Msikilizine Risasi Maulanga anaongea live Star TV

LENGIO

JF-Expert Member
Apr 9, 2012
1,096
508
Huyo Risasi Maulanga anaayejita balozi wa amani anaongea utumbo kwenye Star Tv, eti madiwani na viongozi wanaohama chama kwenda chama kingine washatakiwa na wapewe adhabu kubwa.

Anamsifia raisi Kikwete ni raisi mwenye upeo wa hali ya juu sana. Nafikiri ndio maana mtatiro amekata huo mualiko wa Star Tv na hakika angempiga magumi kwa utumbo anayoögea huyu kada wa CCM.
 
Risasi Mwaulanga anajitangaza na kujitapa kwamba ni "BALOZI WA AMANI." nimebahatika kuona akichangia mada sehemu mbalimbali na hata kwenye vyombo vya habar. Tatizo lake kubwa yupo ki shabiki haonekani akitetea aman anayojitangazia. Hivi kweli anastahili hii sifa anayojipa?
 
mandieta. Amejitangaza mwanachama wa ccm bado anajipa cheo cha ubalozi wa "amani" huu sio unafiki?
 
Last edited by a moderator:
Lile ni gamba maarufu ..mara zote yeye humtetea jakaya..ukisikiliza mijadala yake ni kuwaponda wapinzani tu..watu kama wale huwa nia yao ni kuja kuteuliwa kama akina mbatia..si kuna yule mwenzake naye alikuwa mahiri kwenye kuwatetea magamba kipindi cha midahalo ya katiba ambaye alikuwa anazomewa lakini hakomi..mwisho juzi juzi hapa aliteuliwa kuwa kamishna wa madini.mjini hapa.
 
Ni mpuuzi sana huyo bwana, yupo pale kutafuta fadhira za chama, hana jipya zaidi ya kubwabwaja huku akijiita Mwanaharakati wa Amani duuh! STAR TV NEXT TIME MSIFANYE MADUDU YA KUMLETA HUYO BWANA TENA, HANA HOJA ZAIDI YA PROPAGANDA.
 
Huyo Risasi Mwaulanga atakuwa anajipendekeza kwa JK ili ateuliwe kuwa mkuu wa wilaya,hana lolote huyo.
 
Huyo risasi maulanga anaayejita balozi wa amani anaongea utumbo kwenye star tv.eti madiwani na viongozi wanaohama chama kwenda chama kingine washatakiwa na wapewe adhabu kubwa.na anamsifia raisi kikwete ni raisi mwenye upeo wa hali ya juu sana.nafikiri ndio maana mtatiro amekata huo mualiko wa star tv na hakika angempiga magumi kwa utumbo anayoögea huyu mshenzi kada mpuuzi wa ccm.
Kaka Pole sana. Kumsikiliza mpuuzi kama huyo jamaa ukitegemea utapata lolote la maana toka kwenye kinywa chake ni sawa na Umeingia choo cha kike. Huyo mpuuzi ni Full kujipendekeza kwa Jk. Halafu inasemekana waungwana "wanapumzika" hapo.
 
Mchumia tumbo huyo! nilimsikilizaga mara moja tu kipindi cha mgomo wa madaktari akanichefua nikabadilisha chanell...

Nchi hii imejaa wachumia tumbo wengi sana
 
mchakamchakani, nakubaliana na wewe kwenye hili kwani anavyochangia si kama mtu anaetaka amani bali ni mnafki mwenye lengo la kulijaza tumbo lake na wala si amani kama anavojigamba
 
Last edited by a moderator:
Watu wengi hapa TZ njaa inawasumbua sana,anaganga njaa na kutegemea labda naye siku moja atapewa tuzo kama mbatia,sielewi watu wa aina hii 2015 wataficha wapi sura zao.Juzi nimeshangaa vijana wasomi kabisa wanaotegemewa hawana aibu wanaenda kwa nape heti kushinikiza mawaziri wajiudhuru,niliwashangaa sana na usomi wao kwani TV siku hizi hadi vijijini,kila mtu anajua hiyo hoja ya mawaziri kujiudhuru ilianzia wapi na muelekeo wake,sasa wao baaada ya kuona muelekeo ni wazi raisi atawaondoa mawaziri wenye tuhuma,sasa na kihehere chao heti wanaandamana ili mwisho wa siku nao wa hesabiwe kuwa walichangia kupiga vita ufisadi,niliwaona ni watoto wadogo sana hasa yule kiongozi wao,wanajidhalilisha kwa umri wao,sisi kwa kabira letu tunaamini kuwa ukiwa mnafiki katika ujana basi ukizeeka unakuwa mchawi.Wangesoma enzi zetu za mzee PANCHI basi ama wangejinyonga kama Revina Mukasa au wangekimbia chuo,wamuulize KALOLA KANASHA- aka Mpingo.
 
Back
Top Bottom