye kupanga matokeo na kuyatamka kwa mbwembwe vile? Kamwe asingeweza kuweka kitumbua chake mchanga yoote haya Mungu anajua! Shame on you Magayane and CCM!

ushabiki wa kitu ukizidi, unakuwa kama tahila.

Ni kweli kabisa kuwa mkurugenzi anatokana na wizara ya TAMISEMI, na huwa anapendekezwa na waziri wa TAMISEMI/au walio ndani ya TAMISEMI ambao kwa vyovyote ni MAGAMBA asilimia 100%.

Lakini turudi nyuma, mnataka asemeje? Hivi chukulia wewe ndo msimamizi katika jimbo hilo, na kukosea kwako kidogo means kumwaga damu. Yeye ameepusha hayo, si lazima kuwapongeza wapiga kura waliopiga kura?

kama angesema CCM Hoyeee, tungekuwa na sababu ya kumhukumu lakini kusema IGUNGA hoyeee yuko neutral means ansimama katikati ya waliochagua CCM, CDM na CUF.

TUANDIKE MICHANGO YETU KAMA GT
 
Nadhani hakuna tatizo, amewapongeza wananchi.
Angeshangilia chama hapo maswali yangeongezeka
 
Kumpa mkurugenzi wa halmashauri ndo awe msimamizi mkuu wa shughuli za uchaguzi ni ukiritimba maana yeye ni mwakilishi wa serikali inayoundwa na chama fulani (tawala) so sishangai kama kashangilia maana ni sawa na kesi ya nyani kuiba mahindi unampelekea ngedere ndo awe hakimu unategemea nini? Hivi hamkusikia wanapigwa mkwara na viongozi wa ngazi za juu kuwa mkurugenzi atakae sababisha jimbo lipotee nae hana kazi! sasa kwa mazingira hayo tuseme uchaguzi ni huru na haki na tunashangilia hata wasomi mnaoweza chambua ukweli wa mambo. Mimi si mwanachama wa chama chochote ila nasema ukweli wa mambo maana haya wanayofanyiwa wapinzani ipo siku watafanyiwa CCM na wao walalamike lakini kwa sasa hoja hizi wanaziita kelele za chura, na wanasingizia eti sheria ya uchaguzi ndivyo inavyosema, kwani sheria ni jiwe? Hata jiwe hupondwa na kutoa kokoto. ebu tuwe wakweli na tuipende nchi yetu tuache umimi. kumbuka siku zote muosha uoshwa!!!!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom