Msikilizeni JK Jamani, Eti Anasema Viongozi Afrika wawe Wabunifu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msikilizeni JK Jamani, Eti Anasema Viongozi Afrika wawe Wabunifu!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Mtoboasiri, May 19, 2011.

 1. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #1
  May 19, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Kikwete-Viongozi Afrika wawe wabunifu

  RAIS Jakaya Kikwete amesema Bara la Afrika lipo hatarini kuwa masikini wa kutupwa kuliko mabara yote duniani ikiwa viongozi wake hawatapata mbinu mpya za kiuongozi za kukabiliana na matatizo.

  Baadhi ya changamoto alizozitaja Rais Kikwete ni mabadiliko ya hali ya hewa, umasikini, kasi ya ongezeko la watu, baadhi ya viongozi kutowajibika, uwazi na mabadiliko ya teknolojia; akisema mambo hayo yatalifikisha Bara hili pabaya yasipofanyiwa kazi.

  Rais Kikwete alikuwa akifungua Mkutano wa Kwanza wa Bodi ya Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute) jijini Dar es Salaam jana ulioratibiwa na Executive Solution na kuitaka taasisi hiyo kuwa kitovu cha mafunzo ya kuwanoa viongozi wa umma katika suala zima la uwajibikaji.

  Ametoa ushauri kwa taasisi hiyo kuwasaidia viongozi kujifunza kutokana na uzoefu wa uongozi imara kwa Bara la Amerika na Ulaya na kuiga mbinu za kiuchumi kwa nchi zilizofanikiwa katika kama China, India, Brazil, Korea Kusini, Singapore na sasa Afrika Kusini.

  “Ni matumaini yangu kuwa, mafunzo yatakayotolewa na taasisi hii, yatawahusu pia viongozi wa nje ya Tanzania. Natoa wito kwa viongozi wote wa Afrika, kuimarisha uongozi wao kwa kupata utaalamu mpya kuimarisha uongozi bora kwa umma,” amesema Rais Kikwete.

  Katika kuonesha kuwa Serikali imedhamiria viongozi wake na wa mataifa mengine kufaidi matunda ya taasisi hiyo, alisemaSerikali imetoa ekari 400 kuwezesha ujenzi wa taasisi hiyo mapema iwezekanavyo.

  Kuhusu ongezeko la watu, Kikwete amesema, licha ya maendeleo yanayoonekana kwa kuwa na amani, utawala wa sheria na haki za binadamu, ongezeko la watu linakodiriwa kufikia bilioni 1.7 mwaka 2050 kutoka bilioni moja hivi sasa, liwe sababu ya maendeleo na si umasikini.

  Amesema, taasisi hiyo kupitia Bodi ya Wakurugenzi, ina kazi ya kuhakikisha viongozi wa umma na sekta binafsi wanapata mafunzo madhubuti na Tanzania inakuwa kiini cha mafanikio yake na ya Afrika katika kuzalisha viongozi watakaosimamia ipasavyo ukuaji wa uchumi, huduma za jamii na kutimiza malengo ya millennia.

  Awali kabla ya kumkaribisha Rais Kikwete, Mwenyekiti wa Bodi, Ritva Koukku-Ronde kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland, alisema lengo la taasisi hiyo ni kuwajengea uwezo viongozi wa Afrika katika suala la uwajibikaji ili kuleta maendeleo yenye tija yanayotokana na sera madhubuti.

  Koukku-Ronde amesema, Malengo ya Maendeleo ya Milenia hayawezi kufikiwa bila uongozi imara na kuongeza kuwa programu za mafunzo zitakazotolewa zitazingatia masuala ya utawala wa sheria, uwazi, uwajibikaji, mgawanyo wa madaraka na rasilimali, ushiriki wa sekta binafsi kama chachu ya maendeleo kwa wananchi ambayo ni msingi wa uongozi bora.

  Ofisa Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo, Profesa Joseph Semboja alisema imeshaanza kutoa mafunzo kwa viongozi kuanzia ngazi ya wakurugenzi tangu mwaka jana, lakini mpaka kufikia mwaka 2013, watakuwa wamekamilisha ujenzi wa majengo katika eneo la ekari 400 walilopewa na Serikali mjini Bagamoyo.

  Kuanzishwa kwa taasisi hiyo kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Finland kumekuja baada ya mabadiliko ya Chuo cha Uongozi IDM-Mzumbe cha Serikali mkoani Morogoro kuwa Chuo Kikuu na hivyo Serikali kutokuwa na taasisi kama hiyo nchini.
   
 2. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #2
  May 19, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 740
  Trophy Points: 280
  Sawa,yeye kabuni nini kwa taifa lake?Porojo.
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  May 19, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Code:
   
  Baadhi ya changamoto alizozitaja Rais Kikwete ni mabadiliko ya hali ya hewa, umasikini, kasi ya ongezeko la watu, baadhi ya viongozi kutowajibika, uwazi na mabadiliko ya teknolojia; akisema mambo hayo yatalifikisha Bara hili pabaya yasipofanyiwa kazi. 
  
  
  
  Sasa rais anaposema hayo, si anawakatisha watu tamaa?
  Kutaja matatizo tu siyo ujanja!...Changamoto bila mikakati ni bure wee ******!
   
 4. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #4
  May 19, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Hivi yeye ameonesha ubunifu upi vile?
   
 5. MJINI CHAI

  MJINI CHAI JF-Expert Member

  #5
  May 19, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 587
  Trophy Points: 280
  Wewe ulitaka aseme nini?.... kama kiongozi ulitaka anyamaze tu?...........Vitu vingine bana havina mashiko.......kwa waelewa wa mambo ni maneno mazuri ambayo viongozi wanatakiwa kuyafanyia kazi.............USIKURUPUKE
   
 6. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #6
  May 19, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Hopeless Kikwete, Poor Kikwete sio wakuonewa huruma hajui kuwa katika hao Criminal wanaoibia wananchi wao Africa kuwa na yeye ni mmoja wao?
   
 7. luckyperc

  luckyperc JF-Expert Member

  #7
  May 19, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 496
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  kwanini asikurupuke wewe...!!!!
   
 8. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #8
  May 19, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Viongozi wepi? yeye naye si kiongozi! lazima atoe suluhisho! naye anaongea kama wananchi wakawaida huo ni ujinga na wewe unasaport!
   
 9. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #9
  May 19, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Point! Wakati mwingine Great Thinkers wanajisahau, JK anao uhuru wa kusema kilichopo moyoni, kwani hayo ndiyo yanayoisumbua Africa na Tanzania, bravo JK!
   
 10. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #10
  May 19, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Bora angenyamaza hakuna cha msingi alichoongea ni unafiki mtupu....
  JK, JK, JK... Be sincere; be brief; be seated.
   
 11. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #11
  May 19, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Hata yeye ni mbunifu jamani. Hamuoni semina elekezi zikiendelea pamoja na migao ya umeme? Ndio ubunifu anaouongelea huo
   
Loading...